WELCOME TO TANZANIA NATIONAL ASSEMBLY OFFICIAL BLOG: CONTACT US: P.O.BOX 941 DODOMA, TANZANIA, WEBSITE: parliament.go.tz , FIND US ON FACEBOOK >>> www.facebook.com/bungetz1, FOLLOW US ON TWITTER >>> @bunge_tz.>>>KARIBUNI

Wednesday, September 21, 2022

SPIKA DKT. TULIA AFANYA MAZUNGUMZO NA WABUNGE KUTOKA BUNGE LA ZIMBABWE JIJINI DODOMA




Spika wa Bunge, Mhe. Dkt. Tulia Ackson akizungumza na Wabunge kutoka Bunge la Zimbabwe ambao pia ni Wajumbe wa kamati ya Afya na Huduma kwa Watoto kutoka Bunge hilo wakiongozwa na Kaimu Mwenyekiti wa kamati hiyo, Kanali Mstaafu Dkt. Joshua Murire (kulia) katika kikao kilichofanyika leo tarehe 21 Septemba, 2022 Bungeni Jijini Dodoma.



Spika wa Bunge, Mhe. Dkt. Tulia Ackson akimpatia zawadi yenye mfano wa jengo la Bunge, Mbunge kutoka Bunge la Zimbabwe ambae pia ni Kaimu Mwenyekiti wa kamati ya Afya na Huduma kwa Watoto, Kanali Mstaafu Dkt. Joshua Murire pale ugeni kutoka Bunge hilo ulipomtembelea leo tarehe 21 Septemba, 2022 Bungeni Jijini Dodoma.



Spika wa Bunge, Mhe. Dkt. Tulia Ackson akiwa katika picha ya pamoja na Wabunge kutoka Bunge la Zimbabwe ambao pia ni Wajumbe wa kamati ya Afya na Huduma kwa Watoto wakiongozwa na Kaimu Mwenyekiti wa kamati hiyo, Kanali Mstaafu Dkt. Joshua Murire (kulia kwake) baada ya mazungumzo yaliyofanyika leo tarehe 21 Septemba, 2022 Bungeni Jijini Dodoma. 

SPIKA DKT. TULIA AFANYA MAZUNGUMZO NA BALOZI WA JAPAN NCHINI TANZANIA

Spika wa Bunge, Mhe. Dkt. Tulia Ackson akisalimiana na Balozi wa Japan nchini Tanzania ambaye pia ni Mwakilishi wa Japan katika Jumuiya ya Afrika Mashariki, Mhe. Yusushi Misawa alipomtembelea leo tarehe 21 Septemba, 2022 Bungeni Jijini Dodoma.





Spika wa Bunge, Mhe. Dkt. Tulia Ackson akizungumza na Balozi wa Japan nchini Tanzania ambaye pia ni Mwakilishi wa Japan katika Jumuiya ya Afrika Mashariki, Mhe. Yusushi Misawa alipomtembelea leo tarehe 21 Septemba, 2022 Bungeni Jijini Dodoma.



Spika wa Bunge, Mhe. Dkt. Tulia Ackson akimpatia zawadi yenye mfano wa jengo la Bunge Balozi wa Japan nchini Tanzania ambaye pia ni Mwakilishi wa Japan katika Jumuiya ya Afrika Mashariki, Mhe. Yusushi Misawa alipomtembelea leo tarehe 21 Septemba, 2022 Bungeni Jijini Dodoma.


Spika wa Bunge, Mhe. Dkt. Tulia Ackson akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Japan nchini Tanzania ambaye pia ni Mwakilishi wa Japan katika Jumuiya ya Afrika Mashariki, Mhe. Yusushi Misawa alipomtembelea leo tarehe 21 Septemba, 2022 Bungeni Jijini Dodoma. 

Tuesday, September 20, 2022

KAMATI YA BUNGE YA MASUALA YA UKIMWI, HUDUMA NA MAENDELEO YA JAMII ZAFANYA MAZUNGUMZO NA KAMATI YA AFYA NA HUDUMA KWA WATOTO KUTOKA BUNGE LA ZIMBABWE


Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Masuala ya Ukimwi, Udhibiti wa dawa za kulevya na Ugonjwa wa Kifua kikuu, Mhe. Fatma Toufiq (katikati) akiongoza mazungumzo kati ya Wajumbe wa kamati hiyo, Kamati ya Huduma na Maendeleo ya Jamii pamoja na kamati ya Afya na Huduma kwa Watoto kutoka Bunge la Zimbawe wakiongozwa na Kaimu Mwenyekiti wa kamati hiyo, Kanali Mstaafu Dkt. Joshua Murire (kulia) katika kikao kilichofanyika leo tarehe 20 Septemba, 2022 katika Ukumbi wa Spika Bungeni Jijini Dodoma.





