WELCOME TO TANZANIA NATIONAL ASSEMBLY OFFICIAL BLOG: CONTACT US: P.O.BOX 941 DODOMA, TANZANIA, WEBSITE: parliament.go.tz , FIND US ON FACEBOOK >>> www.facebook.com/bungetz1, FOLLOW US ON TWITTER >>> @bunge_tz.>>>KARIBUNI

Thursday, April 30, 2020

WABUNGE WANAWAKE WAPATIWA MAFUNZO KUHUSU YA SHERIA ZA MIRATHI



Afisa wa Bunge Ndg. Seraphine Tamba akifafanua jambo alipokuwa akitoa mada kwenye Kikao cha kuwawezesha Wabunge Wanawake juu ya Uelewa wa Utata na Uwiano usio sawa wa Mgawanyo wa Mirathi kwa Wajane na Wagane (Sheria za Mirathi) kwenye Ukumbi wa Msekwa Bunge Jijini Dodoma hii leo.
Mwenyekiti wa Umoja wa Wabunge Wanawake (TWPG) Mheshimiwa Margret Sitta akifafanua jambo alipokuwa kwenye Kikao cha kuwawezesha Wabunge Wanawake juu ya Uelewa wa Utata na Uwiano usio sawa wa Mgawanyo wa Mirathi kwa Wajane na Wagane (Sheria zaMirathi) kwenye Ukumbi wa Msekwa Bunge Jijini Dodoma hii leo.
Sehemu ya Wabunge Wanawake wakifuatilia jambo kwenye Kikao cha kuwawezesha Wabunge Wanawake juu ya Uelewa wa Utata na Uwiano usio sawa wa Mgawanyo wa Mirathi kwa Wajane na Wagane (Sheria zaMirathi) kwenye Ukumbi wa Msekwa Bunge Jijini Dodoma hii leo.

Saturday, April 18, 2020

MHESHIMIWA ZUNGU AFUNGUA MAFUNZO KWA WABUNGE KUHUSU USIMAMIZI WA MISITU YA ASILI NCHINI

Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira, Mheshimiwa Mussa Zungu akizungumza jambo alikuwa mgeni rasmi kwenye ufunguzi wa mafunzo ya kuwajengea uwezo wabunge juu ya usimamizi bora wa misitu ya asili iliyomo nchini. 


Mwenyekiti wa Chama cha Wabunge Marafiki wa Mazingira Mheshimiwa Jitu Soni akizungumza jambo kwenye ufunguzi wa mafunzo ya kuwajengea uwezo wabunge juu ya usimamizi bora wa misitu ya asili iliyomo nchini. 


Mtaalam mwezeshaji kutoka Shirika la Kuhifadhi Misitu ya Asili Tanzania (TFCG) Ndg. Charles Meshack akielezea jambo kwenye mafunzo yalitolewa kuwajengea uwezo Wabunge juu ya ya Usimamizi bora wa misitu ya asili nchini.

Mkurugenzi wa Wakala wa Misitu Tanzania ((TFS) Prof. Dos Santos Silayo akielezea jambo kwenye mafunzo yalitolewa kuwajengea uwezo Wabunge juu ya ya Usimamizi bora wa misitu ya asili nchini. 


MHESHIMIWA ZUNGU AFUNGUA MAFUNZO KWA WABUNGE KUHUSU USIMAMIZI WA MISITU YA ASILI NCHINI

Wabunge wanaounda Chama cha Wabunge Marafiki wa Mazingira (TAPAFE) wamepewa mafunzo ya kuwajengea uwezo wabunge juu ya usimamizi bora wa misitu ya asili iliyomo nchini.
Akizungumza katika mafunzo hayo Mgeni rasmi ambaye ni Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira, Mheshimiwa Mussa Zungu alisema kutokana na kutoweka kwa kasi kwa misitu mingi ya asili, Wizara yake inalo jukumu kubwa kuhakikisha hali hiyo inadhibitiwa kwa kushirikiana na wananchi.
Aidha, Mheshimiwa Zungu alitoa wito kwa wananchi kujikita kwenye matumizi ya nishati mbadala ikiwemo Gesi na Makaa ya mawe ili kukabiliana na upotevu mkubwa wa misitu ya asili na kuepusha uchafuzi wa mazingira unaotokana na hewa ukaa ambayo huzalishwa na kuni na mkaa.
Alisema “pamoja na juhudi zote zinazofanywa na Serikali ya awamu ya tano, Wadau wa maendeleo pamoja na Sekta binafsi, wananchi tuna wajibu wa kushirikiana na wadau hawa ili kukomesha uharibifu wa misitu kwa kujikita kwenye matumizi ya nishati mbadala”
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Wabunge wanaounda Chama cha Wabunge Marafiki wa Mazingira (TAPAFE) Mheshimiwa Jitu Soni alimhakikishia Mheshimiwa Waziri kuwa Chama hicho kiko tayari kusaidiana na Serikali kutoa elimu sehemu mbalimbali nchini juu ya umuhimu wa kuhifadhi misitu.
Naye mtaalam mwezeshaji kutoka Shirika la Kuhifadhi Misitu ya Asili Tanzania (TFCG) Ndg. Charles Meshack alisema, kati ya hekta milioni 22 za ardhi zilizoko chini ya Vijiji ni hekta milioni 2 pekee ndizo zinazohifadhiwa na mamlaka za Serikali na hivyo kufanya sehemu kubwa ya ardhi ya Vijiji kuwa hatarini kuharibiwa.
Akichangia mada katika mafunzo hayo, Mkurugenzi wa Wakala wa Misitu Tanzania (TFS) Prof. Dos Santos Silayo alisema takwimu zinaonyesha kuwa Serikali inapoteza mapato ya shilingi bilioni 200 kila mwaka kutokana na kukosekana kwa usimamizi wa misitu iliyo chini ya mamlaka za Vijiji huku hekta laki 4 za misitu zikitoweka kila mwaka sambamba na hilo.
Mafunzo hayo yaliyohudhuriwa na Wabunge ambao ni wajumbe wa Kamati za Ardhi, Maliasili na Utalii na Kamati ya Viwanda, Biashara na Mazingira yalifanyika kwenye Ukumbi wa Msekwa Bungeni Jijini Dodoma hii leo.
Mwisho.

Thursday, April 2, 2020

NAIBU SPIKA AKABIDHIWA TUZO NA BARAZA LA WATU WANAOISHI NA VIRUSI VYA UKIMWI NCHINI (NACOPHA)

Naibu Spika Mheshimiwa Dkt Tulia Ackson akipokea tuzo maalum ya kuthamini mchango wake katika kupambana na Ukimwi na Kifua kikuu nchini iliyotolewa na Baraza la Watu wanaoishi na Virusi vya Ukimwi nchini (NACOPHA) na kukabidhiwa kwake na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya masuala ya Ukimwi Mheshimiwa Oscar Mukasa hii leo Ofisini kwake Jijini Dodoma.

Naibu Spika Mheshimiwa Dkt Tulia Ackson akiwa katika picha ya pamoja na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya masuala ya Ukimwi Mheshimiwa Oscar Mukasa aliyemkabidhi tuzo maalum ya kuthamini mchango wake katika kupambana na Ukimwi na Kifua kikuu nchini iliyotolewa na Baraza la Watu wanaoishi na Virusi vya Ukimwi nchini (NACOPHA) hii leo Ofisini kwake Jijini Dodoma.