WELCOME TO TANZANIA NATIONAL ASSEMBLY OFFICIAL BLOG: CONTACT US: P.O.BOX 941 DODOMA, TANZANIA, WEBSITE: parliament.go.tz , FIND US ON FACEBOOK >>> www.facebook.com/bungetz1, FOLLOW US ON TWITTER >>> @bunge_tz.>>>KARIBUNI

Friday, December 15, 2017

SPIKA APOKEA BARUA ZA WABUNGE WAWILI KUJIUZULU UBUNGE

Spika wa Bunge Mheshimiwa Job Ndugai akifafanua jambo mbele ya Waandishi wa Habari Mjini Dodoma baada ya kupokea barua ya Mhe. Said Abdalah Mtulia (CUF) na Mhe. Dkt. Godwin Aloyce Mollel (CHADEMA) ambao wamejiuzulu Ubunge, Mheshimiwa Spika amesema ameiandikia barua Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) ili iendelee na hatua nyingine.
Spika wa Bunge Mheshimiwa Job Ndugai akizungumza na Waandishi wa Habari Mjini Dodoma baada ya kupokea barua ya Mhe. Said Abdalah Mtulia (CUF) na Mhe. Dkt. Godwin Aloyce Mollel (CHADEMA) ambao wamejiuzulu Ubunge, Mheshimiwa Spika amesema ameiandikia barua Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) ili iendelee na hatua nyingine.


Monday, December 4, 2017

SPIKA NDUGAI AFUNGUA MASHINDANO YA NANE YA MABUNGE YA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI JIJINI, DAR ES SALAAM

 Spika wa Bunge Mheshimiwa Job Ndugai akiwatambulisha Waheshimiwa Wabunge wa Bunge la Tanzania wakati wa ufunguzi wa Mashindano ya Kimichezo ya Mabunge ya  Jumuiya ya Afrika Mashariki katika ukumbi wa Sabasaba Jijini, Dar es Salaam
 Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai (watatu toka kulia) katika picha ya pamoja na Wageni wa meza kuu wakati wa ufunguzi huo
 Waheshimiwa Wabunge wa Tanzania wakifanya usajili wakati wa ufunguzi huo
Washiriki wa Mashindano ya Mabunge ya Jumuiya ya Afrika Mashariki ambao ni Waheshimiwa Wabunge na Watumishi wa Mabunge hayo wakifuatilia ufunguzi wa Mashindano hayo Jijini Dar es Salaam

 Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa (wa tano toka kulia mstari wa mbele) akiongoza Wageni waalikwa na Wachezaji wa Timu za Bunge la Tanzania na Burundi kuimba nyimbo ya Taifa ya Mataifa yao kabla ya kuanza kwa mechi baina ya timu hizo Uwanja wa Taifa ikiwa ni sehemu ya mashindano ya Mabunge ya Afrika Mashariki
 Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa akiwasalimia wachezaji wa Timu ya Bunge la Burundi kabla ya kuanza kwa mechi yao na Timu ya Tanzania ikiwa ni sehemu ya mashindano ya Mabunge ya Afrika Mashariki
Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa akiwasalimia wachezaji wa Timu ya Bunge la Tanzania kabla ya kuanza kwa mechi yao na Timu ya Burundi  ikiwa ni sehemu ya mashindano ya Mabunge ya Afrika Mashariki

 Waziri Mkuu wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa akiteta jambo na Kocha wa Timu ya Bunge la Tanzania Mhe. Venance Mwamoto kabla ya kuanza kwa mechi kati ya Timu ya Bunge la Tanzania na Burundi katika Uwanja wa Taifa Jijini Dar
Naibu Spika Dkt. Tulia Ackson akiwasalimia wachezaji wa Timu ya Bunge la Tanzania kabla ya kuanza kwa mechi yao na Timu ya Burundi  ikiwa ni sehemu ya mashindano ya Mabunge ya Afrika Mashariki


 Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa akizungumza na Wachezaji wa  Timu ya Bunge la Tanzania na Burundi (hawapo pichani)  kabla ya kuanza kwa mechi baina ya timu hizo Uwanja wa Taifa ikiwa ni sehemu ya mashindano ya Mabunge ya Afrika Mashariki
Kikosi cha Bunge la Tanzania

Kikosi cha Bunge la Burundi 

Na Debora Sanja-Bunge
Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai amefungua mashindano ya Nane ya Mabunge ya Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki huku akisisitiza michezo hiyo kudumisha umoja na ushirikiano katika Jumuiya hiyo.

Akizungumza katika ufunguzi wa michezo hiyo uliofanyika katika Ukumbi wa Sabasaba Jijini Dar es Salaaam alisema mbali na michezo kuimarisha afya lakini pia inadumisha umoja baina ya nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki.

“Tutumie michezo hii kudumisha ushirikiano uliopo ndani ya Nchi za Afrika Mashariki ili uzidi kuwa na nguvu na Umoja huu uwe mfano kwa Nchi nyingine za Afrika,” alisema.

Alisema Tanzania ikiwa mwenyeji wa Mashindano hayo imejipanga kuhakikisha yanafanyika na kumalizika kwa usalama kwa kuwa hali ya Ulinzi na Usalama imeimarishwa.
Aidha, alisema Timu za Bunge za Tanzania zimejiandaa kisawasawa kuchukua ushindi katika michezo yote.

