WELCOME TO TANZANIA NATIONAL ASSEMBLY OFFICIAL BLOG: CONTACT US: P.O.BOX 941 DODOMA, TANZANIA, WEBSITE: parliament.go.tz , FIND US ON FACEBOOK >>> www.facebook.com/bungetz1, FOLLOW US ON TWITTER >>> @bunge_tz.>>>KARIBUNI

Friday, November 25, 2022

WACHEZAJI TIMU YA BUNGE SPORTS CLUB WASHIRIKI KATIKA UZINDUZI WA MICHEZO YA MABUNGE YA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI NCHINI SUDAN KUSINI
















Matukio katika picha yaliyojiri leo tarehe 25 Novemba, 2022 wakati wachezaji wa timu ya Bunge Sports Club wakishiriki katika uzinduzi wa Michezo ya Mabunge ya Jumuiya ya Afrika Mashariki katika Ukumbi wa Freedom Hall, Juba Nchini Sudan Kusini.

Kauli Mbiu ya Michezo hiyo ni Kupanua na Kuimarisha Muungano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa Kuongeza umoja wa Wananchi wake kupitia Michezo.


 

Wednesday, November 23, 2022

WACHEZAJI WA BUNGE SPORTS CLUB WAWASILI SUDAN KUSINI KUSHIRIKI MASHINDANO YA MICHEZO YA MABUNGE YA AFRIKA MASHARIKI

Naibu Spika wa Bunge, Mheshimiwa Mussa Azzan Zungu kwa niaba ya Spika wa Bunge akiwakabidhi bendera ya Bunge Wachezaji wa Bunge Sports Club wanaoelekea nchini Sudan Kusini kushiriki katika michezo ya 12 ya Mabunge ya Jumuiya ya Afrika Mashariki. Tukio la kuwaaga Wachezaji hao limefanyika katika Ofisi Ndogo za Bunge Jijini Dar es Salaam.

Naibu Spika wa Bunge, Mheshimiwa Mussa Azzan Zungu akizungumza wakati akiwaaga  kwa niaba ya Spika wa Bunge   Wachezaji wa Bunge Sports Club wanaoelekea nchini Sudan Kusini kushiriki katika michezo ya 12 ya Mabunge ya Jumuiya ya Afrika Mashariki. Tukio la kuwaaga Wachezaji hao limefanyika katika Ofisi Ndogo za Bunge Jijini Dar es Salaam.

Mwenyekiti wa Bunge Sports Club, Mheshimiwa Tarimba Abbas akizungungumza wakati wakuwaaga Wachezaji wa Bunge Sports Club wanaoelekea nchini Sudan Kusini kushiriki katika michezo ya 12 ya Mabunge ya Jumuiya ya Afrika Mashariki. Tukio la kuwaaga Wachezaji hao limefanyika katika Ofisi Ndogo za Bunge Jijini Dar es Salaam.   

Wachezaji wa Timu ya Bunge Sports Club wakiwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Juba nchini Sudan kwa ajili ya kushiriki katika michezo ya 12 ya Mabunge ya Jumuiya ya Afrika Mashariki
Wachezaji wa Timu ya Bunge Sports Club wakiwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Juba nchini Sudan kwa ajili ya kushiriki katika michezo ya 12 ya Mabunge ya Jumuiya ya Afrika Mashariki

 Wachezaji wa Timu ya Bunge Sports Club wakiwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Juba nchini Sudan kwa ajili ya kushiriki katika michezo ya 12 ya Mabunge ya Jumuiya ya Afrika Mashariki.

....................................................................................


Wachezaji wa Timu ya Bunge Sports Club wamewasili Jijini Juba nchini Sudan Kusini kwa ajili ya kushiriki katika mashidano ya michezo ya 12 ya Mabunge ya Jumuiya ya Afrika Mashariki inayotarajiwa kuanza tarehe 25 Novemba hadi 2 Disemba 2022.

