WELCOME TO TANZANIA NATIONAL ASSEMBLY OFFICIAL BLOG: CONTACT US: P.O.BOX 941 DODOMA, TANZANIA, WEBSITE: parliament.go.tz , FIND US ON FACEBOOK >>> www.facebook.com/bungetz1, FOLLOW US ON TWITTER >>> @bunge_tz.>>>KARIBUNI

Saturday, August 31, 2019

SPIKA AONGOZA KIKAO CHA BODI YA UWEKEZAJI YA CPA KANDA YA AFRIKA

Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (katikati) akiongoza kikao cha Bodi ya Uwekezaji ya Chama cha Mabunge ya Nchi za Jumuiya ya Madola (CPA), Kanda ya Afrika kilichofanyika katika Hotel ya Manidat AL Bahr Business and Spa Hotel. Kushoto ni Mhe. Elijah Okupa Mhasibu Msaidizi na Katibu wa CPA Kanda ya ya Afrika, Ndugu Stephen Kagaigai.


Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (wa kwanza kushoto) akiongoza kikao cha Bodi ya Uwekezaji ya Chama cha Mabunge ya Nchi za Jumuiya ya Madola (CPA), Kanda ya Afrika kilichofanyika katika Hotel ya Manidat AL Bahr Business and Spa Hotel. Katikati ni Katibu wa CPA Kanda ya Afrika, Ndugu Stephen Kagaigai na Ndugu Said Yakubu Katibu Msaidizi wa CPA Afrika
Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (katikati) akiongoza kikao cha Bodi ya Uwekezaji ya Chama cha Mabunge ya Nchi za Jumuiya ya Madola (CPA), Kanda ya Afrika kilichofanyika katika Hotel ya Manidat AL Bahr Business and Spa Hotel.

NAIBU SPIKA DKT. TULIA ACKSON AKUTANA NA NAIBU SPIKA WA BUNGE LA JAMHURI YA AFRIKA YA KUSINI

Naibu Spika, Mhe. Dkt. Tulia Ackson akimkaribisha Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Afrika ya Kusini, Mhe. Lechesa Tsenoli wakati walipokutana katika Hoteli ya Madinat Al Bahr Business and Spa. Viongozi hao wapo visiwani Zanzibar kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa 50 wa Mabunge ya Nchi za Jumuiya ya Madola (CPA), Kanda ya Afrika.

Naibu Spika,Mhe.  Dkt. Tulia Ackson akizungumza na Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Afrika ya Kusini, Mhe. Lechesa Tsenoli katika Hoteli ya Madinat Al Bahr Business and Spa. Viongozi hao wapo visiwani Zanzibar kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa 50 wa Mabunge ya Nchi za Jumuiya ya Madola (CPA), Kanda ya Afrika.
 Naibu Spika, Mhe. Dkt. Tulia Ackson akiwa pamoja na Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Afrika ya Kusini, Mhe. Lechesa Tsenoli wakifurahia dafu wakati walipotembelea shamba la viungo (Spice farm)  visiwani Zanzibar. Viongozi hao wapo visiwani humo kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa 50 wa Mabunge ya Nchi za Jumuiya ya Madola (CPA), Kanda ya Afrika.

 Naibu Spika, Mhe. Dkt. Tulia Ackson akipewa zawadi ya bangili wakati yeye na Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Afrika ya Kusini, Mhe. Lechesa Tsenoli walipotembelea shamba la viungo (Spice farm)  visiwani Zanzibar. Viongozi hao wapo visiwani humo kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa 50 wa Mabunge ya Nchi za Jumuiya ya Madola (CPA), Kanda ya Afrika.
Naibu Spika,Mhe.  Dkt. Tulia Ackson pamoja na Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Afrika ya Kusini, Mhe. Lechesa Tsenoli wakitazama viungo mbalimbali wakati walipotembelea shamba la viungo (Spice farm)  visiwani Zanzibar. Viongozi hao wapo visiwani humo kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa 50 wa Mabunge ya Nchi za Jumuiya ya Madola (CPA), Kanda ya Afrika.

