WELCOME TO TANZANIA NATIONAL ASSEMBLY OFFICIAL BLOG: CONTACT US: P.O.BOX 941 DODOMA, TANZANIA, WEBSITE: parliament.go.tz , FIND US ON FACEBOOK >>> www.facebook.com/bungetz1, FOLLOW US ON TWITTER >>> @bunge_tz.>>>KARIBUNI

Friday, April 21, 2023

SPIKA DKT. TULIA, KAMATI YA BUNGE YA MAMBO YA NJE WAFANYA MAZUNGUMZO NA KAMATI TEULE YA MHE. RAIS YA KUTATHMINI UFANISI NA UTENDAJI WA WIZARA YA MAMBO YA NJE



Spika wa Bunge, Mhe. Dkt. Tulia Ackson akizungumza na Wajumbe wa Kamati teule ya Mhe. Rais ya kutathmini ufanisi na utendaji wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakiongozwa na Mwenyekiti, Balozi Mstaafu, Mhe. Hassan Yahya (Kulia kwake) walipomtembelea leo tarehe 20 Aprili, 2023 Bungeni Jijini Dodoma.



Mwenyekiti wa Kamati teule ya Mhe. Rais ya kutathmini ufanisi na utendaji wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Mstaafu Hassan Yahya akizungumza jambo wakati wa kikao kati ya Wajumbe wa kamati hiyo na Spika wa Bunge, Mhe. Dkt. Tulia Ackson (hayupo kwenye picha) kilichofanyika leo tarehe 20 Aprili, 2023 Bungeni Jijini Dodoma.




Wajumbe wa Kamati teule ya Mhe. Rais ya kutathmini ufanisi na utendaji wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakiwa katika kikao na Spika wa Bunge, Mhe. Dkt. Tulia Ackson (hayupo kwenye picha) walipomtembelea leo tarehe 20 Aprili, 2023 Bungeni Jijini Dodoma.


Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, Mhe. Vita Kawawa akiongoza kikao kati ya Wajumbe wa Kamati hiyo na Wajumbe wa Kamati teule ya Mhe. Rais ya kutathmini ufanisi na utendaji wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakiongozwa na Mwenyekiti, Balozi Mstaafu, Mhe. Hassan Yahya (kushoto kwake) walipowatembelea leo tarehe 20 Aprili, 2023 Bungeni Jijini Dodoma.



Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, Mhe. Cosato Chumi akizungumza jambo wakati wa kikao cha kamati hiyo na Wajumbe wa Kamati teule ya Mhe. Rais ya kutathmini ufanisi na utendaji wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki walipowatembelea leo tarehe 20 Aprili, 2023 Bungeni Jijini Dodoma.



Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama wakiwa katika kikao cha kamati hiyo na Wajumbe wa Kamati teule ya Mhe. Rais ya kutathmini ufanisi na utendaji wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakiongozwa na Mwenyekiti, Balozi Mstaafu, Mhe. Hassan Yahya walipowatembelea leo tarehe 20 Aprili, 2023 Bungeni Jijini Dodoma. Kuanzia Kushoto ni Mbunge wa Viti Maalum, Mhe. Neema Lugangira, Mbunge wa Lupembe, Mhe. Edwin Swalle na Mbunge wa Ukerewe, Mhe. Joseph Mkundi.