WELCOME TO TANZANIA NATIONAL ASSEMBLY OFFICIAL BLOG: CONTACT US: P.O.BOX 941 DODOMA, TANZANIA, WEBSITE: parliament.go.tz , FIND US ON FACEBOOK >>> www.facebook.com/bungetz1, FOLLOW US ON TWITTER >>> @bunge_tz.>>>KARIBUNI

Saturday, November 18, 2023

KATIBU NENELWA AHAIRISHA KIKAO CHA BARAZA LA WAFANYAKAZI OFISI YA BUNGE, TUGHE TAIFA YAMPONGEZA SPIKA DKT. TULIA KWA USHINDI WA URAIS WA IPU
















Katibu wa Bunge ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi ofisi ya Bunge, Ndg. Nenelwa Mwihambi, ndc amehairisha kikao cha Baraza la Wafanyakazi ofisi ya Bunge baada ya kusoma na kuridhia maazimio yaliyofikiwa katika kikao hicho.

Kikao hicho kimehairishwa leo tarehe 18 Novemba, 2023 katika hoteli na kituo cha Mikutano cha APC kilichopo Mbweni Jijini Dar es Salaam.

Maazimio mbalimbali yalifikiwa katika kikao hicho ikiwemo kuendelea kusimamia utekelezaji wa Mpango kazi wa ofisi ili kuhakikisha malengo yaliyokusudiwa katika mwaka wa fedha 2023/2024 yanatimia na baada ya mpango wa maendeleo wa Taifa kupitishwa na Bunge idara na vitengo vianze mchakato wa kuweka vipaumbele katika kutenga Bajeti hususan kwa miradi ya inayoendelea. Aidha, kwa miradi mipya maandiko ya miradi ikamilike na yapitishwe katika hatua zote muhimu za maamuzi kabla ya kutenga Bajeti.

Akizungumza wakati wa kikao hicho mwakilishi wa Katibu Mkuu wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali na Sekta ya Afya (TUGHE)Taifa ambaye ni Mjumbe wa Kamati kuu TUGHE Taifa, Ndg. Brendon Maro amempongeza Spika wa Bunge, Mhe. Dkt. Tulia Ackson kwa ushindi alioupata wa kuwa Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU).

“Ushindi wake umekuja kwa kuwa ana mtandao mmoja kutoka kwenye taasisi yake anayoifanyia kazi hasa watumishi wamesaidia sana”amesema Maro

Awali, akizungumza wakati akihairisha kikao hicho Katibu wa Bunge, Ndg. Nenelwa Mwihambi, ndc ameshukuru kwa salamu hizo zilizotolewa na TUGHE Taifa kwa Mhe. Spika na kuhaidi kumfikishia, Pia alihimiza watumishi wafanye kazi kwa bidii ili ilete tija kwa Bunge na Taifa.

Kikao hicho cha muda wa siku mbili kimeanza jana tarehe 17 Novemba, 2023 na kimehitimishwa leo tarehe 18 Novemba, 2023.

 

Friday, November 17, 2023

KATIBU NENELWA AONGOZA KIKAO CHA BARAZA LA WAFANYAKAZI WA OFISI YA BUNGE JIJINI DAR ES SALAAM


















Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi ofisi ya Bunge, Ndg. Nenelwa Mwihambi, ndc ameongoza kikao cha Baraza hilo kilichopokea taarifa ya utekelezaji wa Bajeti ya mfuko wa Bunge kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024 na taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya idara ya utawala na rasilimali watu kwa Mwezi Julai - Septemba 2023 kilichofanyika katika hoteli na Kituo cha Mikutano cha APC Jijini Dar es Salaam.


 

Thursday, November 9, 2023

KATIBU NENELWA AFANYA MAZUNGUMZO NA NAIBU KATIBU MKUU WA CHAMA CHA MABUNGE YA JUMUIYA YA MADOLA


Katibu wa Bunge, Ndg. Nenelwa Mwihambi, ndc akizungumza na Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Mabunge ya Jumuiya ya Madola, Ndg. Jarvis Matiya alipomtembelea leo tarehe 9 Novemba, 2023 ofisini kwake Bungeni Jijini Dodoma.