Friday, August 30, 2019

SPIKA WA BUNGE, MHE.JOB NDUGAI AWASILI ZANZIBAR

Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai amewasili Uwanja wa Ndege wa Zanzibar kwa ajili ya kuhudhuria Mkutano wa 50 wa Mabunge ya Nchi za Jumuiya ya Madola (CPA), Kanda ya Afrika, katikati ni Mwenyekiti wa CPA Tawi la Zanzibar, Mhe. Simai Mohammed Said na Katibu wa CPA Kanda ya Afrika, Ndugu Stephen Kagaigai. Mkutano huo utaanza Agosti 30 hadi Septemba 5, 2019 katika Hoteli ya Madinat Al Bahr Business and Spa.

Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai amewasili Uwanja wa Ndege wa Zanzibar kwa ajili ya kuhudhuria Mkutano wa 50 wa Mabunge ya Nchi za Jumuiya ya Madola (CPA), Kanda ya Afrika, katikati ni Mwenyekiti wa CPA Tawi la Zanzibar, Mhe. Simai Mohammed Said na Katibu wa CPA Kanda ya Afrika, Ndugu Stephen Kagaigai. Mkutano huo utaanza Agosti 30 hadi Septemba 5, 2019 katika Hoteli ya Madinat Al Bahr Business and Spa.

Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai amewasili Uwanja wa Ndege wa Zanzibar kwa ajili ya kuhudhuria Mkutano wa 50 wa Mabunge ya Nchi za Jumuiya ya Madola (CPA), Kanda ya Afrika, katikati ni Mwenyekiti wa CPA Tawi la Zanzibar, Mhe. Simai Mohammed Said na Katibu wa CPA Kanda ya Afrika, Ndugu Stephen Kagaigai. Mkutano huo utaanza Agosti 30 hadi Septemba 5, 2019 katika Hoteli ya Madinat Al Bahr Business and Spa.

SPIKA WA BUNGE LA LESOTHO AWASILI ZANZIBAR KUHUDHURIA MKUTANO WA CPA

Spika wa Bunge la Lesotho, Mhe. Sephiri Enoch Motanyane akiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Zanzibar na kupokelewa na Maafisa Itifaki wa Bunge la Tanzania kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa 50 wa Mabunge ya Nchi za Jumuiya ya Madola (CPA), Kanda ya Afrika utakaofanyika tarehe 30 Agosti hadi tarehe 5 Septemba mwaka huu katika Hoteli ya Madinat Al Bahr Business and Spa 

Spika wa Bunge la Lesotho, Mhe. Sephiri Enoch Motanyane akiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Zanzibar.
Spika wa Bunge la Lesotho, Mhe. Sephiri Enoch Motanyane akiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Zanzibar Chumba cha mapumziko na wenyeji wake.

Thursday, August 29, 2019

SPIKA WA BARAZA LA WAWAKILISHI AKAGUA MAANDALIZI YA MKUTANO WA CPASpika wa Bunge la Baraza la Wawakilishi Mheshimiwa Zubeir Ali Maulid amewataka Wazanzibari na Watanzania kwa ujumla kutumia fursa waliyoipata ya kuwa wenyeji wa  Mkutano wa 50 wa Mabunge ya Jumuiya ya Madola (CPA), Kanda ya Afrika kujitangaza kibiashara na kitalii.

Mheshimiwa Maulid ametoa rai hiyo leo Kisiwani Zanzibar wakati akikagua maandalizi ya Mkutano huo unaotarajiwa kufanyika kuanzia tarehe 30 Agosti hadi septemba 5 mwaka huu katika Hoteli ya Madinat Al Bahr Business & Spa.

Alisema mkutano huo kufanyika Zanzibar utafungua fursa katika sekta za biashara ikiwemo utalii na kuwataka Watanzania kuonyesha ukarimu kwa wageni hao.

“Tuonyeshe ukarimu wakati kupokea wageni hawa, tuitendee haki nchi yetu, tukikaa nao vizuri wageni wetu itatosha kwa sisi kujitangaza, tutumie fursa hii kwa kadri tutakavyoona inaweza kuisaidia nchi” alisema.

Alisema mkutano huo ni wa kihistoria kwa kuwa unaweza kuvunja rekodi ya mahudhurio ya wajumbe zaidi ya 400 kutoka nchi 18 wanachama ambao unajumuisha maspika, manaibu spika na wabunge.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa CPA, Tawi la Zanzibar, Mheshimiwa Simai Mohammed Said alisema mkutano huo mbali na kutoa fursa za kiuchumi lakini pia utawezesha wajumbe kubadilishana uzoefu wa jinsi ya kutekeleza majukumu yao ikiwemo kuisimamia Serikali katika mambo yanayogusa wananchi.

