WELCOME TO TANZANIA NATIONAL ASSEMBLY OFFICIAL BLOG: CONTACT US: P.O.BOX 941 DODOMA, TANZANIA, WEBSITE: parliament.go.tz , FIND US ON FACEBOOK >>> www.facebook.com/bungetz1, FOLLOW US ON TWITTER >>> @bunge_tz.>>>KARIBUNI

Monday, March 17, 2025

KAMATI YA BUNGE YA ELIMU, UTAMADUNI NA MICHEZO YARIDHISHWA NA MRADI WA UKARABATI NA UPANUZI WA CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM




















Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Elimu, Utamaduni na Michezo wameridhishwa na mradi wa Ukarabati na Upanuzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam wakati walipofanya ziara ya kukagua Ukarabati na Upanuzi wa Chuo hicho.


Ziara ya kukagua Ukarabati na Upanuzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam imefanyika leo tarehe 17 Machi, 2025 Jijini Dar es Salaam.


Akizungumza wakati wa ziara hiyo, Mwenyekiti wa Kamati, Mhe. Husna Sekiboko ameipongeza Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan kwa utayari na utashi wake wa Maendeleo.


“Serikali ya Rais Samia Kupitia Wizara ya Fedha imetoa kiasi cha sh. Bil 9.4 ambazo ni sehemu ya mtiririko wake wa Fedha wanazozitoa kwa ajili ya Maendeleo na ndio maana ukarabati na upanuzi unaenda kwa haraka” alisema Mhe. Sekiboko


Aidha, amewapongeza wanafunzi wote waliosoma Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kwa mchango waliotoa ambao ni kiasi cha sh. bil. 4.4 ambazo zimechochea Maendeleo kufanyika kwa haraka.


Akizungumzia kauli ya mtu mwenye digrii kwenda kusoma VETA, Mhe. Sekiboko alisema mtu yoyote anaweza kwenda VETA kuongeza ujuzi, kama taifa tunapaswa kushukuru na kujivunia tuichukulie ile kauli kama ya kujenga kwa kuwa tukishajifunza, tunapata ujuzi na tunaitawala dunia.


Kwa Upande wake Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, alisema Serikali wamejikita katika ujenzi wa hosteli za wanafunzi ili kuangalia namna ya kupunguza changamoto za wanafunzi za sehemu za kuishi.


Ameongeza, Kama Serikali tunampango wa kusomesha wahadhiri zaidi ya 1,000 ili kuhakikisha tunakuwa na watu wenye ujuzi zaidi ambayo ni chachu ya elimu bora Chuoni hapa na Maendeleo ya Taifa kwa ujumla.


Naye Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Prof. William Anangisye alisema majengo ya Chuo ni juhudi za Rais Samia Suluhu Hassan baada ya kusikia na kuona changamoto iliyopo hivyo kutoa fedha kwa wakati.


Vile vile, uwepo wa Baraza la Chuo Kikuu limechochea ujenzi mpaka kufika hatua hii kwa ushauri, mawazo na msukumo wao uliochochea Maendeleo Chuoni hapo.

Saturday, March 8, 2025

WATUMISHI WA OFISI YA BUNGE WATOA ELIMU YA UMMA KUHUSU BUNGE MKOANI MTWARA












Watumishi wa Ofisi ya Bunge wakitoa elimu ya umma kuhusu Bunge kwa Shule ya Sekondari ya Mtwara Sisters, Shule ya Sekondari ya Ufundi Mtwara na Shule ya Sekondari ya Shangani zilizopo Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara, Mkoa wa Mtwara tarehe 26 Februari, 2025.