WELCOME TO TANZANIA NATIONAL ASSEMBLY OFFICIAL BLOG: CONTACT US: P.O.BOX 941 DODOMA, TANZANIA, WEBSITE: parliament.go.tz , FIND US ON FACEBOOK >>> www.facebook.com/bungetz1, FOLLOW US ON TWITTER >>> @bunge_tz.>>>KARIBUNI

Wednesday, November 15, 2017

WAHARIRI NA WAANDISHI WA MAGAZETI MATATU WAHOJIWA MBELE YA KAMATI YA BUNGE YA MAADILI KWA KOSA LA KUTOA TAARIFA ZINAZOHUSU USHAHIDI NA MWENENDO WA KIKAO CHA KAMATI HIYO BILA KUPATA IDHINI YA BUNGE

  Mhariri  Mtendaji wa Gazeti la Mtanzania Bw. Denis Msacky akijieleza mbele ya Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge Nipashe kwa kosa  la kutoa taarifa zinazohusu ushahidi na mwenendo wa  kikao cha Kamati hiyo bila kupata idhini ya Bunge kitendo ambacho ni kinyume na kifungu cha 34 (1) (f)  na (g) ya Sheria ya Kinga, Madaraka na Haki za Bunge, Sura ya 296.
 Mhariri/Mwandishi wa Habari Gazeti la Mtanzania Bw. Bakari Kimwaga akiapaa kabla ya kuanza  akijieleza mbele ya Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge Nipashe kwa kosa  la kutoa taarifa zinazohusu ushahidi na mwenendo wa  kikao cha Kamati hiyo bila kupata idhini ya Bunge kitendo ambacho ni kinyume na kifungu cha 34 (1) (f)  na (g) ya Sheria ya Kinga, Madaraka na Haki za Bunge, Sura ya 296.
 Mhariri  Mtendaji wa Gazeti la Mwananchi  Bw. Angetile Osiah na Mwanasheria wake mbele ya Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge Nipashe kwa kosa  la kutoa taarifa zinazohusu ushahidi na mwenendo wa  kikao cha Kamati hiyo bila kupata idhini ya Bunge kitendo ambacho ni kinyume na kifungu cha 34 (1) (f)  na (g) ya Sheria ya Kinga, Madaraka na Haki za Bunge, Sura ya 296.
   Mhariri  wa Gazeti la Nipashe   Bw. Edmond Msangi akijieleza mbele ya Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge Nipashe kwa kosa  la kutoa taarifa zinazohusu ushahidi na mwenendo wa  kikao cha Kamati hiyo bila kupata idhini ya Bunge kitendo ambacho ni kinyume na kifungu cha 34 (1) (f)  na (g) ya Sheria ya Kinga, Madaraka na Haki za Bunge, Sura ya 296. 


 Na Debora Sanja

Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge, imewahoji wahariri pamoja Waandishi wa Habari wa Magazeti ya Mtanzania, Mwananchi na Nipashe kwa kosa  la kutoa taarifa zinazohusu ushahidi na mwenendo wa  kikao cha Kamati hiyo bila kupata idhini ya Bunge.

Akizungumza mara baada ya kuwahoji mashahidi hao, Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhe. Almasi Athuman  Maige (Mb) alisema wahusika wote walifika mbele ya Kamati na kujibu tuhuma hizo ambazo ni kinyume na kifungu cha 34 (1) (f)  na (g) ya Sheria ya Kinga, Madaraka na Haki za Bunge, Sura ya 296.

Mheshimiwa Maige alisema Kamati baada ya kuwasikiliza mashahidi wote waliofika itaandaa Taarifa yake na kuiwasilisha kwa Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai.

“Kanuni zimeweka masharti kuwa shughuli za Kamati hii zinazofanywa zitabakia kuwa ni siri hadi hapo itakapomaliza kazi yake na kuwasilisha taarifa Bungeni,” alisema.

Aliwataja waliofika katika Kamati hiyo kuwa ni Ndugu Denis Msaki ambaye ni Mhariri Mtendaji wa gazeti la Mtanzania na mwandishi wake Ndugu Bakari Kimwanga, Ndugu Edmond Msangi Mhariri Mtendaji wa Gazeti la Nipashe na mwandishi wake Ndugu Gwamaka Alipipi na Ndugu Angetile Osiah Mhariri Mtendaji wa gazeti la Mwananchi  na Mwandishi wake Ndugu Elias Msuya.
SPIKA NDUGAI APOKEA TAARIFA YA MKUTANO WA BUNGE LA AFRIKA ULIOFANYIKA KUANZIA TAREHE 6 MPAKA 20 OKTOBA, 2017 NCHINI AFRIKA YA KUSINI

 Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (kushoto) akizungumza na Waheshimiwa Wabunge wa Bunge la Afrika wanaowakilisha Bunge la Tanzania katika kikao kilichofanyika leo ofisini kwake Mjini Dodoma. wa pili kushoto ni Mwenyekiti wa Wabunge wa Tanzania, Mhe. Asha Juma, wa pili kulia ni Mjumbe Mhe. Stephen Masele na kulia ni Mjumbe Mhe. David Silinde.
 Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (wa pili kushoto) akipokea taarifa ya Mkutano wa Bunge la Afrika uliofanyika kuanzia tarehe 6 mpaka 20 Oktoba, 2017 nchini Afrika ya kusini, wakiongozwa na Mwenyekiti wa Wabunge wa Bunge la Afrika wanaowakilisha Bunge la Tanzania, Mheshimiwa Asha Juma (wa pili kulia) katika kikao kilichofanyika leo ofisini kwake Mjini Dodoma. kushoto ni Mjumbe, Mhe. Stephen Masele na kulia ni Mjumbe, Mhe. David Silinde

Monday, November 6, 2017

NAIBU SPIKA DKT. TULIA KATIKA MKUTANO WA KIMATAIFA WA CHAMA CHA JUMUIYA YA MADOLA UNAOFANYIKA MJINI DHAKA, BANGALADESH.

Naibu Spika, Mhe. Dkt Tulia Ackson akiwa katika Mkutano wa Kimataifa wa Chama cha Jumuiya ya Madola unaofanyika Mjini Dhaka, Bangaladesh. Katika Mkutano huo Naibu Spika alitoa mada kuhusu kuwashirikisha vijana kwenye uongozi, Kulia kwake ni Naibu ni Mhe. Kazi Nabil Ahmed, Mbunge Bangladesh, kushoto ni Mhe. Sumitra Mahjan Spika kutoka India.


Naibu Spika, Mhe. Dkt Tulia Ackson akiwa katika Mkutano wa Kimataifa wa Chama cha Jumuiya ya Madola unaofanyika Mjini Dhaka, Bangaladesh. Katika Mkutano huo Naibu Spika alitoa mada kuhusu kuwashirikisha vijana kwenye uongozi, Kulia kwake ni Naibu ni Mhe. Kazi Nabil Ahmed, Mbunge Bangladesh, kushoto ni Mhe. Sumitra Mahjan Spika kutoka India.


Naibu Spika, Mhe. Dkt Tulia Ackson akiwa katika Mkutano wa Kimataifa wa Chama cha Jumuiya ya Madola unaofanyika Mjini Dhaka, Bangaladesh. Katika Mkutano huo Naibu Spika alitoa mada kuhusu kuwashirikisha vijana kwenye uongozi, Kulia kwake ni Naibu ni Mhe. Kazi Nabil Ahmed, Mbunge Bangladesh, kushoto ni Mhe. Sumitra Mahjan Spika kutoka India.

Sunday, November 5, 2017

WAJUMBE WA KAMATI TATU ZA BUNGE WAKIWA KATIKA SEMINA MJINI DODOMA

Ndugu Seraphine Tamba akitoa mada kuhusu Mchakato wa Utungaji Sheria katika Semina ya Wabunge wa Kamati ya Kamati ya Katiba na Sheria, Kamati ya Sheria Ndogo na Kamati Mambo Nje, Ulinzi na Usalama.

Wajumbe wa Kamati tatu za Bunge wakifuatiliana mada kuhusu mchakato wa Utungaji Sheria kutoka kwa Ndugu Seraphine Tamba  katika Semina ya Wabunge iliyofanyika Mjini Dodoma. Wajumbe wa Kamati zilizohudhuria Semina hiyo ni Kamati ya Katiba na Sheria, Kamati ya Sheria Ndogo na Kamati Mambo Nje, Ulinzi na Usalama.

Baadhi ya Wajumbe wa Kamati za Bunge zilizoshiriki Semina kuhusu Mchakato wa Utungaji Sheria wakifuatilia mada katika Semina iliyofanyika Mjini Dodoma.

Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Sheria Ndogo, Mheshimiwa Andrew Chenge akitoa mchango wake Katika Semina ya Wabunge iliyofanyika Mjini Dodoma. Wajumbe wa Kamati zilizohudhuria Semina hiyo ni Kamati ya Katiba na Sheria, Kamati ya Sheria Ndogo na Kamati Mambo Nje, Ulinzi na Usalama.

Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama Balozi Adadi Rajabu akizungumza katika Semina ya Wabunge wa Kamati ya Katiba na Sheria, Kamati ya Sheria Ndogo na Kamati Mambo Nje, Ulinzi na Usalama iliyofanyika Mjini Dodoma.Kushoto kwake ni Mwenyekiti wa Kamati ya Katiba na Sheria Mohamed Mchengelwa