WELCOME TO TANZANIA NATIONAL ASSEMBLY OFFICIAL BLOG: CONTACT US: P.O.BOX 941 DODOMA, TANZANIA, WEBSITE: parliament.go.tz , FIND US ON FACEBOOK >>> www.facebook.com/bungetz1, FOLLOW US ON TWITTER >>> @bunge_tz.>>>KARIBUNI

Wednesday, March 8, 2017

TAARIFA KUHUSU VIKAO VYA KAMATI ZA BUNGE


Kamati ya Bunge yatua Loliondo kusaka suluhuKamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imefanya ziara katika  katika Pori Tengefu la Loliondo ili kujionea  hali hailisi ya mgogogro  wa muda mrefu katika pori hilo kwa kutembelea baadhi ya maeneo muhimu ambayo ndio hutajwa kama kiini cha mgogoro huo.
Mwenyekiti wa kamati hiyo Mheshimiwa Muhandisi Atashasta  Nditiye anasema wamejionea walicho kiona na wataishauri serikali ipasavyo ili iweze kutoa maamuzi sahihi ili kumaliza mvutano wa muda mrefu katika eneo hilo
Mheshimiwa Mhandisi Nditiye amesema wajumbe wa kamati hiyo, wamefanikiwa kupita sehemu kubwa ya eneo hilo, ambalo linapendekezwa kugawanywa ili kutengwa eneo la kilomita 1500 kwa ajili ya uhifadhi wa ikolojia ya Serengeti.
Akitoa maelezo kwa wajumbe wa kamati hiyo, Mhifadhi mkuu wa hifadhi ya Serengeti, William Mwakilema alisema kwa manufaa yaTaifa na dunia ni muhimu kutengwa eneo la kilomita 1500 ili lihifadhiwe.
Alisema eneo hilo ambalo ni mapito ya nyumbu kutoka hifadhi ya Masai Mara nchini Kenya, hadi Serengeti na baadaye hifadhi ya Ngorongoro pia ndio eneo la mazalia ya nyumbu na vyanzo vya maji, limeharibiwa sana na mifugo na shughuli za kibinaadamu na lisipo hifadhiwa uhai wa Serengeti upo mashakani.
Hata hivyo, Mwenyekiti wa halmashauri ya Loliondo, Methew Siloma alisema msimamo wao bado wanapinga kutengwa eneo hilo kwa kuwa ni la vijiji na wanataka kutafutwa suluhu.
Mbunge Geita, Joseph Kasheku (Msukuma) ambaye ni mjumbe wa kamati hiyo alieleza kuwa ameona udhaifu uliopo katika utunzwaji wa eneo hilo na kutaka jamii inayozunguka eneo hili ishirikishe ili kutambua umuhimu wa eneo hilo.
Wabunge wengine Mheshimiwa Grace Kiwelu na mheshimiwa Lucy Owenya wa viti maalum mkoa Kilimanjaro wameshauri kutazamwa maslahi mapana ya taifa katika kulinda ikolojia ya Serengeti.
Kwaupande wake Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe, alisema dhamira ya serikali ni kuhakikisha ikolojia ya Serengeti inalindwa kwa manufaa ya sasa na vizazi vijavyo.
Eneo hilo la pori Tengefu la Loliondo lenye kilomita za mraba 4000, limeingia katika mgogoro baada ya wizara ya Maliasilina Utalii, kutangaza uamuzi ya kutaka kulitenga eneo la kilomita 1500 kwa ajili ya uhifadhi na eneo lililobaki kurejeshwa kwa halmashauri ya Ngorongoro.

Mtafiti mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori Tanzania Dkt. Edward Kohi(wa kwanza kulia) akitoa maelezo ya kitaalamu kwa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi maliasili na Utalii waliotembelea Pori Tengefu la Loliondo, wilayani Ngorongoro mkoani Arusha.

