WELCOME TO TANZANIA NATIONAL ASSEMBLY OFFICIAL BLOG: CONTACT US: P.O.BOX 941 DODOMA, TANZANIA, WEBSITE: parliament.go.tz , FIND US ON FACEBOOK >>> www.facebook.com/bungetz1, FOLLOW US ON TWITTER >>> @bunge_tz.>>>KARIBUNI

Thursday, March 31, 2022

WAJUMBE KAMATI YA KATIBA NA SHERIA WAPOKEA NA KUJADILI MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI YA WIZARA YA KATIBA NA SHERIA KWA MWAKA WA FEDHA 2022/2023

Wajumbe wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya katiba na Sheria wakiwa katika kikao cha kupokea na kujadili Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Katiba na Sheria kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023 leo Machi 31, 2022 katika Ukumbi wa Msekwa Bungeni Jijini Dodoma.

Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya Bunge ya katiba na Sheria, Mhe. Dkt. Joseph Mhagama akiongoza kikao cha kupokea na kujadili Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Katiba na Sheria kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023 leo Machi 31, 2022 katika Ukumbi wa Msekwa Bungeni Jijini Dodoma.


Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. George Simbachawene akijibu hoja Mbalimbali za Wajumbe wa kamati ya katiba na Sheria wakati wa kupokea na kujadili Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Katiba na Sheria kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023 leo Machi 31, 2022 katika Ukumbi wa Msekwa Bungeni Jijini Dodoma.


Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Mhe. Jaji. Dkt. Eliezer Feleshi akijibu hoja Mbalimbali za Wajumbe wa kamati ya katiba na Sheria wakati wa kupokea na kujadili Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Katiba na Sheria kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023 leo Machi 31, 2022 katika Ukumbi wa Msekwa Bungeni Jijini Dodoma. Kushoto kwake ni Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. George Simbachawene, Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria, Ndg. Mary Makondo na Naibu Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Geoffrey Pinda

SPIKA DKT. TULIA AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA BALOZI MABONERO JIJINI DODOMA

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson akizungumza na Balozi wa Uganda nchini Tanzania, Mhe. Richard Mabonero ofisini kwake Bungeni Jijini Dodoma.

Balozi huyo amemtembela Mhe. Spika kwa lengo la kumuaga baada ya kumaliza muda wake wa kufanya kazi hapa nchini.



Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson katika picha ya pamoja na Balozi wa Uganda nchini Tanzania, Mhe. Richard Mabonero ofisini kwake Bungeni Jijini Dodoma.

Balozi huyo amemtembela Mhe. Spika kwa lengo la kumuaga baada ya kumaliza muda wake wa kufanya kazi hapa nchini.

Wednesday, March 30, 2022

KAMATI YA PAC IMETEMBELEA BOHARI YA DAWA (MSD) NA KUKAGUA KIWANDA CHA KUTENGENEZA BARAKOA

 

Kaimu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), Mhandisi Isack Kamwelwe akizungumza katika kikao cha Kamati hiyo na watendaji wa Bohari ya Dawa (MSD) wakati Kamati hiyo ilipokagua kiwanda cha kutengeneza barakoa, kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Brig.Jen.Dkt. Gabriel Mhidize, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. Seif Shekhalage Na kulia ni Katibu wa Kamati Erick Maseke

 

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda cha Dawa cha Keko, Betia Kaema akiwaelezea wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) jinsi dawa zinavyotengenezwa wakati Kamati hiyo ilipotembelea Bohari ya Dawa (MSD) na kukagua kiwanda hicho na Kiwanda cha kutengeneza brake


Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda cha Dawa cha Keko, Betia Kaema akizungumza wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) kabla ya wajumbe hao hawajangia ndani  ya Kiwanda cha kutengeneza dawa cha Keko wakati Kamati hiyo ilipotembelea Bohari ya Dawa (MSD) na kukagua kiwanda hicho na Kiwanda cha kutengeneza barakoa 
Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Brig.Jen.Dkt. Gabriel Mhidize akizungumza wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) kabla ya wajumbe hao hawajangia ndani  ya Kiwanda cha kutengeneza dawa cha Keko wakati Kamati hiyo ilipotembelea MSD na kukagua kiwanda hicho na Kiwanda cha kutengeneza barakoa
Afisa Udhibiti Ubora kutoka Bohari ya Dawa (MSD), akiwaelezea wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) jinsi mashine ya kutengeneza barakoa inavyofanya kazi wakati Kamati hiyo ilipotembelea MSD na kukagua kiwanda hicho na Kiwanda cha kutengeneza dawa cha Keko

