WELCOME TO TANZANIA NATIONAL ASSEMBLY OFFICIAL BLOG: CONTACT US: P.O.BOX 941 DODOMA, TANZANIA, WEBSITE: parliament.go.tz , FIND US ON FACEBOOK >>> www.facebook.com/bungetz1, FOLLOW US ON TWITTER >>> @bunge_tz.>>>KARIBUNI

Wednesday, July 20, 2016

UFAFANUZI KUHUSU TAARIFA ILIYOTOLEWA NA GAZETI LA JAMHURI KUHUSU OFISI YA BUNGE





RAIS ALIPOGAWA MADAWATI YALIYOTENGENEZWA BAADA YA OFISI YA BUNGE KUBANA MATUMIZI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akipokea Dawati kutoka kwa Naibu Spika wa Bunge Dkt. Tulia Ackson kwa ajili ya kuyagawa kwa Waheshimiwa Wabunge katika Viwanja vya Karimjee, Jijini Dar es Salaam.


Rais Dkt John Pombe Magufuli na Viongozi wengine wa Kiataifa wakiwa katika picha ya pamoja na Makamishina wa Tume ya Utumishi ya Bunge mara baada ya kugawa Madawati yaliyotengezwa kwa fedha zilizopatikana baada ya Ofisi ya Bunge kubana matumizi.

Wanafunzi wa shule ya Msingi Bunge wakipakia Madawati tayari kuyapeleka shuleni kwao baada ya Rais kuyagawa

Naibu Spika wa Bunge Dkt Tulia Ackson (kulia) akimuonesha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli Madawati ili aweze kuyagawa kwa Waheshimiwa Wabunge

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akikagua Madawati yaliyotengenezwa baada ya Ofisi ya Bunge kubana matumizi.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiendelea kukagua Madawati yaliyotengenezwa baada ya Ofisi ya Bunge kubana matumizi.

Rais Dkt John Pombe Magufuli akimkabidhi Mwenyekiti wa Bunge Mhe. Mussa Azzan Zungu (Mb) Madawati kwa niaba ya Wabunge wote. Madawati hayo yametengenezwa kutokana na fedha zilizopatikana baada ya Ofisi ya Bunge kubana matumizi.

Rais Dkt John Pombe Magufuli (kulia) pamoja na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa (katikati) na Naibu Spika wa Bunge Dkt Tulia Ackson katika picha ya pamoja wakiwa wamekalia Madawati kabla ya kuyagawa kwa Waheshimiwa Wabunge.

Monday, July 4, 2016

UZINDUZI WA BUNGE LA VIJANA BUNGENI MJINI DODOMA.

Mkuu wa Kitengo cha Habari, Elimu na Mawasiliano Ofisi ya Bunge, Owen Mwandumbya akihutubia alipokuwa akizundua rasmi Bunge la Vijana la mwaka 2016, katika Ukumbi wa Pius Msekwa, mjini Dodoma jana. Mkutano huo ni wa tatu toka kuanzishwa kwa Bunge la Vijana chini ya mradi Legislatures Support Project(LSP).

Spika wa Bunge la Vijana, Regnald Massawe (kulia) kutoka Chuo cha Uhasibu Arusha akila kiapo mbele ya Katibu wa bunge hilo, Agness Mwamanda kutoka Chuo cha Mzumbe baada ya kuanza kwa mkutano wa tatu wa Bunge la Vijana la mwaka 2016, mjini Dodoma

Spika wa Bunge la Vijana, Regnald Massawe (kushoto) kutoka Chuo cha Uhasibu Arusha akimuapisha Stella Wadson-kutoka Chuo cha Ustawi wa Jamii kuwa Naibu Spika wa Bunge hilo baada ya kuanza kwa mkutano wa tatu wa Bunge la Vijana la mwaka 2016, mjini Dodoma.

Wabunge wa Bunge la Vijana la mwaka 2016, kutoka Vyuo mbalimbali vya Elimu ya Juuu wakila kiapo cha utii baada ya kuanza kwa mkutano wa tatu wa bunge hilo, mjini Dodoma.
Sekretarieti ya Bunge la Vijana na Viongozi wa Bunge la Vijana (waliokaa mbele) wakiwa katika picha ya Pamoja na Wabunge wa Bunge la mwaka 2016, mara ya uzinduzi wa Bunge hilo uliofanyika katika Ukumbi wa Pius Msekwa. Mkutano huo ni wa tatu toka kuanzishwa kwa Bunge la Vijana chini ya mradi Legislatures Support Project(LSP).