Awali akizungumzia maandalizi ya awali, Katibu Msaidizi wa CPA, Kanda ya Afrika, Said Yakubu alisema Nchi zote 18 wanachama zimethibitisha ushiriki na kwamba maspika 23 kutoka mabunge makubwa na madogo watahudhuria.

Alisema nchi wanachama wa CPA, Kanda ya Afrika ni Botswana, Cameroon, Eswatini, Ghana, Kenya, Lesotho, Malawi, Mauritius, Msumbiji, Namibia, Nigeria, Rwanda, Seychelles, Siera – Leone, Afrika ya Kusini, Tanzania, Uganda na Zambia.SPIKA WA BUNGE MHESHIMIWA JOB NDUGAI AKARIBISHA USHIRIKIANO NA NCHI YA IRELAND

Spika wa Bunge Mheshimiwa, Job Ndugai ameishukuru Serikali ya Ireland kwa kuendelea kuimarisha ushirikiano na Tanzania katika sekta ya sheria na haki za binadamu.
Mheshimiwa Spika ametoa shukrani hizo leo ofisini kwake Bungeni JIjini Dodoma wakati alipokutana na Ujumbe wa Wanasheria wa haki za binadamu kutoka Ubalozi wa Ireland wakiongozwa na Naibu Balozi wa Ireland hapa nchini Mheshimiwa Bronagh Carr.
Alisema Tanzania itaendelea kudumisha ushirikiano huo na Serikali ya Ireland katika masuala hayo ya sheria pamoja na kudumisha haki za binadamu.
Aidha, alisema upo umuhimu ujumbe huo, ukakutana na Umoja wa Wabunge Wanawake nchini (TWPG) ili kujadili changamoto za kijinsia zilizopo katika maeneo yao na kuzitafutia ufumbuzi kwa kuwa Ireland imepiga hatua kubwa kwenye masuala ya usawa wa kijinsia.
aliwataka pia wakutane na  Kamati ya kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii ambapo miswada yote inayoathiri huduma za jamii ikiwemo masuala ya elimu na jinsia hujadiliwa kwenye kamati hiyo kabla ya kuingia Bungeni.
“Katika suala la usawa kwa jinsia Bunge letu limepiga hatua kubwa ambapo Wabunge wa Viti Maalum Wanawake ni asilimia 30 ya Wabunge wote 393 pia wapo Wabunge wa majimbo ambao ni Wanawake hivyo kuongeza nafasi ya uwakilishi wa jinsi hiyo Bungeni” alisema Mheshimwa Spika.
kwa upande wake Kaimu Balozi wa Ireland, Mheshimiwa Bronagh Carr alimshukuru Mheshimiwa Spika kwa kukubali kukutana nae pamoja na Kamati za Bunge.
Alisema ushirikiano kati ya Tanzania na Ireland umekuwepo kwa kipindi cha miaka 40 na unazidi kuimarika siku hadi siku.
Ujumbe huo umelenga kukutana na wadau mbalimbali wa masuala ya kisheria  ikiwemo Wabunge, Mwendesha mashitaka mkuu wa Serikali pamoja na Jeshi la polisi nchini ili kuimarisha ushirikiano katika masuala ya sheria na jinsia.
Spika wa Bunge Mheshimiwa Job Ndugai akisalimiana na Naibu Balozi wa Ireland hapa nchini walipokutana na kufanya mazungumzo Ofisini kwake Bungeni Jijini Dodoma hii leo. 
Spika wa Bunge Mheshimiwa Job Ndugai akifafanua jambo alipokutana na Ujumbe wa Wanasheria kutoka ubalozi wa Ireland nchini Ofisini kwake Bungeni Jijini Dodoma hii leo.
Spika wa Bunge Mheshimiwa Job Ndugai akiwa katika picha ya pamoja na ujumbe wa Wanasheria kutoka ubalozi wa Ireland nchini waliomtembelea Ofisini kwake Bungeni Jijini Dodoma hii leo.


