WELCOME TO TANZANIA NATIONAL ASSEMBLY OFFICIAL BLOG: CONTACT US: P.O.BOX 941 DODOMA, TANZANIA, WEBSITE: parliament.go.tz , FIND US ON FACEBOOK >>> www.facebook.com/bungetz1, FOLLOW US ON TWITTER >>> @bunge_tz.>>>KARIBUNI

Monday, October 31, 2016

VIDEO: MHE SPIKA AKIZUNGUMZA NA WAANDISHI


MHE SPIKA AKIZUNGUMZIA KUHUSU KUANZA KWA MKUTANO WA TANO WA BUNGEpika wa Bunge Mhe Job Ndugai akizungumza na Waandishi wa Habari Mjini Dodoma kuhusu kuanza kwa Mkutano wa Tano wa Bunge

Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai akizungumza na Waandishi wa Habari Mjini Dodoma kuhusu kuanza kwa Mkutano wa Tano wa Bunge

Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai akizungumza na Waandishi wa Habari Mjini Dodoma kuhusu kuanza kwa Mkutano wa Tano wa Bunge

Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai akizungumza na Waandishi wa Habari Mjini Dodoma kuhusu kuanza kwa Mkutano wa Tano wa Bunge

Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai akizungumza na Waandishi wa Habari Mjini Dodoma kuhusu kuanza kwa Mkutano wa Tano wa Bunge

Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai akizungumza na Waandishi wa Habari Mjini Dodoma kuhusu kuanza kwa Mkutano wa Tano wa Bunge

Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai akizungumza na Waandishi wa Habari Mjini Dodoma kuhusu kuanza kwa Mkutano wa Tano wa Bunge.
MHE SPIKA AZUNGUMZIA KUANZA KWA MKUTANO WA TANO WA BUNGE
Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai ametangaza kuanza kwa vikao vya Mkutano wa Tano wa Bunge la 11 Mjini Dodoma kesho huku akitaja baadhi ya shughuli zitakazofanywa katika Mkutano huo.
Akizungumza na Waandishi wa Habari Ofisini kwake Mjini Dodoma, Mheshimiwa  Spika alisema shughuli ya kwanza itakuwa ni Bunge kukaa kama Kamati ya Mipango kwa mujibu wa Kanuni ya 94 ya Kanuni za Kudumu za Bunge ili  kujadili Mapendekezo ya Mpango wa Taofa unaokusudiwa kutekelezwa na Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2017/ 2018.
Alisema katika mjadala huo wabunge watatoa ushauri kwa Serikali kuhusiana na vyanzo mbalimbali vya mapato na vipaumbele vya kuzingatia wakati Serikali ikiandaa bajeti ijayo.
“Mbali na shughuli hiyo vipindi vya Maswali na Majibu vitakuwepo kama kawaida ikiwemo kipindi cha Maswali kwa Waziri Mkuu kinachokuwepo siku ya Alhamisi,” alisema Mhe Spika.
Alisema pia Katika Mkutano huu, Bunge litapokea Taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) pamoja na majibu ya Serikali kuhusiana na taarifa hiyo.
“Pia Bunge litajadili taarifa Taarifa ya Kamati za Kudumu za Bunge za Hesabu za Serikali (PAC) na Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) kuhusu Hesabu za Serikali Kuu na Serikali za Mitaa zilizokaguliwa kwa mwaka wa Fedha  2014/15 
“Vievile Kamati ya Bunge ya Sheria Ndogo itawasilisha taarifa yake bungeni kuhusu Uchambuzi wa Sheria Ndogo,” alisema 
Aidha, Mheshimiwa Spika alisema jumla ya miswada miwili ya sheria itajadiliwa na kupitishwa ambayo ni Muswada wa Sheria ya Huduma za Habari wa mwaka 2016(The Media Services Bill, 2016), na Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali Na. 3 wa mwaka 2016 (The written Miscellaneous Amendments) (No. 3) Bill, 2016).
Alisema kutakuwepo na semina kwa wabunge wote kuhusu Mkataba wa Makubaliano ya Ushirikiano wa Kiuchumi katika Nchi za Afrika Mashariki na Jumuiya ya Ulaya.
Mwisho.


    

Saturday, October 29, 2016

KAMATI YA HUDUMA NA MAENDELEO YA JAMII YAPOKEA NA KUJADILI MAONI YA WADAU KUHUSU MUSWADA WA SHERIA YA HUDUMA ZA HABARI 2016.

Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii Mhe. Peter Serukamba akifafanua jambo mbele ya kamati hiyo katika kikao kilichofanyika leo Mjini Dodoma. Kulia kwake ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye na Kushoto kwake ni Katibu kamati wa Bunge Ndugu. Pamela Pallangyo
Mjumbe wa kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii Mhe. Mussa Azzan Zungu akichangia jambo mbele ya Wajumbe wa kamati hiyo katika kikao kilichofanyika leo Mjini Dodoma.

Wajumbe wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii wakichambua maoni ya wadau katika Muswada wa Sheria za Huduma za Habari katika kikao kilichofanyika leo Mjini Dodoma.

Friday, October 28, 2016

SPIKA WA BUNGE ALIPOTEMBELEA KAMATI YA SHERIA NDOGO

Spika wa Bunge Mheshimiwa Job Ndugai akitoa ufafanuzi wa jambo alipotembelea Kamati ya Sheria Ndogo katika ukumbi wa Hazina leo Manispaa ya Dodoma

Spika wa Bunge Mheshimiwa Job Ndugai na Mwenyekiti wa Kamati ya Sheria Ndogo wakifurahia jambo baada ya kutembelea Kamati hiyo leo.

Mmoja wa wajumbe wa Kamati ya Sheria Ndogo akichangia mada baada ya Spika wa Bunge Mheshimiwa Job Ndugai na ofisi yake kuwasili katika Kamati hiyo.

Thursday, October 27, 2016

KAMATI YA PAC YAENDELEA NA VIKAO VYAKE DODOMA

Mwenyekiti wa Kamati ya Hesabu za Mashirika ya Umma (PAC), Mheshimiwa Naghenjwa Kaboyoka akiongoza kikao cha Kamati hiyo ambapo  Kamati  ilikataa taarifa hesabu za shirika la Maendeleo ya Petrol  (TPDC) zinazoishia mwaka 2014/15 kutokana na taarifa hiyo kuchelewa kuwasilishwa katika Kamati.

Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Maendeleo ya Petrol (katikakati), Profesa Sufian Bukurura akisikiliza hoja za Kamati katika kikao hicho leo Mjini Dodoma wa kwanza kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Shirika hilo, Ndg.Kapulya Msomba.


Mjumbe wa Kamati ya Hesabu za Serikali (PAC), Dkt.Haji Mponda akiuhoji uongozi wa Shirika la Maendeleo (TPDC) kwa kuchelewa kuwasilisha taarifa yao mbele ya Kamati hiyo

Wednesday, October 26, 2016

KAMATI YA KATIBA NA SHERIA YAPOKEA TAARIFA YA OFISI YA WAZIRI MKUU-SERA, BUNGE, KAZI, AJIRA, VIJANA NA WALEMAVU

Mmoja wa wajumbe wa Kamati ya Katiba na Sheria akichangia mada baada ya Ofisi ya Waziri Mkuu- Sera, Bunge,Kazi,Ajira, Vijana na Walemavu kuwasilisha taarifa kuhusu utekelezaji wa shughuli za Mamlaka ya Usimamizi wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii (SSRA)

 Ofisi ya Waziri Mkuu- Sera, Bunge,Kazi,Ajira, Vijana na Walemavu walipowasilisha taarifa kuhusu utekelezaji wa shughuli za Mamlaka ya Usimamizi wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii (SSRA)

Mwenyekiti wa Kamati ya Katiba na Sheria akitoa ufafanuzi leo katika vikao vyake baada ya Ofisi ya Waziri Mkuu- Sera, Bunge,Kazi,Ajira, Vijana na Walemavu kuwasilisha taarifa kuhusu utekelezaji wa shughuli za Mamlaka ya Usimamizi wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii (SSRA)

PAC yakutana na TANESCO

Mjumbe wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), Mheshimiwa Japhet Hasunga akiuliza swali kwa maafisa wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) wakati Kamati hiyo ilipokuwa ikichambua Taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kuhusu hoja za ukaguzi za Shirika hilo.

Maafisa kutoka Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) wakiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika hilo, Felchesmi Mramba wakiwa mbele ya wajumbe wa Kamati ya Hesabu za Serikali kujibu hoja za wajumbe wa Kamati hiyo kuhusiana Taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kuhusu hoja za ukaguzi za Shirika hilo.