Katibu wa Bunge, Ndg. Nenelwa Mwihambi, ndc akizungumza na Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Mabunge ya Jumuiya ya Madola, Ndg. Jarvis Matiya (katikati) alipomtembelea leo tarehe 9 Novemba, 2023 ofisini kwake Bungeni Jijini Dodoma. Kushoto ni Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uhusiano wa Kimataifa ofisi ya Bunge, Ndg. Daniel Eliufoo.

Katibu wa Bunge, Ndg. Nenelwa Mwihambi, ndc akiwa katika picha ya pamoja na Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Mabunge ya Jumuiya ya Madola, Ndg. Jarvis Matiya alipomtembelea leo tarehe 9 Novemba, 2023 ofisini kwake Bungeni Jijini Dodoma.

Katibu wa Bunge, Ndg. Nenelwa Mwihambi, ndc akiwa katika picha ya pamoja na Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Mabunge ya Jumuiya ya Madola, Ndg. Jarvis Matiya alipomtembelea leo tarehe 9 Novemba, 2023 ofisini kwake Bungeni Jijini Dodoma. Kulia ni Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uhusiano wa Kimataifa ofisi ya Bunge, Ndg. Daniel Eliufoo.

 Katibu wa Bunge, Ndg. Nenelwa Mwihambi, ndc akiwa katika picha ya pamoja na Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Mabunge ya Jumuiya ya Madola, Ndg. Jarvis Matiya alipomtembelea leo tarehe 9 Novemba, 2023 ofisini kwake Bungeni Jijini Dodoma. Kulia ni Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uhusiano wa Kimataifa ofisi ya Bunge, Ndg. Daniel Eliufoo.

BUNGE LA 12, MKUTANO WA 13-KIKAO CHA 9

Tuesday, November 7, 2023

SPIKA DKT. TULIA AFANYA MAZUNGUMZO NA VIONGOZI WA BENKI YA NMB BUNGENI JIJINI DODOMA

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU), Mhe. Dkt. Tulia Ackson akizungumza na Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB, Ndg. Ruth Zaipuna alipomtembelea leo tarehe 7 Novemba, 2023 ofisini kwake Bungeni Jijini Dodoma.


Spika wa Bunge na Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani, Mhe. Dkt. Tulia Ackson akizungumza na Viongozi kutoka Benki ya NMB wakiongozwa na Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki hiyo, Ndg. Ruth Zaipuna walipomtembelea ofisini kwake Bungeni Jijini Dodoma.

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU), Mhe. Dkt. Tulia Ackson akipokea zawadi kutoka kwa Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB, Ndg. Ruth Zaipuna alipomtembelea leo tarehe 7 Novemba, 2023 ofisini kwake Bungeni Jijini Dodoma.

Zawadi hiyo ni ya kumpongeza Mhe. Spika kwa kuchaguliwa kwake kuwa Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU).

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU), Mhe. Dkt. Tulia Ackson akiwa katika picha ya pamoja na Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB, Ndg. Ruth Zaipuna alipomtembelea leo tarehe 7 Novemba, 2023 ofisini kwake Bungeni Jijini Dodoma.


Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU), Mhe. Dkt. Tulia Ackson akiagana na Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB, Ndg. Ruth Zaipuna mara baada ya mazungumzo yaliyofanyika leo tarehe 7 Novemba, 2023 ofisini kwake Bungeni Jijini Dodoma.


Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani, Mhe. Dkt. Tulia Ackson akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi kutoka Benki ya NMB wakiongozwa na Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki hiyo, Ndg. Ruth Zaipuna (kulia kwake) walipomtembelea leo tarehe 7 Novemba, 2023 ofisini kwake Bungeni Jijini Dodoma.


 

BUNGE LA 12, MKUTANO WA KUMI NA TATU-KIKAO CHA SABA