Friday, August 23, 2019

KATIBU WA BUNGE ATEMBELEWA NA JAJI MFAWIDHI WA MAHAKAMA KUU KANDA YA DODOMAKatibu wa Bunge, Ndugu Stephen Kagaigai akizungumza na Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Dodoma, Mhe. Lameck Mlacha wakati Jaji huyo alipomtembelea Ofisini kwake Bungeni Jjijini  Dodoma.


Katibu wa Bunge, Ndugu Stephen Kagaigai akiwa katika picha ya pamoja na Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Dodoma, Mhe. Lameck Mlacha wakati Jaji huyo alipomtembelea Ofisini kwake Bungeni Jijini Dodoma.
Katibu wa Bunge, Ndugu Stephen Kagaigai akiagana na Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Dodoma, Mhe. Lameck Mlacha mara baada ya Jaji huyo kumtembelea Ofisini kwake Bungeni Jijini Dodoma.

Tuesday, August 20, 2019

WAJUMBE WA KAMATI YA BAJETI WAKIWA KATIKA KIKAO

Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Bajeti wakiwa katika kikao cha Kamati hiyo kilichofanyika katika Ofisi za Bunge Jijini Dodoma

Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Bajeti wakiwa katika kikao cha Kamati hiyo kilichofanyika katika Ofisi za Bunge Jijini Dodoma


Afisa Bajeti kutoka Ofisi ya Bunge, Maombi Kakozi akifafanua jambo  kwa Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Bajeti katika kikao cha Kamati hiyo kilichofanyika katika Ofisi za Bunge Jijini Dodoma

WAJUMBE WA KAMATI YA NISHATI WAPOKEA TAARIFA YA MAENDELEO YA UTEKELEZAJI MIRADI YA REA

Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Nishati, Mhe. Dunstun Kitandula akifuatilia jambo katika kikao cha Kamati hiyo kilichofanyika katika Ofisi za Bunge Jijini Dodoma, pembeni yake ni Katibu wa Kamati hiyo, Felister Mgonja.


Waziri wa Nishati, Mhe. Medard Kalemani akizungumza katika kikao cha Kamati ya Bunge ya Nishati ambapo Wizara yake iliwasilisha Taarifa ya Maendeleo na Utekelezaji wa Miradi ya REA, kikao hicho kilifanyika katika Ofisi za Bunge Jijini Dodoma, pembeni yake ni Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Subira Mgalu.

Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Nishati wakiwa katika kikao cha Kamati hiyo ambapo walipokea Taarifa ya Maendeleo na Utekelezaji wa Miradi ya REA kutoka Wizara ya Nishati, kikao hicho kilifanyika katika Ofisi za Bunge Jijini Dodoma.

KAMATI YA UTAWALA NA SERIKALI ZA MITAA YAJADILI MUSWADA WA SHERIA YA SERIKALI MTANDAO WA MWAKA 2019Mshauri wa Masuala ya Sheria wa Bunge Ndg. Mosi Lukuvi

 akitoa maelezo ya uchambuzi wa Muswada wa Sheria ya Serikali 

Mtandao 2019  (The e-Gvernment Act 2019),kwa Kamati ya 

Utawala na Serikali za Mitaa,Jijini Dodoma. Kulia ni Makamu 

Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mheshimiwa Mwanne Nchemba na 

katikati ni Katibu wa Kamati hiyo Ndg. Chacha Nyakega. 

Mshauri wa Masuala ya Sheria wa Bunge Ndg. Mosi Lukuvi

 akitoa maelezo ya uchambuzi wa Muswada wa Sheria ya Serikali 

Mtandao 2019  (The e-Gvernment Act 2019),kwa Kamati ya 

Utawala na Serikali za Mitaa,Jijini Dodoma. Kulia ni Makamu 

Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mheshimiwa Mwanne Nchemba na 

katikati ni Katibu wa Kamati hiyo Ndg. Chacha Nyakega. 

Wajumbe wa Kamati ya Utawala na Serikali za Mitaa wakisikiliza

 maelezo ya uchambuzi wa Muswada wa Sheria ya Serikali 

Mtandao 2019  (The e-Gvernment Act 2019)kutoka kwa Mshauri 

wa Masuala ya Sheria wa Bunge Ndg. Mosi Lukuvi.


