WELCOME TO TANZANIA NATIONAL ASSEMBLY OFFICIAL BLOG: CONTACT US: P.O.BOX 941 DODOMA, TANZANIA, WEBSITE: parliament.go.tz , FIND US ON FACEBOOK >>> www.facebook.com/bungetz1, FOLLOW US ON TWITTER >>> @bunge_tz.>>>KARIBUNI

Thursday, March 31, 2016

KAMATI YA MALIASILI YATEMBELEA HIFADHI YA SAADANI PAMOJA NA KUKUTANA NA TANAPAMwenyekiti wa Kamati ya Ardhi, Maliasili na Utalii Mhe Atashasta Nditiye akizungumza na Menejimenti ya TANAPA wakati kamati hiyo iliopotembelea Hifadhi ya Saadani. Kulia kwake ni Naibu Waziri wa Utalii na Maliasili Mhandisi Ramo Makani.


Mkurugenzi wa Masoko na Utalii wa TANAPA Bw. Ibrahim Musa akitoa ufafanuzi wa masuala mbalimbali wakati akizungumza na Wajumbe wa Kamati ya Ardhi, Maliasili na Utalii. Kamati hiyo ilikutana na TANAPA katika Hifadhi ya Saadani.Naibu Waziri wa Utalii na Maliasili Mhandisi Ramo Makani akifafanua jambo kwa Wajumbe wa Kamati ya Ardhi, Maliasili na Utalii. Kamati hiyo ilikutana na TANAPA katika Hifadhi ya Saadani.


Mkuu wa Hifadhi ya Saadani Bw. Hassan Nguluma akiwaonesha Wajumbe wa Kamati ya Maliasili, Utalii na Ardhi ramani ya Hifadhi hiyo wakati kamati hiyo ilipoitembelea Hifadhi ya Saadani pamoja na kukutana na Menejimenti ya TANAPA. Wengine katika picha ni Naibu Waziri wa Utalii na Maliasili Mhandisi Ramo Makani (mweye miwani) na Kulia kwake ni Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe Atashasta Nditiye.

Wednesday, March 30, 2016

SPIKA JOB NDUGAI AKUTANA NA CHAMA CHA MABENKI TANZANIA (TBA)


Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Job Ndugai akiongea na viongozi wa Chama cha Mabenki Tanzania (TBA) wakati walipomtembelea ofisini kwake 30 Machi, 2016 jijini Dar es Salaam.


Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson akiongea na viongozi wa Chama cha Mabenki Tanzania (TBA) wakati walipomtembelea Spika ofisini kwake 30 Machi, 2016 jijini Dar es Salaam.


Mmoja wa Viongozi wa Chama cha Mabenki (TBA) Bwana Neech Msuya (kushoto) akifafanua jambo mbele ya Spika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Job Ndugai (hayupo pichani) wakati walipomtembelea ofisini kwake 30 Machi, 2016 jijini Dar es Salaam.


Mmoja wa wajumbe wa Chama cha Mabenki (TBA) Bwana Shani Kinswaga (kushoto) akifafanua jambo mbele ya Spika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Job Ndugai (hayupo pichani) wakati walipomtembelea ofisini kwake 30 Machi, 2016 jijini Dar es Salaam.
(Picha zote na Benedict Liwenga)