Wajumbe wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Masuala ya Ukimwi, Udhibiti wa dawa za kulevya na Ugonjwa wa Kifua kikuu pamoja na Kamati ya Huduma na Maendeleo ya Jamii wafanya mazungumzo na kamati ya Afya na Huduma kwa Watoto kutoka Bunge la Zimbawe kikao kilichofanyika leo tarehe 20 Septemba, 2022 katika Ukumbi wa Spika Bungeni Jijini Dodoma.

Friday, September 16, 2022

TIMU YA BUNGE SPORTS CLUB YAKABIDHIWA VIFAA VYA MICHEZO NA BENKI YA NMB


Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB, Ndg. Ruth Zaipuna (kulia) amemkabidhi vifaa vya michezo Mwenyekiti wa timu ya Bunge Sports Club, Mhe. Tarimba Abbas (wapili kulia) tukio lililofanyika leo tarehe 16 Septemba, 2022 katika Ukumbi wa Msekwa Bungeni Jijini Dodoma. Wapili kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa timu ya Bunge Sports Club, Mhe. Esther Matiko na Afisa wa Bunge, Ndg. Rai Karinga

Makabidhiano hayo ni kuelekea katika bonanza kati ya timu ya Bunge Sports Club na Benki ya NMB linalotegemewa kufanyika kesho tarehe 17 Septemba, 2022 katika viwanja vya Chinangali Jijini Dodoma.


WAJUMBE KAMATI YA BUNGE YA MAMBO YA NJE, ULINZI NA USALAMA WAFANYA MAZUNGUMZO NA MABALOZI WA NCHI ZA UMOJA WA ULAYA BUNGENI JIJINI DODOMA



 

Makamu Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, Mhe. Vicent Mbogo akiongoza mazungumzo kati ya Wajumbe wa kamati hiyo (kushoto) na Mabalozi wa Nchi za Umoja wa Ulaya (kulia) wakiongozwa na Balozi wa Umoja huo, Mhe. Manfredo Fanti (kulia) walipowatembelea leo tarehe 16 Septemba, 2022 Bungeni Jijini Dodoma.


Thursday, September 15, 2022

SPIKA DKT. TULIA AFANYA MAZUNGUMZO NA MABALOZI WA NCHI ZA UMOJA WA ULAYA BUNGENI JIJINI DODOMA

Spika wa Bunge, Mhe. Dkt. Tulia Ackson akizungumza na Balozi wa Umoja wa Ulaya, Mhe. Manfredo Fanti pale ugeni kutoka Mabalozi wa Nchi za Umoja wa Ulaya walipomtembelea leo tarehe 15 Septemba, 2022 Bungeni Jijini Dodoma.



Spika wa Bunge, Mhe. Dkt. Tulia Ackson akizungumza na Mabalozi wa Nchi za Umoja wa Ulaya wakiongozwa na Balozi wa Umoja huo, Mhe. Manfredo Fanti (kulia kwake) walipomtembelea leo tarehe 15 Septemba, 2022 Bungeni Jijini Dodoma.


Spika wa Bunge, Mhe. Dkt. Tulia Ackson akionyesha zawadi ya vitabu alivyopewa na Balozi wa Umoja wa Ulaya, Mhe. Manfredo Fanti pale ugeni wa Mabalozi wa Nchi za Umoja wa Ulaya walipomtembelea leo tarehe 15 Septemba, 2022 Bungeni Jijini Dodoma.



Spika wa Bunge, Mhe. Dkt. Tulia Ackson akiwa katika picha ya pamoja na Mabalozi wa Nchi za Umoja wa Ulaya wakiongozwa na Balozi wa Umoja huo, Mhe. Manfredo Fanti (kulia kwake) walipomtembelea leo tarehe 15 Septemba, 2022 Bungeni Jijini Dodoma.

Wednesday, September 14, 2022

SPIKA DKT. TULIA AFANYA MAZUNGUMZO NA NAIBU SPIKA WA PILI WA BUNGE LA GHANA, KIONGOZI WA UPINZANI BUNGE LA UGANDA

Spika wa Bunge, Mhe. Dkt. Tulia Ackson akisalimiana na Naibu Spika wa Pili wa Bunge la Ghana, Mhe. Andrew Amoako pale Wageni kutoka Bunge hilo walipomtembelea leo tarehe 14 Septemba, 2022 Bungeni Jijini Dodoma.


Spika wa Bunge, Mhe. Dkt. Tulia Ackson akizungumza na Naibu Spika wa Pili wa Bunge la Ghana, Mhe. Andrew Amoako pale Wageni kutoka Bunge hilo walipomtembelea leo tarehe 14 Septemba, 2022 Bungeni Jijini Dodoma.