Tuesday, March 29, 2022

SPIKA DKT. TULIA ATAKA MABUNGE YA AFRIKA KUJIENDESHA KWA MFUMO WA KIDIGITALI


SPIKA DKT. TULIA ATAKA MABUNGE YA AFRIKA KUJIENDESHA KWA MFUMO WA KIDIGITALI
 
SPIKA DKT. TULIA ATAKA MABUNGE YA AFRIKA KUJIENDESHA KWA MFUMO WA KIDIGITALI



Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Tulia Ackson (Mb), ameshauri Mabunge ya Afrika kujiunga na kujiendesha katika mfumo wa kimtandao katika kuendesha shughuli zake ili kuendana na teknolojia ya sasa.
 
Spika Tulia ameyasema hayo leo Machi 28, 2022 wakati akifungua semina ya Chama cha Mabunge ya Jumuiya ya Madola Kanda ya Afrika (CPA) iliyofanyika katika ukumbi wa hoteli ya Ramada, Jijini Dar es salaam.
 
Pamoja na mambo mengine, amesisitiza kuwa kwa kutumia mfumo wa Bunge mtandao itawawezesha wananchi kupata taarifa mbalimbali za Bunge kwa wakati ikiwa ni pamoja na kuwawezesha kujua yale yote yanayoazimiwa na Bunge lao lakini na wao pia kuwasilisha maoni na ushauri wao. 
 
“Semina hii tunahitaji kuwajengea uwezo Wabunge kutoka Mabunge yote Afrika ili waweze kwenda kushauri kwenye nchi zao, zipo faida nyingi za kuwa na Bunge mtandao kwamaana zipo nyakati Wananchi, watafiti wanahitaji taarifa fulani za Bunge lakini zinamlazimu hadi aende Dodoma wakati angeweza kwa kutumia progam hii akayapata yote kwa wakati” amesema Spika Dkt. Tulia
 
Vilevile Spika Dkt. Tulia amesisitiza mfumo huo utawezesha pia kutoa uwanja mpana wa Wabunge kujadili mambo mbalimbali ya kiuchumi likiwemo suala la mapinduzi ya kilimo.

 

KAMATI YA PAC IMEKAGUA MRADI WA BRT AWAMU YA II


Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), wakipokea maelezo kutoka kwa Meneja Mradi wa mabasi yaendayo kasi (BRT), Barakael Mmari kuhusiana na ujenzi wa Daraja la Mabasi hayo unaondelea katika eneo la Bandari, wajumbe hao wamekagua mradi huo wa Awamu ya II unaotekelezwa na Wakala wa Barabara (TANROADS)

Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC),Mheshimiwa Japhet Hasunga akizungumza wakati Kamati hiyo ilipokuwa inakagua mradi wa mabasi yaendayo kasi (BRT) Awamu ya II unaotekelezwa na Wakala wa Barabara (TANROADS)

 
Meneja Usafirishaji wa mabasi yaendayo kasi (BRT), Mohamed Kugonda akiwaeleza wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), kuhusu Kituo cha abiria cha mabasi hayo cha Kariakoo, wajumbe hao wamekagua mradi huo wa Awamu ya II unaotekelezwa na Wakala wa Barabara (TANROADS)

Meneja Mradi wa mabasi yaendayo kasi (BRT), Barakael Mmari akiwaeleza wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), kuhusu Kituo cha abiria cha mabasi hayo cha Kariakoo, wajumbe hao wamekagua mradi huo wa Awamu ya II unaotekelezwa na Wakala wa Barabara (TANROADS)

 

Monday, March 28, 2022

KAMATI YA PAC IMEKAGUA MRADI WA MAJI MKURANGA UNAOTEKELEZWA NA DAWASA


Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA), Mhandisi Cyprian Luhemeja akiwaonyesha wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) tenki la maji lililopo Mkuranga wakati wajumbe hao walipotembelea DAWASA na kukagua utekelezaji wa mradi wa maji wa Mkuranga
Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), Mheshimiwa Japhet Hasunga akibonyeza kitufe cha kuwashia pampu ya maji  wakati kamati hiyo ilipotembelea na kukagua utekelezaji wa mradi wa maji wa Mkuranga unaotekelezwa na Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA)
Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) wakiangalia tenki la maji lililopo Mkuranga wakati wajumbe hao walipotembelea na kukagua utekelezaji wa mradi wa maji wa Mkuranga unaotekelezwa na Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA)

