WELCOME TO TANZANIA NATIONAL ASSEMBLY OFFICIAL BLOG: CONTACT US: P.O.BOX 941 DODOMA, TANZANIA, WEBSITE: parliament.go.tz , FIND US ON FACEBOOK >>> www.facebook.com/bungetz1, FOLLOW US ON TWITTER >>> @bunge_tz.>>>KARIBUNI

Friday, July 15, 2022

SPIKA DKT. TULIA AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA BALOZI POLEPOLE JIJINI LILONGWE


Spika wa Bunge, Mhe. Dkt. Tulia Ackson akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili katika ofisi za Ubalozi wa Tanzania nchini Malawi.




Spika wa Bunge, Mhe. Dkt. Tulia Ackson akizungumza na Balozi wa Tanzania nchini Malawi, Mhe. Humphrey Polepole (kushoto) alipomtembelea Ubalozini hapo Jijini Lilongwe. Wengine ni Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania walioambatana na Mhe. Spika


Balozi wa Tanzania nchini Malawi, Mhe. Humphrey Polepole akiwasilisha taarifa ya Mahusiano baina ya Tanzania na Malawi mbele ya Spika wa Bunge, Mhe. Dkt. Tulia Ackson (kulia) katika ofisi za Ubalozi huo Jijini Lilongwe nchini Malawi. Wengine ni Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania walioambatana na Mhe. Spika



Spika wa Bunge, Mhe. Dkt. Tulia Ackson akipokea taarifa ya Mahusiano baina ya Tanzania na Malawi kutoka kwa Balozi wa Tanzania nchini Malawi, Mhe. Humphrey Polepole alipomtembelea Ubalozini hapo Jijini Lilongwe.


Spika wa Bunge, Mhe. Dkt. Tulia Ackson akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Tanzania nchini Malawi, Mhe. Humphrey Polepole alipotembelea Ubalozini hapo Jijini Lilongwe.

Spika wa Bunge, Mhe. Dkt. Tulia Ackson akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Tanzania nchini Malawi, Mhe. Humphrey Polepole (kulia kwake) alipotembelea Ubalozini hapo Jijini Lilongwe. Kuanzia kushoto ni Wabunge wa Bunge la Tanzania walioambatana na Mhe. Spika ambao ni Mhe. Selemani Zedi, Mhe. Hawa Mwaifunga, Mhe. Kassim Haji, Mhe. Shally Raymond na Mhe. Dkt. Alfred Kimea.



Spika wa Bunge, Mhe. Dkt. Tulia Ackson akiongozana na Balozi wa Tanzania nchini Malawi, Mhe. Humphrey Polepole mara baada ya mazungumzo yaliyofanyika Ubalozini hapo Jijini Lilongwe.




SPIKA DKT. TULIA ATEMBELEA BUNGE LA MALAWI










 Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson aungana na Maspika wa Mabunge ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika kutembelea Bunge la Malawi lililopo Jijini Lilongwe.

Wednesday, July 13, 2022

SPIKA DKT. TULIA ATOA WITO WA KUFUNGAMANISHA SEKTA ZA KILIMO NA NISHATI


Spika wa Bunge la Tanzania Mhe. Dkt. Tulia Ackson ametoa wito kwa nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) kufungamanisha sekta za kilimo na nishati kupitia mikakati mbalimbali ya kukuza uchumi inayotekelezwa kwenye nchi hizo.

 

Akizungumza leo katika Mkutano Mkuu wa 51 wa Jukwaa la Mabunge ya SADC, unaoendelea Jijini Lilongwe nchini Malawi, Dkt. Tulia amebainisha umuhimu wa kufungamanisha sekta hizo ili ziwezeshe ukuaji wa uchumi katika ukanda wa SADC.

 

“Endapo tunahitaji nchi zetu ziweze kujitegemea kwenye suala la usalama wa chakula, tunapaswa kujifunza kupitia nchi zingine zilizofanikiwa katika sekta hii kama zilivyoainishwa kwenye taarifa ya kamati ya Chakula.”