Friday, August 16, 2019

KAMATI YA PAC YAPEWA MAFUNZO NA OFISI YA MSAJILI WA HAZINA

Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali PAC wakifuatilia jambo kwa karibu kwenye Semina kuhusu Changamoto za usimamizi wa matumizi ya Mashirika ya Umma nchini iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Msekwa Bungeni Jijini Dodoma hii leo. 
Mkurugenzi wa Uwekezaji kutoka Ofisi ya Msajili wa Hazina Ndg. Lightness Mauki akifafanua jambo alipokuwa akitoa Mada kuhusu Changamoto za usimamizi wa Matumizi ya Mashirika ya Umma nchini kwa wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali PAC iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Msekwa Bungeni Jijini Dodoma hii leo. 


Thursday, August 15, 2019

BARAZA LA WAFANYAKAZI WA OFISI YA BUNGE LANDELEA NA KIKAO

Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi la Ofisi ya Bunge, Ndugu Stephen Kagaigai akizungumza katika kikao kilichofanyika katika Ofisi  Ndogo za Bunge, Tunguu Zanzibar, pamoja naye ni Katibu wa Baraza Ndugu Frank Mbilinyi.

Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi la Ofisi ya Bunge, Ndugu Stephen Kagaigai akizungumza katika kikao kilichofanyika katika Ofisi  Ndogo za Bunge, Tunguu Zanzibar, pamoja naye ni Katibu wa Baraza Ndugu Frank Mbilinyi.
Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi wa Afya na Serikali Kuu (TUGHE), Tawi la Bunge, Ndugu Chacha Nyakega akitoa nasaha za chama hicho katika kikao cha Baraza la Wafanyakazi wa Ofisi ya Bunge lililofanyika katika Ofisi ndogo za Bunge, Tunguu Zanzibar.

Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi wa Afya na Serikali Kuu (TUGHE), Tawi la Bunge, Ndugu Chacha Nyakega akitoa nasaha za chama hicho katika kikao cha Baraza la Wafanyakazi wa Ofisi ya Bunge lililofanyika katika Ofisi ndogo za Bunge, Tunguu Zanzibar.
Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi la Ofisi ya Bunge wakifuatilia mada kuhusu Umuhimu wa Kuzingatia Maadili katika Utumishi wa Umma katika shughuli za Bunge kilichofanyika Ofisi Ndogo za Bunge, Tunguu Zanzibar

Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi la Ofisi ya Bunge wakifuatilia mada kuhusu Umuhimu wa Kuzingatia Maadili katika Utumishi wa Umma katika shughuli za Bunge kilichofanyika Ofisi Ndogo za Bunge, Tunguu ZanzibarWednesday, August 14, 2019

SPIKA WA BUNGE AWATAKA WAFANYAKAZI WA OFISI YA BUNGE KUFANYA KAZI KWA BIDII
Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai amewataka watumishi wa Bunge kuacha kufanya kazi kwa mazoea badala yake wafanye kazi kwa bidii.

Mhe. Spika alitoa rai hiyo kupitia hotuba yake iliyosomwa kwa niaba yake na Naibu Spika, Mhe. Dkt. Tulia Ackson alipokuwa anazindua Baraza la Wafanyazi la Ofisi ya Bunge lililofanyika  katika Ofisi Ndogo za Bunge Tunguu Zanzibar.

Alisema kunahitajika mabadiliko katika utekelekezaji wa majukumu ya kila siku kwa watumishi katika kuchapa kazi ili kuleta utendaji kazi wenye tija na ufanisi.

Aidha, aliwataka wajumbe kupitia mada zitakazowasilishwa katika Mkutano huo wa Baraza kukumbuka wajibu wao katika kutelekeza majukumu waliyopewa kulingana na taaluma husika na hatimaye kufanikisha utekelezaji bora wa majukumu na madaraka ya Bunge Kikatiba.

Vilevile, alimpongeza Katibu wa Bunge, Ndugu Stephen Kagaigai kwa kufanikisha utatuzi wa changamoto ya muda mrefu ya muundo wa Ofisi ya Bunge ambayo hatimaye ufumbuzi umewezesha kuundwa kwa Baraza la Wafanyakazi.