KAMATI YA BUNGE YA PAC IMETEMBELEA CHUO CHA UALIMU VIKINDU NA KUKAGUA MRADI WA UJENZI NA UKARABATI WA CHUO HICHO

Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) wakiongozwa na Makamu Mwenyekiti wa Kamati, Mheshimiwa Japhet Hasunga wakiangalia kisima cha maji katika Chuo cha Ualimu Vikindu wakati Kamati hiyo ilipotembelea na kukagua mradi wa ujenzi na ukarabati wa Chuo hicho
Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) Mheshimiwa Japhet Hasunga akizungumza wakati Kamati hiyo ilipokuwa inakagua ujenzi wa mabweni katika Chuo cha Ualimu Vikindu, Kamati ya PAC imetembelea Chuo hicho na kukagua mradi wa ujenzi na ukarabati wa Chuo hicho

Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) Mheshimiwa Japhet Hasunga akivalishwa skafu na kijana wa skauti wakati kamati hiyo ilipowasili katika Chuo cha Ualimu Vikindu na kukagua mradi wa ujenzi na ukarabati wa Chuo hicho

 

Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Eliamani Sedoyeka akizungumza katika kikao cha Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) na watendaji wa Chuo cha Ualimu Vikindu wakati kamati hiyo ilipotembelea Chuo hicho na kukagua mradi wa ujenzi na ukarabati wa majengo mbalimbali, katikati ni Makamu Mwenyekiti wa Kamati Mheshimiwa Japhet Hasunga na Mkuu wa Chuo Amina Tou 

Saturday, March 26, 2022

KAMATI YA PAC IMEKAGUA MRADI WA MAJI WA MAKONGO HADI BAGAMAYO UNAOTEKELEZWA NA DAWASA

Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Majisafi na usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA), Mhandisi Cyprian Luhemeja akiwaelezea wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) kuhusu ujenzi wa tenki la maji lililopo eneo la Tegeta A wakati wajumbe hao walipotembelea DAWASA na kukagua utekelezaji wa mradi wa maji wa Makongo hadi Bagamoyo

 

Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Majisafi na usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA), Mhandisi Cyprian Luhemeja akiwaonyesha wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) maeneo mbalimbali katika mradi wa tenki la maji lililopo eneo la Tegeta A wakati wajumbe hao walipotembelea DAWASA na kukagua utekelezaji wa mradi wa maji wa Makongo hadi Bagamoyo

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Majisafi na usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA), Jen.Mstaafu Davis Mwamunyange akizungumza katika kikao cha watendaji
wa mamlaka hiyo na wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), wakati Kamati hiyo ilipotembelea DAWASA na kukagua utekelezaji wa mradi wa maji wa Makongo hadi Bagamoyo, kulia ni Makamu Mwenyekiti wa Kamati, Mheshimiwa Japhet Hasunga
 
Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali(PAC), Mheshimiwa Japhet Hasunga akizungumza wakati kamati hiyo ilipokuwa inakagua ujenzi wa tenki la maji katika eneo la Tegeta A, Kamati ya PAC imetembelea Mamlaka ya Majisafi na usafi wa Mazingira Dar es Salaam  (DAWASA) na kukagua utekelezaji wa mradi wa maji wa Makongo hadi Bagamoyo

 

Friday, March 25, 2022

KAMATI YA PAC IMETEMBELEA NA KUKAGUA MRADI WA NYUMBA ZA MAKAZI ENEO LA MAGOMENI KOTA AWAMU YA II

Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Majengo (TBA), Arch. Daudi Kandoro akiwasilisha maelezo kuhusu mradi wa ujenzi wa nyumba za makazi eneo la Magomeni Kota Awamu ya II kwa wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) wakati wajumbe hao walipotembelea na kukagua mradi huo

Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Majengo (TBA), Arch. Saudi Kandoro akiwaelezea wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) kuhusu mradi wa ujenzi wa nyumba za makazi eneo la Magomeni Kota Awamu ya II wakati wajumbe hao walipotembelea na kukagua mradi huoMtendaji Mkuu wa Wakala wa Majengo (TBA), Arch. Daudi Kandoro akiwaonyesha wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) kuhusu mradi wa ujenzi wa nyumba za makazi eneo la Magomeni Kota Awamu ya I wakati wajumbe hao walipotembelea na kukagua mradi huo.



