WELCOME TO TANZANIA NATIONAL ASSEMBLY OFFICIAL BLOG: CONTACT US: P.O.BOX 941 DODOMA, TANZANIA, WEBSITE: parliament.go.tz , FIND US ON FACEBOOK >>> www.facebook.com/bungetz1, FOLLOW US ON TWITTER >>> @bunge_tz.>>>KARIBUNI

Friday, August 31, 2018

KAMATI YA BAJETI YATEMBELEA VIWANDA SINGIDA

Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti wakiongozwa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mheshimiwa George Simbachawene wakifuatilia Uwasilishwaji wa Taarifa ya utekelezaji wa kazi za Shirika la Maendeleo ya Viwanda Vidogo vidogo (Sido) Mkoa wa Singida kwa kipindi cha mwaka 2016 hadi Juni 2018 katika ziara ya Kamati hiyo iliyoanza hii leo Mkoani humo.
Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti wakiongozwa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mheshimiwa George Simbachawene wakikagua maeneo mbalimbali ya hatua za uzalishaji katika kiwanda cha Mafuta ya Alizeti cha Mount Meru kilichopo Mjini Singida, Kamati hiyo ipo katika ziara ya kutembelea Viwanda mbalimbali Mkoani humo.
Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti wakiashuhudia bidhaa ya mafuta ya Alizeti iliyo tayari kwa ajili ya kupelekwa sokoni walipotembelea Kiwanda cha Mount Meru kilichopo Mjini Singida hii leo.Kamati hiyo ipo katika ziara yake Mkoani Singida.

KAMATI YA LAAC YAANZA ZIARA MKOANI MOROGORO

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Dkt. Stephen Kebwe akizungumza na wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Serikali za Mitaa (LAAC) baada ya Kamati hiyo kumtembelea ofisini kwake leo. Kamati hiyo iko ziara Mkoani Morogoro.

Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC), Mhe. Vedasto Ngombale akizungumza na wajumbe wa kamati hiyo na watendaji wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Morogoro. kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Stephen Kebwe na kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa LAAC, Mhe. Abdallah Chikota. Kamati hiyo ilikwenda kumtembelea Mkuu wa Mkoa kabla ya kuanza ziara yake ya kikazi mkoani humo


Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) wakiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Stephen Kabwe na watendaji mbalimbali wa Mkoa huo.kamati hiyo ilikwenda kumtembelea Mkuu wa Mkoa kabla ya kuanza ziara yake ya kikazi mkoani humo


Wednesday, August 29, 2018

KAMATI YA NISHATI NA MADINI YAKUTANA NA WATENDAJI WA WIZARA YA NISHATI

Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini, wakiwa 
katika kikao cha Kamati hiyo kilichofanyika katika Ofisi ya 
Bunge Jijini Dodoma. Kamati hiyo leo ilikutana na watendaji wa 
Wizara ya Niishati wakiongozwa na Naibu Waziri, Mhe. Subira Mgalu.

Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini, wakiwa 

katika kikao cha Kamati hiyo kilichofanyika katika Ofisi ya 

Bunge Jijini Dodoma. Kamati hiyo leo ilikutana na watendaji wa 

Wizara ya Niishati wakiongozwa na Naibu Waziri, Mhe. Subira Mgalu.

Naibu Waziri wa Wizara ya Nishati, Mhe. Subira Mgalu akiwa na 

watendaji wake katika Kikao cha Kamati ya Bunge ya Nishati 

kilichofanyika leo Jijini Dodoma. Kamati hiyo leo ilikuwa 

inapokea taarifa ya wizara hiyo kuhusu maendeleo nachangamoto 

za uendelezaji wa migodi ya makaa ya mawe nchini na taarifa 

kuhusu uwekezaji katika madini ya kimkakati.


KAMATI YA BAJETI YAKUTANA IKIONGOZWA NA MWENYEKITI WAKE MHE. GEORGE SIMBACHAWENE


Kamati ya Bunge ya Bajeti ikiongozwa na Mwenyekiti wakeMhe. 

George Simbachawene ikiwa katika kikao cha Kamati leo katika 

Ofisi za Bunge Jijini Dodoma.Kamati hiyo ilikuwa ikipitia na 

kuchambua Muswada wa Sheria ya Ubia baina ya Sekta yaUmma 

na Sekta Binafsi wa mwaka 2018 

Mwenyekiti wa Kamati ya Bajeti , Mhe. Goerge Simbachawene 

akiongoza Kikao cha Kamati hiyo kilichokutana leo  katika Ofisi 

za Bunge Jijini Dodoma., pembeni ni Makamu Mwenyekiti wa 

Kamati hiyo, Mhe. Mashimba Ndaki . Kamati hiyo ilikuwa 

ikipitia na kuchambua Muswada wa Sheria ya Ubia baina yaSekta 

ya Umma na Sekta Binafsi wa mwaka 2018 

Mwenyekiti wa Kamati ya Bajeti , Mhe. Goerge Simbachawene 

akisisitiza jambo katika Kikao cha Kamati hiyo kilichokutana leo  

katika Ofisi za Bunge Jijini Dodoma., pembeni ni Makamu 

Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhe. Mashimba Ndaki . Kamati 

hiyo ilikuwa ikipitia na kuchambua Muswada wa Sheria ya Ubia 

baina ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi wa mwaka 2018 

Kamati ya Bunge ya Bajeti ikiongozwa na Mwenyekiti wakeMhe. 
George Simbachawene ikiwa katika kikao cha Kamati leo katika 

Ofisi za Bunge Jijini Dodoma.Kamati hiyo ilikuwa ikipitia na 

kuchambua Muswada wa Sheria ya Ubia baina ya Sekta ya 

Umma na Sekta Binafsi wa mwaka 2018 

KAMATI YA SHERIA NDOGO YAKUTANA NA WAZIRI WA ARDHI

Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Sheria Ndogo wakimsikiliza Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mheshimiwa William Lukuvi alipokuwa akitoa majibu ya hoja za Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Sheria Ndogo katika kikao cha Kamati hiyo kilichofanyika leo Jijini Dodoma.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mheshimiwa William Lukuvi akiiongoza Wizara yake kutoa majibu ya hoja za Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Sheria Ndogo katika kikao cha Kamati hiyo kilichofanyika leo Jijini Dodoma.