 

 “Tunapaswa kuweka kipaumbele kwenye miundombinu wezeshi itakayosaidia kukuza sekta ya kilimo, kama ni sekta ya nishati basi twende pamoja kama Jumuiya kuhakikisha inakuza kilimo chetu,” amesema.

 

Akitolea mfano nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Mhe. Spika amesema “Nakubaliana na wenzetu wa Kongo kuwa mradi wa umeme wa maji wa Inga unaweza kutoa umeme kwa nchi zote za SADCna hivyo kusaidia katika juhudi za kukuza sekta ya kilimo.”

 

Dkt. Tulia amewaomba wajumbe wa Mkutano huo kuweka nguvu kwenye maeneo mengine ya kiuchumi yatakayofungamanishwa ili kukuza sekta ya kilimo kabla ya kufikiria kupata wawekezaji wakubwa watakaokuja kuwekeza katika sekta hiyo. 

 

Aidha, Dkt. Tulia ametoa wito kwa wajumbe hao kuzishauri nchi zao kuondoa vikwazo katika biashara ya mazao mbalimbali yanayozalishwa kwa wingi miongoni mwa nchi hizo kama sehemu ya juhudi za kukuza sekta ya kilimo.

Kadhalika, Mhe.Spika ameshauri kuimarishwa kwa ushirikiano wa biashara baina ya nchi hizo ili kuhakikisha kunakuwapo na soko la uhakika kwa mazao yanayozalishwa na wakulima.

 

“Iwapo nchi mojawapo katika ukanda huu inazalisha kwa wingi zao fulani, kwanini nchi zingine wanachama zisiiunge mkono kwa kununua zao hilo badala ya kwenda kununua katika nchi zilizo nje ya Jumuiya ya SADC,kwa kufanya hivyo tutatengeneza soko la ndani la bidhaa za kilimo,”amesema

 

Awali, Mjumbe wa Jukwaa hilo na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya SADC PF ya Chakula, Kilimo na Maliasili, Mhe.Ishmael Onani amewasilisha Taarifa ya Kamati hiyo iliyobeba Kaulimbiu ya Ushiriki wa Mabunge katika ujenzi wa mifumo imara ya kilimo kupitia usimamizi wa fedha za umma. 

 

Amesema, pamoja na ukweli kwamba kilimo ni kati ya sekta muhimu za kukuza uchumi na kupunguza umaskini lakini kumekuwa na uwekezaji mdogo kwenye sekta hiyo jambo linalosababisha ukuaji hafifu wa uchumi kwa nchi za SADC. 

SPIKA DKT. TULIA AWAONGOZA WAJUMBE WA JUKWAA LA MABUNGE YA JUMUIYA YA MAENDELEO KUSINI MWA AFRIKA KUTOKA BUNGE LA TANZANIA KATIKA MKUTANO WA 51 WA SADC – PF NCHINI MALAWI














 Matukio katika Picha yaliyojiri leo Julai 13, 2022 wakati Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson akiwaongoza Wajumbe wa Jukwaa la Mabunge ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC – PF) kutoka Bunge la Tanzania katika Mkutano wa 51 wa SADC – PF unaoendelea katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Bingu Jijini Lilongwe nchini Malawi.

Tuesday, July 12, 2022

SPIKA DKT. TULIA AONGOZA WABUNGE WA TANZANIA KATIKA MKUTANO WA 51 WA SADC – PF




Spika wa Bunge, Mhe. Dkt. Tulia Ackson akichangia mada kuhusu mwelekeo wa upatikanaji wa nishati ya uhakika, endelevu na inayojitosheleza katika Ukanda wa Kusini mwa Afrika wakati wa Mkutano wa 51 wa Jukwaa la Mabunge ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC – PF) katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Bingu Jijini Lilongwe nchini Malawi, leo Julai 12, 2022.