Thursday, March 24, 2022

KAMATI YA PAC IMETEMBELEA NA KUKAGUA MAABARA YA UTAFITI WA SAMAKI ILIYOPO KUNDUCHI JIJINI DAR ES SALAAM

Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC),Mheshimiwa Japhet Hasunga akizungumza na watendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Uvuvi Tanzania (TAFIRI) wakati Kamati hiyo ilipotembelea na kukagua mradi wa ujenzi wa maabara ya Utafiti wa Samaki iliyopo Kunduchi Jijini Dar es SalaamMkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Uvuvi Tanzania (TAFIRI), Ismail Kimerei akiwakaribisha wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) wakati wajumbe hao walipotembelea na kukagua mradi wa ujenzi wa Maabara ya Utafiti wa Samaki iliyopo Kunduchi Jijini Dar es Salaam

 Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi(uvuvi), Dkt. Rashid Tamatamah akizungumza na wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) wakati wajumbe hao walipotembelea na kukagua mradi wa ujenzi wa Maabara ya Utafiti wa Samaki iliyopo Kunduchi Jijini Dar es Salaam, kulia ni Makamu Mwenyekiti wa Kamati, Mheshimiwa Japhet HazingMshauri Muelekezi wa mradi wa ujenzi wa Maabara ya Utafiti wa Samaki, Yasin Mlingo akiwalezea wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) kuhusu mradi huo ,wakati wajumbe hao walipotembelea na kukagua maabara hiyo iliyopo  Kunduchi Jijini Dar es 
Salaam

Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) wakiwa katika kikao na watendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Uvuvi Tanzania (TAFIRI) wakati wajumbe hao walipotembelea na kukagua mradi wa ujenzi wa Maabara ya Utafiti wa Samaki iliyopo Kunduchi Jijini Dar es Salaam

Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi(uvuvi), Dkt. Rashid Tamatamah akizungumza na wajumbe wa wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) wakati wajumbe hao walipotembelea na kukagua mradi wa ujenzi wa Maabara ya Utafiti wa Samaki iliyopo Kunduchi Jijini Dar es Salaam, katikati ni Makamu Mwenyekiti wa Kamati, Mheshimiwa Japhet Hasunga na kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Taasisi ya Utafiti wa Uvuvi Tanzania (TAFIRI) Yahaya Mgawe

 

SPIKA DKT. TULIA ASHIRIKI KIKAO CHA BARAZA LA UONGOZI LA UMOJA WA MABUNGE DUNIANI (IPU)

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson (Mb), akishiriki Kikao cha Baraza la Uongozi la Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) kilichopokea na kupitisha taarifa mbalimbali, taarifa ya Mkaguzi wa Ndani wa Fedha kwa Mwaka 2021, pamoja na Taarifa za kamati Mbalimbali ikiwemo taarifa ya kamati ya kudumu ya Haki za Binadamu kwa Wabunge, Majukwaa ya Wabunge Wanawake na Vijana. Kikao hicho kimefanyika leo Machi 24, 2022 katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano Bali nchini Indonesia wakati wa Mkutano wa 144 wa IPU.


Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson (Mb), akishiriki Kikao cha Baraza la Uongozi la Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) kilichopokea na kupitisha taarifa mbalimbali, taarifa ya Mkaguzi wa Ndani wa Fedha kwa Mwaka 2021, pamoja na Taarifa za kamati Mbalimbali ikiwemo taarifa ya kamati ya kudumu ya Haki za Binadamu kwa Wabunge, Majukwaa ya Wabunge Wanawake na Vijana. Kikao hicho kimefanyika leo Machi 24, 2022 katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano Bali nchini Indonesia wakati wa Mkutano wa 144 wa IPU. Kuanzia kushoto ni Mhe. Dkt. Joseph Mhagama (Mjumbe wa Baraza la Uongozi), Balozi wa Tanzania nchini Malaysia, Mhe. Dkt. Ramadhani Dau, Mjumbe wa IPU, Mhe. Elibariki Kingu na Mjumbe wa Baraza la Uongozi, Mhe. Esther Matiko