Kwa upande wake Spika wa Bunge la Seneti la Burundi, Mheshimiwa Reverien Ndikuriyo alishukuru kwa mapokezi mazuri kutoka Tanzania na kusisitiza pia kudumisha umoja katika michezo hiyo.

Awali akitoa maelezo ya mashindano hayo, Katibu wa Bunge, Ndugu Stephen Kagaigai alisema michezo hiyo imeshirikisha Nchi nne za Uganda, Burundi, Kenya na Tanzania pamoja na Timu ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC).
Alisema Nchi za Rwanda na Sudan ya Kusini wameomba udhuru wa kutoshiriki mashindano haya kwa mwaka huu.

Naye Mwenyekiti wa Timu ya Bunge, Mheshimiwa William Ngeleja aliitaja michezo itakayochezwa katika mashindano hayo kuwa ni mpira wa miguu, mpira wa kikapu, mpira wa wavu, mpira wa pete, riadha, kuvuta kamba na gofu.

Baadhi ya viongozi wengine waliohudhuria hafla ya uzinduzi huo ni pamoja na Naibu Spika wa Bunge la Tanzania, Dkt. Tulia Ackson, Naibu Spika wa Bunge la Kenya, Mheshimiwa Moses Cheboi, Kiongozi wa Upinzani kutoka Bunge la Uganda, mabalozi na viongozi wa vyombo vya ulinzi na usalama.

Mara baada ya uzinduzi kulifanyika mchezo wa riadha na kuvuta kamba ambapo katika mchezo wa riadha Timu ya Wanawake ya Bunge la Tanzania iling’ara huku kwa wanaume Timu ya Kenya iliongoza.

Kwa upande wa Kuvuta Kamba Timu ya wanaume ya Tanzania iliibuka na ushindi huku wanawake ilishinda Timu ya Kenya.

  • Waziri Mkuu awaasa Wchezaji
 Waziri Mkuu , Mheshimiwa Kassim Majaliwa amezitaka Timu za Mabunge ya Jumuiya ya Afrika Mashariki kucheza kwa kufuata viwango vya Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) ili michezo hiyo izidi kudumisha umoja na ushirikiano kwa nchi za Jumuiya hiyo.



Mheshimiwa Majaliwa  ametoa Rai hiyo wakati akifungua mashindano ya Mpira wa Miguu katika Tanzania na Burundi yaliyofanyika katika Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam.



Alisema pamoja na kwamba kila nchi inahitaji ushindi lakini inapokuwa inatafuta ushindi huo iangalia jinsi gani inawapa Watanzania Burudani kwa kuzingatia viango hivyo vya ‘Fair Play’.



“Leo tunaanza mashindano ya Mpira wa Miguu, najua kila nchi inahitaji ushindi lakini hata hivyo tunangalie burudani tunayowapa Watanzania, tuangalie Sheria za FIFA za ‘Fair Play’, kila mtu aendelee kucheza bila dosari na ninawatakia mchezo mwema kila mmoja apate amafanikio,” alisema.



Waziri Mkuu alisema nchi zote zinashiriki mashindano hayo ni  ndugu hivyo ni vema wakayatumia katika kuimarisha ushirikiano wa Mabunge ya Jumuiya hiyo. 



Katika ufunguzi huo Waziri Mkuu aliambatana na Naibu Spika wa Bunge la Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Tulia Ackson, Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Mheshimiwa Dkt.  Harrison Mwakyembe pamoja na Katibu wa Bunge la Tanzania Stephen Kagaigai.



Katika mechi ya kwa kwanza timu ya Bunge la Tanzania imeibuka kidedea baada ya kuibamiza magoli matatu (3) kwa mawili (2) Timu ya Bunge la Burundi.


Katika mechi ya pili iliyowakutanisha Timu ya Uganda na Kenya ambapo Timu ya Bunge la Uganda iliibuka kidedea baada ya kuibugiza magoli saba (7)  kwa sifuri (0) Timu ya Bunge la Kenya.

  •  Sambamba na hilo ,
Mke wa Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne, Mheshimiwa Salma Kikwete (Mb) ,amewataka wachezaji wa Timu za Mabunge ya Jumuiya ya Afrika Mashariki wanaposhiriki mashindano hayo wazingatie kwamba michezo ni afya.



Mama Salma ametoa kauli hiyo wakati akifungua mashindano ya Mpira wa Wavu kwa Timu za wanaume za Bunge la Kenya na Tanzania.



Alisema mbali na burudani lakini pia wachezaji watambue kwamba michezo ni afya hivyo wajitokeze kwa wingi kushirii mashindano hayo kwa ajili ya kuimarisha afya zao.



“Mnashiriki mashindano haya, naomba mtambue kuwa mbali na burudani, pia michezo ni afya, undugu na unadumisha uyshirikiano hivyo ni vizuri tukiidumisha,’ alisema.



Katika mchezo huo Timu ya Bunge la Kenya iliibuka mshindi kwa kuifunga Timu ya Bunge la Tanzania kwa seti 3 – 1.


Katika Mechi nyingine Timu ya Mpira wa Pete ya Bunge la Uganda iliibuka kidedea dhidi ya Timu ya Bunge la Kenya.