WELCOME TO TANZANIA NATIONAL ASSEMBLY OFFICIAL BLOG: CONTACT US: P.O.BOX 941 DODOMA, TANZANIA, WEBSITE: parliament.go.tz , FIND US ON FACEBOOK >>> www.facebook.com/bungetz1, FOLLOW US ON TWITTER >>> @bunge_tz.>>>KARIBUNI

Friday, September 28, 2018

BUNGE LA EALA NA BUNGE LA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WATOA RAMBIRAMBI KUFUATIA AJALI YA MV NYERERE

Spika wa Bunge  Mheshimiwa Job Y. Ndugai (Mb), (kushoto) akimsilikiliza Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki  Mheshimiwa Alhaji Adam Kimbisa. Mheshimiwa Kimbisa amkabidhi Mhe. Spika kiasi cha Shillingi Milioni Nane Laki tano na elfu Hamsini kwa niaba ya Wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki ikiwa ni rambirambi kufuatia ajali ya kivuko cha Mv Nyerere. Kulia ni Katibu wa Bunge Ndg. Stephen Kagaigai.


Spika wa Bunge akisisitiza jambo mbele ya wanahabari baada ya kupokea  rambirambi kutoka kwa Wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki (EALA) Shilling i Milioni Nane Laki Tano na Hamsini elfu ikiwa ni rambirambi kufuatia ajali ya kivuko cha Mv Nyerere zilizowasilishwa na Mheshimiwa Alhaji Adam Kimbisa (kushoto) .Bunge la Jamahuri ya Muungano pia limetoa rambirambi yake  kiasi cha Sh. milioni 86
 
Spika wa Bunge  Mheshimiwa Job Y. Ndugai (Mb), akipokea shilingi Milioni Nane Laki tano na Elfu Hamsini kutoka kwa Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki Mheshimiwa Alhaji Adam Kimbisa kwa niaba ya Wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki ikiwa ni rambirambi kufuatia ajali ya kivuko cha Mv Nyerere. Bunge la Jamahuri ya Muungano pia limetoa rambirambi yake  kiasi cha Sh. milioni 86

WABUNGE WA TANZANIA WAHUDHURIA SEMINA YA KUJENGEWA UWEZO NCHINI CHINA

Mheshimiwa Fredy Mwakibete ambaye ndiye Mwenyekiti wa Msafara huo wa wabunge akitoa neon la shukrani baada ya kumalizika kwa semina hiyo. Semina ilikuwa inahusu kupeana mikakati mbalimbali ya kuweza kufanikisha malengo 17 ya millennia. Wabunge walipata kujifunza kutoka China ambao wamekuwa mara zote walitimiza malengo ya millennia kwa wakati.
Mheshimiwa Kiza Mayeye akichangia mada katika semina hiyo. Semina hiyo iliwakilishwa na nchi saba za bara la Afrika na Asia.
Kushoto katika picha ni Mheshimiwa Maida Abdallah, akifuatiwa na Mheshimiwa Munira Khatib, Mheshimiwa Kiza Mayeye, Mheshimiwa Joram Hongoli na mwisho kulia ni Mheshimiwa Fredy Mwakibete.


Monday, September 24, 2018

WABUNGE WA TANZANIA WATEMBELEA BUNGE LA CHINA

Wabunge wa Tanzania wakiwa ndani ya Bunge la China. Wabunge hao katika picha ni Mheshimiwa Fredy Mwakibete, Mheshimiwa kiza Mayeye, Mheshimiwa Maida Mustafa, Mheshimiwa Joram na Mheshimiwa M,unira Mustafa. Waheshimiwa hao wapo katika ziara ya mafunzo ya jinsi China wanavyotumia mikakati mbalimbali katika kutimiza malengo ya milenia.hii ni semina ya tatu kufanyika nchini humo na nchi saba zilishiriki.
Wabunge wa Tanzania wakiwa katika ziara ya mafunzo nchini China, wamepata nafasi ya kutembelea Bunge la China Beijing. Wabunge hao walialikwa na Bunge la China kufanya ziara katika Bunge lao.

Wednesday, September 12, 2018

WANAFUNZI WAZURU BUNGENI KUPATA ELIMU KUHUSU BUNGE

Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Kamati za Bunge Ndg. Dickson Bisile akitoa elimu kwa Wanafunzi kutoka Shule ya Jumapili ya Kanisa la Moravian Jimbo la Dodoma waliotembelea Bunge kwa lengo la kujifunza Shughuli mbalimbali zinazofanywa na Mhimili wa Bunge.
Afisa wa Bunge Ndg. Stanslaus Yusufu akifafanua jambo mbele ya Wanafunzi kutoka Shule ya Jumapili ya Kanisa la Moravian Jimbo la Dodoma waliotembelea Bunge kwa lengo la kujifunza Shughuli mbalimbali zinazofanywa na Mhimili wa Bunge.