WELCOME TO TANZANIA NATIONAL ASSEMBLY OFFICIAL BLOG: CONTACT US: P.O.BOX 941 DODOMA, TANZANIA, WEBSITE: parliament.go.tz , FIND US ON FACEBOOK >>> www.facebook.com/bungetz1, FOLLOW US ON TWITTER >>> @bunge_tz.>>>KARIBUNI

Wednesday, January 25, 2017

TAMISEMI yawasilisha taarifa ya ukusanyaji mapato kwa njia ya kielektroniki kwa Kamati

 Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa wakipokea na Kujadili Taarifa ya Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa kuhusu Tathimini ya Mfumo wa Ukusanyaji Mapato kwa njia ya Kielektroniki katika Halmashauri nchini na Utekelezaji wa zoezi la kubaini Wanafunzi hewa katika Shule za Msingi na Sekondari za Serikali nchini.
  Mkurugenzi wa Idara ya  Teknolojia ya Habari na Mawasiliano OR – TAMISEMI, Erick Kitali, akiwasilisha Taarifa ya Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa kuhusu Tathimini ya Mfumo wa Ukusanyaji Mapato kwa njia ya Kielektroniki katika Halmashauri nchini na Utekelezaji wa zoezi la kubaini Wanafunzi hewa katika Shule za Msingi na Sekondari za Serikali nchini mbele ya kamati hiyo.
  Naibu Waziri  OR – TAMISEMI, Mhe. Selemani Jafo akifafanua jambo mbele ya Kamati ya akifafanua jambo mbele ya Kamati hiyo.
Monday, January 23, 2017

KAMATI TATU ZAKUTANA KUJADILI CHANGAMOTO ZA BANDARI

Wajumbe wa Kamati ya Bajeti, Kamati ya Miundombinu na Kamati ya Viwanda, Biashara  na Mazingira wamekutana kwa pamoja leo Mjini Dodoma kujadili changamoto mbalimbali za Bandari.kikao hicho kiliongozwa na wenyeviti ambao ni Profesa Norman Sigala King (Miundombuni) wa katikati ni Dk. Dalay Kafumu (Viwanda, Biashara na Mazingira) na Mhe. Josephat Kandege (Bajeti)
Wajumbe wa Kamati ya Bajeti, Kamati ya Miundombinu na Kamati ya Viwanda, Biashara  na Mazingira wamekutana kwa pamoja leo Mjini Dodoma kujadili changamoto mbalimbali za Bandari.
Wajumbe wa Kamati ya Bajeti, Kamati ya Miundombinu na Kamati ya Viwanda, Biashara  na Mazingira wakifuatilia mjadala katika kikao cha Kamati leo Mjini Dodoma.

Saturday, January 21, 2017

KAMATI YA ARDHI, MALIASILI NA MAZINGIRA YAKAGUA MRADI WA ILMIS

Mjumbe wa Kamati ya Ardhi, Maliasili na Utalii, Mheshimiwa Risala Kabongo akiomba kufafanuliwa jambo wakati Kamati hiyo ilipokuwa ikikagua mradi wa Kusimika Mfumo Unganishi wa Taarifa za Ardhi (ILSMIS) leo Jijini Dar es Salaam, kushoto ni Mwenyekiti wa Kamati, Mheshimiwa Atashasta Nditiye, wengine ni Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Angelina Mabula na wa kwanza kulia ni Mjumbe wa Kamati Mhe. Silafu Maufi

Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii wakikagua mradi wa Kusimika Mfumo Unganishi wa Taarifa za Ardhi (ILSMIS) leo Jijini Dar es Salaam.