Katibu Mkuu wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU), Ndg. Martin Chungong akizungumza wakati wa Kikao cha Baraza la Uongozi la Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) kilichopokea na kupitisha taarifa mbalimbali, taarifa ya Mkaguzi wa Ndani wa Fedha kwa Mwaka 2021, pamoja na Taarifa za kamati Mbalimbali ikiwemo taarifa ya kamati ya kudumu ya Haki za Binadamu kwa Wabunge, Majukwaa ya Wabunge Wanawake na Vijana. Kikao hicho kimefanyika leo Machi 24, 2022 katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano Bali nchini Indonesia wakati wa Mkutano wa 144 wa IPU. Wapili kulia ni Rais wa Umoja huo, Ndg. Duarte Pacheco

Wajumbe wa Baraza la Uongozi la Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) wakishiriki kikao cha kupokea na kupitisha taarifa mbalimbali, taarifa ya Mkaguzi wa Ndani wa Fedha kwa Mwaka 2021, pamoja na Taarifa za kamati Mbalimbali ikiwemo taarifa ya kamati ya kudumu ya Haki za Binadamu kwa Wabunge, Majukwaa ya Wabunge Wanawake na Vijana. Kikao hicho kimefanyika leo Machi 24, 2022 katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano Bali nchini Indonesia wakati wa Mkutano wa 144 wa IPU.


SPIKA DKT. TULIA AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA MASPIKA WA BUNGE LA SUDAN KUSINI NA MALAWI


Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson (katikati), akizungumza na Spika wa Bunge la Sudan Kusini, Mhe. Jemma Kumba (kulia) pamoja na Spika wa Bunge la Malawi, Mhe. Catherine Hara katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano Bali nchini Indonesia, leo Machi 24, 2022 alipohudhuria Mkutano wa 144 wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU).

SPIKA DKT. TULIA AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA SPIKA WA BARAZA LA WAWAKILISHI YA JAMHURI YA INDONESIA BALI NCHINI INDONESIA


Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson (Mb), akizungumza na Spika wa Baraza la Wawakilishi la Jamhuri ya Indonesia, Mhe. Dkt. Puan Maharani katika Ofisi za Kituo cha Kimataifa cha Mikutano Bali nchini Indonesia, leo Machi 24, 2022 alipohudhuria Mkutano wa 144 wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU).



Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson (Mb), akiangalia zawadi kutoka kwa Spika wa Baraza la Wawakilishi la Jamhuri ya Indonesia, Mhe. Dkt. Puan Maharani katika Ofisi za Kituo cha Kimataifa cha Mikutano Bali nchini Indonesia, leo Machi 24, 2022 alipohudhuria Mkutano wa 144 wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU).


Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson (Mb),  akionyesha zawadi aliyopatiwa na Spika wa Baraza la Wawakilishi la Jamhuri ya Indonesia, Mhe. Dkt. Puan Maharani katika Ofisi za Kituo cha Kimataifa cha Mikutano Bali nchini Indonesia, leo Machi 24, 2022 alipohudhuria Mkutano wa 144 wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU).

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson (Mb), katika picha ya pamoja na Spika wa Baraza la Wawakilishi la Jamhuri ya Indonesia, Mhe. Dkt. Puan Maharani katika Ofisi za Kituo cha Kimataifa cha Mikutano Bali nchini Indonesia, leo Machi 24, 2022 alipohudhuria Mkutano wa 144 wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU).



 Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson (Mb), katika picha ya pamoja na Spika wa Baraza la Wawakilishi la Jamhuri ya Indonesia, Mhe. Dkt. Puan Maharani (katikati) katika Ofisi za Kituo cha Kimataifa cha Mikutano Bali nchini Indonesia, leo Machi 24, 2022 alipohudhuria Mkutano wa 144 wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU), Wengine ni Balozi wa Tanzania nchini Malaysia, Mhe. Dkt. Ramadhani Dau (kushoto) na Wabunge wa Bunge la Tanzania ambao pia ni Wajumbe wa IPU, Kuanzia kulia ni Mbunge wa Chake Chake, Mhe. Ramadhan Suleiman Ramadhan na Mbunge wa Viti Maalum, Mhe. Esther Matiko