Katika Mkutano huo, Mhe. Spika ameambatana na Wajumbe wa Jukwaa hilo kutoka Bunge la Tanzania ambao ni Mhe. Selemani Zedi, Mhe. Shally Raymomd, Mhe. Hawa Mwaifunga, Mhe. Dkt. Alfred Kimea na Mhe. Haji Kassim.


Wajumbe wa Jukwaa la Mabunge ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC – PF) kutoka Bunge la Tanzania wakishiriki katika Mkutano wa 51 wa SADC – PF wenye mada kuhusu mwelekeo wa upatikanaji wa nishati ya uhakika, endelevu na inayojitosheleza katika Ukanda wa Kusini mwa Afrika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Bingu Jijini Lilongwe nchini Malawi, leo Julai 12, 2022. Kuanzia kushoto ni Mhe. Shally Raymond, Mhe. Selemani Zedi, Mhe. Hawa Mwaifunga, Mhe. Dkt. Alfred Kimea na Mhe. Haji Kassim





 

SPIKA DKT. TULIA ACKSON ASHIRIKI MKUTANO WA 51 WA SADC – PF LILONGWE NCHINI MALAWI.











Matukio katika picha yaliyojiri wakati Spika wa Bunge, Mhe. Dkt. Tulia Ackson akishiriki ufunguzi wa Mkutano wa 51 wa Jukwaa la Mabunge ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC – PF) katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Bingu Jijini Lilongwe nchini Malawi.

Katika Mkutano huo, Mhe. Spika ameambatana na Wajumbe wa Jukwaa hilo kutoka Bunge la Tanzania ambao ni Mhe. Selemani Zedi, Mhe. Shally Raymomd, Mhe. Hawa Mwaifunga, Mhe. Dkt. Alfred Kimea na Mhe. Haji Kassim.

 

SPIKA DKT. TULIA AKUTANA NA RAIS WA MALAWI JIJINI LILONGWE


Spika wa Bunge, Mhe. Dkt. Tulia Ackson akisalimiana na Rais wa Jamhuri ya Malawi, Mhe. Dkt. Lazarus Chakwera walipokutana katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Bingu Jijini Lilongwe nchini Malawi.

Mhe. Spika yupo nchini humo kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa 51 wa Jukwaa la Mabunge ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC – PF).


 Spika wa Bunge, Mhe. Dkt. Tulia Ackson akiwa katika picha ya pamoja na Rais wa Jamhuri ya Malawi, Mhe. Dkt. Lazarus Chakwera (katikati) na Spika wa Bunge la Malawi, Mhe. Catherine Gotani Hara (kulia) walipokutana katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Bingu Jijini Lilongwe nchini Malawi.

Mhe. Spika yupo nchini humo kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa 51 wa Jukwaa la Mabunge ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC – PF).

Sunday, July 10, 2022

SPIKA DKT. TULIA AMEKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA BALOZI POLEPOLE NCHINI MALAWI

Spika wa Bunge, Mhe. Dkt. Tulia Ackson akizungumza na Balozi wa Tanzania Nchini Malawi, Mhe. Humphrey Polepole baada ya kuwasili leo Julai 10, 2022 katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kamuzu uliopo Lilongwe nchini humo.

Mhe. Spika atashiriki Mkutano wa 51 wa Jukwaa la Mabunge ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC – PF) utakaoanza tarehe 11 hadi 16 Julai, 2022 katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Bingu (BICC) Jijini Lilongwe.





 

Friday, July 1, 2022

BUNGE WATEMBELEWA NA WAGENI MBALIMBALI KATIKA VIWANJA VYA SABASABA

Maafisa wa Bunge wakiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe. Stergomena Tax alipotembelea Bunge katika viwanja vya sabasaba Jijini Dar-es-salaam.

Kaimu Balozi wa Jamhuri ya kislamu ya Iran Mhe. Hossein Alvandi Bahineh akisani kitabu cha wageni


Wanafunzi wa shule mbalimbali watembelea banda la Bunge liliopo katika viwanja vya sabasaba jijini Dar-es-salaam