WELCOME TO TANZANIA NATIONAL ASSEMBLY OFFICIAL BLOG: CONTACT US: P.O.BOX 941 DODOMA, TANZANIA, WEBSITE: parliament.go.tz , FIND US ON FACEBOOK >>> www.facebook.com/bungetz1, FOLLOW US ON TWITTER >>> @bunge_tz.>>>KARIBUNI

Monday, May 31, 2021

ALYEKUWA KATIBU WA BUNGE ALIPOTEMBELEA BUNGE NA KUKABIDHI OFISI KWA KATIBU MPYA

Aliyekuwa Katibu wa Bunge, Ndg. Stephen Kagaigai (kushoto) akabidhi Ofisi kwa Katibu Mpya wa Bunge, Ndg. Nenelwa Mwihambi tukio lililofanyika leo katika ofisi za Bunge Jijini Dodoma.

Aliyekuwa Katibu wa Bunge, Bw. Stephen Kagaigai ambaye aliteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro pamoja na Katibu Mpya wa Bunge, Bi. Nenelwa Mwihambi walipotambulishwa Bungeni. 

Aliyekuwa Katibu wa Bunge, Bw. Stephen Kagaigai ambaye aliteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro pamoja na Katibu Mpya wa Bunge, Bi. Nenelwa Mwihambi walipotambulishwa Bungeni. 

Aliyekuwa Katibu wa Bunge, Bw. Stephen Kagaigai akizungumza na Menejimenti ya Ofisi ya Bunge mara baada ya kukabidhi Ofisi kwa Katibu Mpya, Bi. Nenelwa Mwihambi Jijini Dodoma.


 

Aliyekuwa Katibu wa Bunge, Bw. Stephen Kagaigai na Katibu Mpya, Bi. Nenelwa Mwihambi katika picha ya pamoja na na Menejimenti ya Ofisi ya Bunge mara baada ya makabidhiano ya Ofisi Jijini Dodoma.

SPIKA WA BUNGE MHE. JOB NDUGAI AKUTANA NA KUZUNGUMZA NA BALOZI WA CHINA NCHINI

Spika wa Bunge, Job Ndugai (kushoto) akizungumza na ugeni kutoka Ubalozi wa China nchini (kushoto kwake) ukiongozwa na Balozi wa China nchini Tanzania, Mhe. Wang Ke (wa kwanza kushoto kwake) walipomtembelea leo Ofisini kwake Bungeni Jijini Dodoma. Kulia kwake ni Naibu Spika wa Bunge, Dkt.Tulia Ackson


Spika wa Bunge, Job Ndugai (kushoto) akizungumza na Balozi wa China nchini Tanzania, Mhe. Wang Ke alipomtembelea leo Ofisini kwake Bungeni Jijini Dodoma. 

Spika wa Bunge, Job Ndugai (katikati) katika picha ya pamoja na Balozi wa China nchini Tanzania, Mhe. Wang Ke (kulia) na Naibu Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson alipomtembelea leo Ofisini kwake Bungeni Jijini Dodoma. 

 

BUNGE LA 12 MKUTANO WA TATU KIKAO CHA 40 TAREHE 31.05.2021


 

Thursday, May 27, 2021

BUNGENI 27.05.2021


 

MKUU WA MKOA WA DODOMA, MHE. MTAKA AFIKA OFISINI KWA SPIKA NDUGAI KUJITAMBULISHA

Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai  akizungumza na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mhe. Anthony Mtaka alipofika Ofisini kwake kujitambulisha Jijini Dodoma.

 

Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai  akizungumza na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mhe. Anthony Mtaka alipofika Ofisini kwake kujitambulisha Jijini Dodoma.

 

Spika wa Bunge akiongoza kikao baina ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Anthony Mtaka na Wabunge  wa Mkoa wa Dodoma Ofisini kwake Jijini Dodoma.


 

Tuesday, May 25, 2021

BUNGE LA 12 MKUTANO WA TATU KIKAO CHA 36 TAREHE 25.05.2021


 

KAMATI YA ARDHI, MALIASILI NA UTALII YAPEWA MAFUNZO JUU YA MASUALA YA UMILIKI WA ARDHI

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii Mhe. Aloyce Kwezi akichangia jambo kwenye Mafunzo juu ya mtazamo wa kijinsia katika umiliki wa ardhi hapa nchini yaliyotolewa kwa Wajumbe wa Kamati hiyo kwa ushirikiano baina ya TGNP, WFT na HakiArdhi Jijini Dodoma. 

Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii Mhe. Wakifuatilia jambo kwenye Mafunzo juu ya mtazamo wa kijinsia katika umiliki wa ardhi hapa nchini yaliyotolewa kwa Wajumbe wa Kamati hiyo kwa ushirikiano baina ya TGNP, WFT na HakiArdhi Jijini Dodoma.  

Afisa Mwandamizi wa Program kutoka  TGNP Bi. Anna Sangai(katikati)akifafanua jambo kwenye Mafunzo juu ya mtazamo wa kijinsia katika umiliki wa ardhi hapa nchini yaliyotolewa kwa Wajumbe wa Kamati ya Ardhi, Maliasili na Utalii kwa ushirikiano baina ya TGNP, WFT na HakiArdhi Jijini Dodoma.

 

Friday, May 21, 2021

WATUMISHI OFISI YA BUNGE WAMPOKEA KATIBU MPYA WA BUNGE JIJINI DODOMA


Katibu wa Bunge, Ndg. Nenelwa Mwihambi akipokelewa na Mkurugenzi Msaidizi wa Utawala na Rasilimali Watu Bunge, Ndg. Triphonia Mng’ong’o alipowasili katika viwanja vya Bunge leo Jijini Dodoma.


Watumishi Ofisi ya Bunge wakimpokea kwa bashasha Katibu wa Bunge, Ndg, Nenelwa Mwihambi alipowasili katika viwanja vya Bunge leo Jijini Dodoma.

Katibu wa Bunge, Ndg, Nenelwa Mwihambi (Mwenye maua) katika picha ya pamoja na watumishi wa Ofisi ya Bunge nje ya Ukumbi wa Msekwa Bungeni Jijini Dodoma.


Katibu wa Bunge, Ndg, Nenelwa Mwihambi (katikati mbele) katika picha ya pamoja na Menejimenti ya Ofisi ya Bunge nje ya Ukumbi wa Msekwa Bungeni Jijini Dodoma. Wanne kushoto mbele ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama
 

BUNGENI 21.05.2021


 

Wednesday, May 19, 2021

KATIBU MPYA WA BUNGE, BI. NENELWA MWIHAMBI AAPISHWA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akimuapisha Bi. Nenelwa Mwihambi kuwa Katibu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Katibu wa Bunge, Bi. Nenelwa Mwihambi akiapa kiapo cha Maadili ya Utumishi wa Umma baada ya kuapishwa kuwa Katibu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Ikulu Jijini Dar es Salaam
 Katibu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Bi.  Nenelwa Mwihambi akiapa Ikulu Jijini Dar es Salaam

 

Saturday, May 15, 2021

MHE. RAIS SAMIA AMTEUA BI. NENELWA MWIHAMBI KUWA KATIBU WA BUNGE

 

Katibu wa Bunge, Bi. Nenelwa Mwihambi

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan amemteua  Bi. Nenelwa Mwihambi kuwa Katibu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano  Tanzania.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu, Bi. Mwihambi anachukua nafasi ya aliyekuwa Katibu wa Bunge, Bw. Stephen Kagaigai ambaye ameteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro.

Kabla ya kuteuliwa kuwa katibu wa Bunge Bi. Mwihambi alikuwa ni Mkurugenzi wa Idara ya Shughuli za Bunge.

Aidha, Bi. Mwihambi anakuwa Mwanamke wa kwanza kuteuliwa kuwa Katibu wa Bunge.

Friday, May 14, 2021

Wednesday, May 12, 2021

WATUMISHI WA KITUO CHA AFYA CHA BUNGE WASHEREHEKEA SIKU YA WAUGUZI DUNIANI

Watumishi wa Kituo cha Afya cha Bunge wakiwa Katika picha ya pamoja na Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Rasilimali Watu katika Ofisi ya Bunge, Jane Kajiru wa pili kutoka kushoto mstari wa mwisho.Watumishi hao wamefanya hafla fupi ya kuadhimisha ya Siku ya Wauguzi Duniani 
Watumishi wa Kituo cha Afya cha Bunge wakifurahi keki  pamoja na Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Rasilimali Watu katika Ofisi ya Bunge, Jane Kajiru wa kwanza kutoka kulia .Watumishi hao wamefanya hafla fupi ya kuadhimisha ya Siku ya Wauguzi Duniani
Mganga Mfawidhi wa Kituo cha Afya cha Bunge, Dkt. Germin Temba akizungumza katika hafla fupi ya kuadhimisha Siku ya Wauguzi Duniani iliyoandaliwa na Watumishi wa Kituo hicho, kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Rasilimali Watu katika Ofisi ya Bunge, Jane Kajiru
Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Rasilimali Watu katika Ofisi ya Bunge, Jane Kajiru na Mganga Mfawidhi wa Kituo cha Afya cha Bunge, Dkt. Germin Temba wakipokea maandamano ya wauguzi wa Kituo hicho katika hafla fupi ya kuadhimisha Siku ya Wauguzi Duniani

Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Rasilimali Watu wa katika Ofisi ya Bunge, Jane Kajiru akizungumza katika hafla fupi ya kuadhimisha Siku ya Wauguzi Duniani iliyoandaliwa na Watumishi wa Kituo cha Afya cha Bunge.

Saturday, May 8, 2021

WABUNGE WAPEWA SEMINA JUU YA LISHE KWA WATOTO WADOGO

 

Afisa Mawasiliano wa UNICEF- Tanzania Ndg. Usia Ledama akiwasilisha Mada juu ya Hali ya Watoto Tanzania katika Semina kwa Wabunge iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Msekwa Bungeni Jijini Dodoma. 

Mjumbe wa Kamati ya Utawala na Serikali za Mitaa Mhe. Dkt. Pindi Chana akichangia jambo kwenye Semina juu ya umuhimu wa kushughulikia tatizo la upungufu wa Lishe kwa watoto wadogo. 

Sehemu ya Wajumbe wa Kamati za Huduma na Maendeleo ya Jamii, Bajeti, Masuala ya Ukimwi pamoja na Kamati ya Utawala na serikali za Mitaa wapewa Semina na UNICEF juu ya umuhimu wa kushughulikia tatizo la upungufu wa Lishwe kwa watoto wadogo. 

Friday, May 7, 2021

KAMATI YA ARDHI, MALIASILI NA UTALII PAMOJA NA KAMATI YA UTAWALA NA SERIKALI ZA MITAA YAPOKEA TAARIFA

Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi yawasilisha taaarifa ya utekelezaji wa programu ya Kupanga, Kupima na Kumilikisha Ardhi na Miradi ya Nyumba zinazojengwa na Halmashauri mbalimbali nchini kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na utalii pamoja na Kamati ya Utawala na Serikali za Mitaa leo tarehe 7 Mei katika viwanja vya Bunge Jijini Dodoma.

Kamati ya Ardhi, Maliasili na Utalii pamoja na Kamati ya Utawala na Serikali za Mitaa yapokea taarifa ya utekelezaji wa programu ya Kupanga, Kupima na Kumilikisha Ardhi na Miradi ya Nyumba zinazojengwa na Halmashauri mbalimbali nchini leo tarehe 7 Mei katika viwanja vya Bunge Jijini Dodoma.

 

Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi yawasilisha taaarifa ya utekelezaji wa programu ya Kupanga, Kupima na Kumilikisha Ardhi na Miradi ya Nyumba zinazojengwa na Halmashauri mbalimbali nchini kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na utalii pamoja na Kamati ya Utawala na Serikali za Mitaa leo tarehe 7 Mei katika viwanja vya Bunge Jijini Dodoma.


BUNGE LA 12 MKUTANO WA TATU KIKAO CHA 25 TAREHE 07.05.202
 

Wednesday, May 5, 2021

SPIKA NDUGAI AONGOZA WABUNGE KATIKA FUTARI ILIYOANDALIWA NA BENKI YA CRDB JIJINI DODOMASpika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (katikati) akizungumza na Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela (kushoto) baada ya futari iliyoandaliwa na Benki hiyo kwa Waheshimiwa Wabunge kwenye viwanja vya Bunge jijjini Dodoma,  Kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya CRDB, Ndg. Ally Laay


Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (katikati) akifurahi jambo na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. William Lukuvi (kushoto) katika futari iliyoandaliwa na Benki ya CRDB kwa Waheshimiwa Wabunge kwenye viwanja vya Bunge jijjini Dodoma, Wapili kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya CRDB,Ndg. Ally Laay, Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela (wapili kushoto) na Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mustapha Rajabu.


Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai awaongoza Waheshimiwa Wabunge katika futari iliyoandaliwa na Benki ya CRDB kwenye viwanja vya Bunge jijini Dodoma

Waheshimiwa Wabunge wakishiriki katika futari iliyoandaliwa na Benki ya CRDB kwenye viwanja vya Bunge jijini Dodoma