WELCOME TO TANZANIA NATIONAL ASSEMBLY OFFICIAL BLOG: CONTACT US: P.O.BOX 941 DODOMA, TANZANIA, WEBSITE: parliament.go.tz , FIND US ON FACEBOOK >>> www.facebook.com/bungetz1, FOLLOW US ON TWITTER >>> @bunge_tz.>>>KARIBUNI

Wednesday, April 28, 2021

PICHA: SPIKA NDUGAI APOKEA HATI YA JENGO LA BUNGE JIJINI DODOMA

Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (kushoto) akipokea hati ya jengo la Bunge kutoka kwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. William Lukuvi ofisini kwake Bungeni Jijini Dodoma. Katikati ni Katibu wa Bunge, Ndg. Stephen Kagaigai, Pia Spika Ndugai alitoa wito kwa taasisi zote za kiserikali, Wizara na Mashirika kuhakikisha kwamba maeneo yao yote yamepimwa na yana hati 

 

Friday, April 23, 2021

SPIKA NDUGAI ALIPOKUTANA NA KUZUNGUMZA NA BALOZI WA UINGEREZA NA UFARANSA KWA NYAKATI TOFAUTI OFISINI KWAKE JIJINI DODOMA







Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai akizungumza na Balozi wa Uingereza nchini Tanzania, Mhe. David Concar alipomtembelea leo ofisini kwake Bungeni Jijini Dodoma.

Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai katika picha ya  na Balozi wa Uingereza nchini Tanzania, Mhe. David Concar mara baada ya kuzungumza naye ofisini kwake Bungeni Jijini Dodoma.
Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai akisalimiana na Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania, Mhe. Frederic Clavier alipomtembelea  ofisini kwake Bungeni Jijini Dodoma.

Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai akizungumza na Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania, Mhe. Frederic Clavier  ofisini kwake Bungeni Jijini Dodoma.

 

Thursday, April 22, 2021

PICHA: RAIS SAMIA SULUHU HASSAN ALIHUTUBIA TAIFA KUPITIA BUNGE LA 12 BUNGENI JIJINI DODOMA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akilihutubia Taifa kupitia Bunge la 12 Jijini Dodoma. 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akilihutubia Taifa kupitia Bunge la 12 Jijini Dodoma.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akitoka katika ukumbi wa Bunge mara baada ya kulihutubuia Taifa kupitia Bunge la 12 Jijini Dodoma. Mbele ya Mhe. Rais ni Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan (katikati) katika  picha ya pamoja na Rais wa Awamu ya Pili, Mhe. Ali Hassan Mwinyi (kushoto) na Rais wa awamu ya Nne, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete nje ya Ukumbi wa Bunge mara baada ya kulihutubuia Taifa kupitia Bunge la 12 Jijini Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (kushoto) na Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Mhe. Zubeir Ali Maulid nje ya  ukumbi wa Bunge mara baada ya kulihutubuia Taifa kupitia Bunge la 12 Jijini Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan katika picha ya pamoja na kuanzia kushoto Jaji Mkuu wa Tanzania, Prof. Ibrahim Juma, Spika wa Bunge la Tanzania, Mhe. Job Ndugai, SSpika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Mhe. Zubeir Ali Maulid na Jaji Mkuu wa Zanzibar,  Omar Othman Makungu nje ya ukumbi wa Bunge mara baada ya kulihutubuia Taifa kupitia Bunge la 12 Jijini Dodoma.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan (katikati) katika  picha ya pamoja na Naibu Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson nje ya Ukumbi wa Bunge mara baada ya kulihutubuia Taifa kupitia Bunge la 12 Jijini Dodoma.