WELCOME TO TANZANIA NATIONAL ASSEMBLY OFFICIAL BLOG: CONTACT US: P.O.BOX 941 DODOMA, TANZANIA, WEBSITE: parliament.go.tz , FIND US ON FACEBOOK >>> www.facebook.com/bungetz1, FOLLOW US ON TWITTER >>> @bunge_tz.>>>KARIBUNI

Monday, December 23, 2019

WABUNGE WAHUDHURIA MAADHIMISHO YA MIAKA 60 YA TANAPA NA HIFADHI YA NGORONGORO WILAYANI SERENGETI

Makamu wa Rais, Mhe. Samia Suluhu akimkabidhi Mwenyekiti wa Wabunge Walemavu na wadau wa Utalii Mhe. Riziki Lulida Cheti cha Utambulisho wa kutambua mchango wa Wabunge hao kwenye Sekta ya Utalii nchini wakati wa  maadhimisho ya miaka 60 ya Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) na eneo la Hifadhi ya Ngorongoro kwenye Viwanja vya Fort Ikoma Wilayani Serengeti hii leo.

Wabunge wanaounda Umoja wa Wabunge wenye Ulemavu nchini pamoja na Wabunge wengine wakiwa katika picha ya pamoja na Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu na baadhi ya mawaziri kwenye Maadhimisho ya miaka 60 ya Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) na eneo la Hifadhi ya Ngorongoro kwenye Viwanja vya Fort Ikoma Wilayani Serengeti hii leo.

Wabunge wanaounda Umoja wa Wabunge wenye Ulemavu Tanzania wakiwa na wawakilishi wengine wa makundi ya Walemavu wakionyesha Vyeti walivyotunukiwa na Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu kwa kutambua mchango wao kwenye sekta ya Utalii hapa nchini wakati wa Maadhimisho ya miaka 60 ya Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) na eneo la Hifadhi ya Ngorongoro kwenye Viwanja vya Fort Ikoma Wilayani Serengeti hii leo.

Friday, December 13, 2019

KIKAO CHA TATHIMINI YA MRADI WA LSP II CHAFANYIKA MJINI BAGAMOYO

Mratibu wa Mradi wa Kulijengea Bunge Uwezo (LSP II), Mary Laswai akitoa mada  kuhusu utekelezaji wa Mradi huo kwa mwaka 2019 katika Kikao cha Tathimini ya utekelezaji wa Mpango kazi wa mradi kwa Mwaka 2019. Pembeni yake ni Mshauri Mkuu wa Mradi, Ndugu Takawira Musavengana. Kikao hicho kimefanyika leo Mjini Bagamoyo.Kikao hicho pia kitapitia Rasimu ya Mpango Kazi wa Mradi wa mwaka 2020.

Mshauri Mkuu wa Mradi wa Kulijengea Bunge Uwezo (LSP II), Ndugu Takawira Musavengana akisisitiza jambo katika Kikao cha Tathimini ya utekelezaji wa Mpango kazi wa mradi kwa Mwaka 2019. Pembeni yake ni  Mratibu wa Mradi huo, Mary Laswai. Kikao hicho kimefanyika leo Mjini Bagamoyo ambapo pia wajumbe watapitia Rasimu ya Mpango Kazi wa Mradi wa mwaka 2020.

Wajumbe wa Kikao cha Tathimini ya utekelezaji wa Mpango kazi wa Mradi wa Kulijengea Bunge Uwezo (LSP II) wakiwa katika kikao kilichofanyika leo hii Mjini Bagamoyo. Kikao hicho pia Kitapitia Rasimu ya Mpango Kazi wa Mradi wa mwaka 2020.

Baadhi ya wajumbe wa Kikao cha Tathimini ya utekelezaji wa Mpango kazi wa Mradi wa Kulijengea Bunge Uwezo (LSP II) wakiwa katika kikao kilichofanyika leo hii Mjini Bagamoyo. Kikao hicho pia Kitapitia Rasimu ya Mpango Kazi wa Mradi wa mwaka 2020.