WELCOME TO TANZANIA NATIONAL ASSEMBLY OFFICIAL BLOG: CONTACT US: P.O.BOX 941 DODOMA, TANZANIA, WEBSITE: parliament.go.tz , FIND US ON FACEBOOK >>> www.facebook.com/bungetz1, FOLLOW US ON TWITTER >>> @bunge_tz.>>>KARIBUNI

Thursday, August 18, 2016

UJUMBE WA WABUNGE KUTOKA KOREA WAMTAMBELEA NAIBU SPIKA, DK. TULIA ACKSON LEO OFISINI KWAKE JIJINI DAR ES SALAAM.

Naibu Spika, Dkt. Tulia Ackson akizungumza na Ujumbe wa  Wabunge kutoka Korea ya Kusini walipomtembelea leo ofisini kwake Jijini Dar es Salaam wakiongozwa na Kiongozi wao Won Yoochul wa kwanza kutoka kulia.

 Naibu Spika, Dkt. Tulia Ackson akifurahia zawadi ya Jarida la Watoto kati ya Majarida 125 alilopewa na Ujumbe wa Wabunge kutoka Korea ya Kusini walipomtembelea leo Ofisini kwake Jijini Dar es Salaam, kulia ni Kiongozi wa Ujumbe huo, Won Yoochul. 


Naibu SpikA, Dkt. Tulia Ackson akipokea zawadi ya Taa ya Solar kutoka kwa Kiongozi wa Jumbe wa Wabunge kutoka Korea ya Kusini,Won Yoochul Wabunge hao walimtembelea Naibu Spika leo Ofisini kwake Jijini Dar es Salaam.

Naibu Spika, Dkt. Tulia Ackson na Kiongozi wa Ujumbe wa Wabunge kutoka Korea ya Kusini wakionyesha Jarida la Watoto ambalo Wabunge hao kutoka Korea wamemzawadia Naibu Spika jumla ya Nakala 125 za majarida hayo.


Tuesday, August 16, 2016

MHE RAIS ALIPOENDA KUMJULIA HALI MHE. SPIKA


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana kwa furaha na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Job Ndugai mara baada ya kuwasili nyumbani kwake Sala sala nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam.

Rais wa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Spika wa Bunge Job Ndugai nyumbani kwake Sala sala jijini Dar es Salaam alipokwenda kumjulia hali.


Rais Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Mke wa Spika Dkt. Fatma Mganga Ndugai huku Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akiagana na Spika Job Ndugai mara baada ya kuwajulia hali nyumbani kwao Sala sala jijini Dar es Salaam.
Thursday, August 4, 2016

SPIKA WA BUNGE MHE NDUGAI ALIPOTEMBELEWA NA VIONGOZI MBALIMBALI NYUMBANI KWAKE BAADA YA KUREJEA NCHINI KUTOKA INDIA

Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan akizungumza na Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai alipomtembelea nyumbani kwake Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mke wa Spika Dkt Fatma Mganga. Spika amerejea nchini hivi karibuni kutoka India ambapo alikwenda kwa ajili ya Matibabu


Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai alipomtembelea nyumbani kwake Jijini Dar es Salaam. Spika amerejea nchini hivi karibuni kutoka India ambapo alikwenda kwa ajili ya uchunguzi wa Afya yake.

Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai akizungumza na Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe.Mohamed Chande Othman aliyefika kumsalimia nyumbani kwake Jijini Dar es Salaam. Spika amerejea nchini hivi karibuni kutoka India ambapo alikwenda kwa ajili ya uchunguzi pamoja na matibabu ya afya yake.
Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai akifurahia jambo wakati akizungumza na Waziri Mkuu Mhe Majaliwa Kassim aliyemtembelea nyumbani kwake Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Waziri Ofisi ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana na Walemavu.

Kiongozi wa Kambi rasmi ya Upinzani Bungeni Mhe Freeman Mbowe akizungumza na Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai alipomtembelea nyumbani kwake.

Spika wa Baraza la wawakilishi Zanzibar Mhe. Zubeir Ali Maulid akisalimiana na Spika wa Bunge alipomtembelea nyumbani kwake Jijini Dar es Salaam.

Spika Mstaafu Mhe Anne Makinda akizungumza na Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai alipomtembelea nyumbani kwake Jijini Dar es Salaam.

Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai katikati akizungumza na baadhi ya Wabunge waliomtembelea nyumbani kwake Jijini Dar es Salaam