Waziri wa Maliasili na utalii Mhe. Prof Jumanne Maghembe akifafanua jambo kwa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii wakati walipotembelea Pori Tengefu la Loliondo

Mfugaji wa jamii ya kimasai Senditwa Maseke akiwaeleza jambo kwa baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi maliasili na Utalii baada ya kukumkuta akichunga ng’ombe ndani ya Pori Tengefu la Loliondo

Friday, February 3, 2017

SPIKA WA BUNGE MHE. JOB NDUGAI ASHIRIKI MAADHIMISHO YA SIKU YA SHERIA JIJINI DAR ES SALAAM

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akimkabidhi Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai nakala ya ripoti ya mahakama kuhusu kesi za uchaguzi kutoka kwa Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania Profesa Ibrahim Hamisi Juma (kulia) wakati kuadhimisha siku ya Sheria Nchini iliyoambatana na uzinduzi wa Mwaka Mpya wa Kimahakama katika viwanja vya Mahakama vya Mtaaa wa Chimala Ocean Road jijini Dar es Salaam.

Spika wa Bunge Mhe. Mhe Job Ndugai akitoa salamu kwa niaba ya Bunge baada ya kukaribishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli wakati wa maadhimisho ya Siku ya Sheria Nchini katika viwanja vya Mahakama vya Mtaaa wa Chimala Ocean Road jijini Dar es salaam.Kushoto kwake ni Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe. Omar Othman Makungu

Spika wa Bunge Mhe. Mhe Job Ndugai akitoa salamu kwa niaba ya Bunge baada ya kukaribishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli wakati wa maadhimisho ya Siku ya Sheria Nchini katika viwanja vya Mahakama vya Mtaaa wa Chimala Ocean Road jijini Dar es salaam. Kushoto kwake ni Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe. Omar Othman Makungu

Spika wa Bunge Mhe. Mhe Job Ndugai akiagana na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli mara baada ya maadhimisho ya Siku ya Sheria Nchini yaliyofanyika katika viwanja vya Mahakama vya Mtaaa wa Chimala Ocean Road jijini Dar es salaam

Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai akiwa katika Picha ya pamoja na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli, Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania Profesa Ibrahim Hamisi Juma, pamoja na majaji wengine wa Mahakama wakati maadhimisho ya Siku ya Sheria Nchini yaliyofanyika katika viwanja vya Mahakama vya Mtaaa wa Chimala Ocean Road jijini Dar es salaam

Wednesday, February 1, 2017

WABUNGE WANNE WAPYA WALA KIAPO CHA UAMINIFU


  Mhe. Alhaji Abdallah Majura Bulembo (Mbunge wa Kuteuliwa na Mhe Rais) akila Kiapo cha Uaminifu mbele ya Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Job Y. Ndugai.
 Mhe. Ali Juma Ali - ( Mbunge wa Jimbo la Dimani) akila Kiapo cha Uaminifu.

 
 Mhe. Prof. Palamagamba John Kabudi (Mbunge wa Kuteuliwa na Mhe Rais) akila Kiapo cha Uamimifu
Mhe. Anne Kilango Malecela(Mbunge wa Kuteuliwa na Mhe Rais) akila kiapo cha Uaminifu

Wednesday, January 25, 2017

TAMISEMI yawasilisha taarifa ya ukusanyaji mapato kwa njia ya kielektroniki kwa Kamati

 Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa wakipokea na Kujadili Taarifa ya Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa kuhusu Tathimini ya Mfumo wa Ukusanyaji Mapato kwa njia ya Kielektroniki katika Halmashauri nchini na Utekelezaji wa zoezi la kubaini Wanafunzi hewa katika Shule za Msingi na Sekondari za Serikali nchini.
  Mkurugenzi wa Idara ya  Teknolojia ya Habari na Mawasiliano OR – TAMISEMI, Erick Kitali, akiwasilisha Taarifa ya Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa kuhusu Tathimini ya Mfumo wa Ukusanyaji Mapato kwa njia ya Kielektroniki katika Halmashauri nchini na Utekelezaji wa zoezi la kubaini Wanafunzi hewa katika Shule za Msingi na Sekondari za Serikali nchini mbele ya kamati hiyo.
  Naibu Waziri  OR – TAMISEMI, Mhe. Selemani Jafo akifafanua jambo mbele ya Kamati ya akifafanua jambo mbele ya Kamati hiyo.