Awali Naibu Spika wa Bunge, Mheshimiwa Mussa Azzan Zungu aliwakabidhi Wachezaji hao bendera ya Taifa na Bunge kwa niaba ya Spika wa Bunge. Tukio hilo lilifanyika katika Ofisi Ndogo za Bunge Jijini Dar es Salaam.

Aidha akizungumza na Wachezaji hao kabla ya kuwakabidhi bendera Naibu Spika aliwaasa kudumisha heshima ya taifa pamoja na nidhamu wakati wote wa mashidano.

"Nendeni mkadumishe heshima ya taifa letu na mkalitangaze, kama taifa tuna fursa mbalimbali zikiwemo za utalii," alisema Naibu Spika.

Pia Naibu Spika aliwaambia wachezaji hao kwamba wanatarajiwa kurudi na vikombe katika michezo mbalimbali ambayo watashiriki.


Thursday, November 10, 2022

SPIKA DKT. TULIA AFANYA MAZUNGUMZO NA MWAKILISHI WA HESHIMA WA TANZANIA NCHINI UTURUKI, AFUNGUA SEMINA YA TWPG JIJINI DODOMA.


Spika wa Bunge, Mhe. Dkt. Tulia Ackson akizungumza na Mwakilishi wa Heshima wa Tanzania nchini Uturuki, Mhe. Ziya Karahan (katikati) alipomtembelea leo tarehe 10 Novemba, 2022 ofisini kwake Bungeni Jijini Dodoma. Kushoto ni Dkt. Mbaraka Abdallah ameambatana na Mwakilishi huyo.



Spika wa Bunge, Mhe. Dkt. Tulia Ackson akiwa katika picha ya pamoja na Mwakilishi wa Heshima wa Tanzania nchini Uturuki, Mhe. Ziya Karahan alipomtembelea leo tarehe 10 Novemba, 2022 ofisini kwake Bungeni Jijini Dodoma.




Spika wa Bunge, Mhe. Dkt. Tulia Ackson akimpatia zawadi Mwakilishi wa Heshima wa Tanzania nchini Uturuki, Mhe. Ziya Karahan alipomtembelea leo tarehe 10 Novemba, 2022 ofisini kwake Bungeni Jijini Dodoma.




Spika wa Bunge, Mhe. Dkt. Tulia Ackson akifungua semina ya Umoja wa Wabunge Wanawake Tanzania (TWPG) iliyoendeshwa na Benki ya NBC kuhusu elimu za uchumi na Biashara, Usimamizi wa Fedha, Bima za Biashara na Maisha na Bima za hati Fungani iliyofanyika Four Points Hall Kisasa, Jijini Dodoma.




 Spika wa Bunge, Mhe. Dkt. Tulia Ackson akiwa katika picha ya pamoja na  Umoja wa Wabunge Wanawake Tanzania (TWPG) na Watendaji kutoka Benki ya NBC baada ya kufungua semina ya TWPG iliyoendeshwa na Benki hiyo kuhusu elimu za uchumi na Biashara, Usimamizi wa Fedha, Bima za Biashara na Maisha na Bima za hati Fungani iliyofanyika Four Points Hall Kisasa, Jijini Dodoma.

Thursday, November 3, 2022

SPIKA WA BUNGE LA TANZANIA AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA BALOZI WA MORROCO NCHINI TANZANIA

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt, Tulia Ackson (Mb) amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Ufalme wa Morocco nchini Tanzania Mhe. Zakaria El Gowmiri leo tarehe 03Novemba 2022 ofisini kwake Bungeni Jijini Dodoma

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt, Tulia Ackson (Mb) amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Ufalme wa Morocco nchini Tanzania Mhe. Zakaria El Gowmiri leo tarehe 03Novemba 2022 ofisini kwake Bungeni Jijini Dodoma


Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt, Tulia Ackson (Mb) amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Ufalme wa Morocco nchini Tanzania Mhe. Zakaria El Gowmiri leo tarehe 03Novemba 2022 ofisini kwake Bungeni Jijini Dodoma