WELCOME TO TANZANIA NATIONAL ASSEMBLY OFFICIAL BLOG: CONTACT US: P.O.BOX 941 DODOMA, TANZANIA, WEBSITE: parliament.go.tz , FIND US ON FACEBOOK >>> www.facebook.com/bungetz1, FOLLOW US ON TWITTER >>> @bunge_tz.>>>KARIBUNI

Thursday, November 17, 2016

MAFUNZO KUHUSU TARATIBU ZA UNUNUZI KWA WAFANYAKAZI WA BUNGE

Mhadhiri kutoka Chuo Kikuu cha Mzumbe Ndugu. Paul Nsimbila akitoa mafunzo kuhusu taratibu za Ununuzi  kwa Wakuu wa Idara, Wakuu wa Vitengo na Wajumbe wa Bodi ya Zabuni  katika semina iliyofanyika Ofisi za Bunge Mjini Dodoma

Baadhi ya Wakuu wa Idara, Wakuu wa Vitengo wa Ofisi ya Bunge wakiwa katika semina kuhusu taratibu za ununuzi leo Mjini Dodoma

Wednesday, November 16, 2016

SPIKA NDUGAI AKUTANA NA WADAU WA MAENDELEO KUTOKA NCHI ZA NORDIC      Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai akifafanua jambo mbele ya Wadau wa Maendeleo kutoka Timu ya Ujumbe kutoka Nchi za Nordic uliomtembelea Ofisini kwake Dodoma leo kujionea utekelezaji wa Mradi wa Legislature Support Project II unaotekelezwa na Bunge kwa ufadhili  wa wadau hao kupitia Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP). Ujumbe huo uliongozwa na Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa hapa Nchini Alvaro Rodriguez (Kulia kwake) na Bi. kit Clausen Mshauri Mwandamizi wa Ubalozi wa Denmark katika Umoja wa Mataifa Mjini New York - Marekani.


Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai akimsikiliza Bi. kit Clausen, Mshauri Mwandamizi wa Ubalozi wa Denmark katika Umoja wa Mataifa Mjini New York - Marekani wakati akifafanua jambo wakati wadau hao kutoka Nchi za Nordic walipomtembelea Ofisini kwake Dodoma leo.

Wadau wa Maendeleo kutoka Timu ya Ujumbe kutoka Nchi za Nordic walipomtembelea Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai ofisni kwake leo Mjini Dodoma.

Saturday, November 12, 2016

HATIMAYE MAREHEMU SITTA AZIKWA HUKO URAMBO HUKU, MHE SPIKA AKIUNGANA NA VIONGOZI WENGINE KATIKA MAZISHI HAYO

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Job Y. Ndugai akisalimiana na Mkuu wa mkoa wa Tabora Mhe Aggrey Mwanri mara baada ya kuwasili Mkoani humo kushiriki mazishi ya aliyekuwa Spika wa Bunge la Tisa Marehemu Samuel Sitta.

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Job Y. Ndugai akiwasili Nyumbani kwa aliyekuwa Spika wa Bunge la Tisa Marehemu Samuel Sitta Urambo, Tabora kushiriki mazishi ya Spika huyo Mstaafu.

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Job Y. Ndugai akimsabai Mama wa aliyekuwa Spika wa Bunge la Tisa Marehemu Samwel Sitta, Hajjat Zuwena Fundikira.

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Job Y. Ndugai akimsabai Mjane  aliyekuwa Spika wa Bunge la Tisa Marehemu Samwel Sitta Mhe Magreth Sitta wakati wa mazishi wa Spika huyo Mstaafu.

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Job Y. Ndugai akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa aliyekuwa Spika wa Bunge la Tisa Marehemu Samwel Sitta wakati wa mazishi wa Spika huyo Mstaafu.

Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Tulia Ackson akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa aliyekuwa Spika wa Bunge la Tisa Marehemu Samwel Sitta wakati wa mazishi wa Spika huyo Mstaafu.

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Job Y. Ndugai akitoa salama za rambirambi wakati wa mazishi wa  aliyekuwa Spika wa Bunge la Tisa Marehemu Samwel Sitta

 Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Job Ndugai akiweka shada la maua katika Kaburi la aliyekuwa Spika wa Bunge la Tisa Marehemu Samwel Sitta.

Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Tulia Ackson akiweka shada la maua katika Kaburi la aliyekuwa Spika wa Bunge la Tisa Marehemu Samwel Sitta.

Jeneza lilobeba mwili wa aliyekuwa Spika wa Bunge la Tisa Marehemu Samuel John Sitta likitumbukizwa kaburini wakati wa mazishi yaliofanyika Urambo, Tabora.