“Naomba nitumie fursa hii kuwapongeza watumishi wote mlioteuliwa na Tume ya Utumishi wa Bunge kushika nyadhifa mbalimbali za uongozi na ni matumini yangu kwamba mtatumia uwezo na karama mlizojaaliwa na Mwenyezi Mungu katika kutekeleza majukumu yenu kwa ufanisi hivyo kuliwezesha Bunge kufikia malengo yake,” alisema.

Aliwapongeza pia Wajumbe na Wawakilishi wa Idara na Vitengo kwa kuchaguliwa kushika nafasi hizo na kuwataka kutumia nafasi zao ili kuwa kiungo kati ya Wafanyakazi wa kada, ngazi zote, Menejimenti na Tume ya Utumishi wa Bunge.

Uzinduzi wa Baraza la Wafanyakazi ulihudhuriwa na Katibu Mkuu Taifa wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali Kuu na Afya, TUGHE Ndugu Hery Nkunda na Katibu wa TUGHE Mkoa wa Dodoma Ndugu John Mchenya ambao walinasihi Baraza kudumisha ushirikiano na kuongeza ufanisi katika ujenzi wa nchi.

Awali akizungumza katika mkutano huo, Katibu wa Bunge Ndugu Stephen Kagaigai alisema Ofisi ya Bunge imeunda Baraza la Wafanyakazi baada kutokuwepo ya Baraza hilo katika kipindi kirefu kutokana na changamoto zilizokuwepo za kimuundo za Ofisi ya Bunge.

Alisema, lengo la Baraza lililopo kisheria ni kuboresha utendaji kazi  wa taasisi kwa kufanya kazi kwa ushirikiano na bila ya ugomvi  wala mifarakano.

Kabla ya uzinduzi wa Baraza la Wafanyakazi, wajumbe walimchagua Ndugu Frank Mbilinyi kuwa katibu wa Baraza na Ndugu Felister  Njovu kuwa Katibu Msaidizi.NAIBU SPIKA AZINDUA BARAZA LA WAFANYAKAZI OFISI YA BUNGE

Katibu wa Bunge, Ndugu Stephen Kagaigai (katikati) akiimba wimbo wa mshikamano wa Wafanyakazi kabla ya kuanza kwa Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi la  Ofisi ya Bunge uliofanyika katika Ofisi Ndogo za Bunge, Tunguu Zanzibar pamoja na Ndugu Chacha Nyakega Mwenyekiti wa  TUGHE Tawi la Ofisi ya Bunge na Ndugu Triphonia Mng’ong’o Kaimu Mkurugenzi  wa Idara ya  Utawala na  Rasilimaliwatu.

Naibu Spika wa Bunge la Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson akifungua Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi la  Ofisi ya Bunge uliofanyika katika Ofisi Ndogo za Bunge, Tunguu Zanzibar

Naibu Spika wa Bunge la Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson akifungua Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi la  Ofisi ya Bunge uliofanyika katika Ofisi Ndogo za Bunge, Tunguu Zanzibar

Naibu Spika wa Bunge la Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson akimkabidhi Katibu wa Bunge, Ndugu Stephen Kagaigai Mkataba kwa ajili ya kuunda Baraza la Wafanyakazi la Ofisi ya Bunge mara baada ya kuzindua Baraza hilo. Uzinduzi huo umefanyika katika Ofisi Ndogo za Bunge, Tunguu Zanzibar


Naibu Spika wa Bunge la Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson akimkabidhi Katibu Mkuu wa TUGHE Taifa, Ndugu Hery Nkunda Mkataba kwa ajili ya kuunda Baraza la Wafanyakazi la Ofisi ya Bunge baada ya uzinduzi. Uzinduzi huo umefanyika katika Ofisi Ndogo za Bunge, Tunguu Zanzibar
Naibu Spika wa Bunge la Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson akimkabidhi Katibu Mkuu wa TUGHE Mkoa wa Dodoma , Ndugu John Mchenya  Mkataba kwa ajili ya kuunda Baraza la Wafanyakazi la Ofisi ya Bunge mara baada ya kuzindua Baraza hilo. Uzinduzi huo umefanyika katika Ofisi Ndogo za Bunge, Tunguu Zanzibar
 
Wajumbe wa Baraza wakiwa katika picha ya pamoja