Spika wa Bunge, Mhe. Dkt. Tulia Ackson akizungumza na Wageni kutoka Bunge la Ghana wakiongozwa na Naibu Spika wa Pili wa Bunge, Mhe. Andrew Amoako (kulia kwake) walipomtembelea leo tarehe 14 Septemba, 2022 Bungeni Jijini Dodoma.


Spika wa Bunge, Mhe. Dkt. Tulia Ackson akimpatia zawadi yenye mfano wa jengo la Bunge Naibu Spika wa Pili wa Bunge la Ghana, Mhe. Andrew Amoako pale Wageni kutoka Bunge hilo walipomtembelea leo tarehe 14 Septemba, 2022 Bungeni Jijini Dodoma.


Spika wa Bunge, Mhe. Dkt. Tulia Ackson akizungumza na Kiongozi wa Upinzani kutoka Bunge la Uganda, Mhe. Mpuuga Mathias pale Waheshimiwa Wabunge kutoka Bunge hilo walipomtembelea leo tarehe 14 Septemba, 2022 Bungeni Jijini Dodoma.


Spika wa Bunge, Mhe. Dkt. Tulia Ackson akizungumza na Waheshimiwa Wabunge kutoka Bunge la Uganda wakiongozwa na Kiongozi wa Upinzani wa Bunge, Mhe. Mpuuga Mathias (kulia kwake) walipomtembelea leo tarehe 14 Septemba, 2022 Bungeni Jijini Dodoma.


Spika wa Bunge, Mhe. Dkt. Tulia Ackson akiwa katika picha ya pamoja na Kiongozi wa Upinzani kutoka Bunge la Uganda, Mhe. Mpuuga Mathias pale Waheshimiwa Wabunge kutoka Bunge hilo walipomtembelea leo tarehe 14 Septemba, 2022 Bungeni Jijini Dodoma.



Spika wa Bunge, Mhe. Dkt. Tulia Ackson (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Waheshimiwa Wabunge kutoka Bunge la Uganda wakiongozwa na Kiongozi wa Upinzani wa Bunge, Mhe. Mpuuga Mathias (kulia kwake) walipomtembelea leo tarehe 14 Septemba, 2022 Bungeni Jijini Dodoma.

Tuesday, September 13, 2022

SPIKA DKT. TULIA AMUAPISHA MHE. TAMIM HAJI ABASS


Mbunge Tamima Haji Abass akiapa kiapo cha uaminifu mbele ya Spika wa Bunge, Mhe. Dkt. Tulia Ackson wakati wa Mkutano wa Nane Kikao cha kwanza cha Bunge leo tarehe 13 Septemba, 2022 Bungeni Jijini Dodoma. Kushoto ni Katibu wa Bunge, Ndg. Nenelwa Mwihambi

Monday, September 12, 2022

SPIKA DKT. TULIA AONGOZA KIKAO CHA KAMATI YA UONGOZI JIJINI DODOMA






Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson akiongoza kikao cha kamati ya uongozi kilichopokea na kujadili Shughuli za Mkutano wa Nane wa Bunge pamoja na Mapendekezo ya Ratiba ya Mkutano huo leo tarehe 12 Septemba, 2022 katika Ukumbi wa Spika Bungeni Jijini Dodoma. Kushoto kwake ni Katibu wa Bunge, Ndg. Nenelwa Mwihambi na Naibu Spika wa Bunge, Mhe. Mussa Azzan Zungu




Naibu Spika wa Bunge, Mhe. Mussa Azzan Zungu akisoma maelezo ya Spika kwa niaba ya Spika Dkt. Tulia Ackson wakati wa kikao cha kamati ya uongozi kilichopokea na kujadili Shughuli za Mkutano wa Nane wa Bunge pamoja na Mapendekezo ya Ratiba ya Mkutano huo leo tarehe 12 Septemba, 2022 katika Ukumbi wa Spika Bungeni Jijini Dodoma.




Katibu wa Bunge, Ndg. Nenelwa Mwihambi akishiriki kikao cha kamati ya uongozi kilichopokea na kujadili Shughuli za Mkutano wa Nane wa Bunge pamoja na Mapendekezo ya Ratiba ya Mkutano huo leo tarehe 12 Septemba, 2022 katika Ukumbi wa Spika Bungeni Jijini Dodoma.



Wajumbe wa kamati ya uongozi wakiwa katika kikao cha kamati hiyo kilichopokea na kujadili Shughuli za Mkutano wa Nane wa Bunge pamoja na Mapendekezo ya Ratiba ya Mkutano huo leo tarehe 12 Septemba, 2022 katika Ukumbi wa Spika Bungeni Jijini Dodoma. Kuanzia kushoto ni Mhe. Joseph Mhagama, Mhe. Najma Giga na Mhe. David Kihenzile



Wajumbe wa kamati ya uongozi wakiwa katika kikao cha kamati hiyo kilichopokea na kujadili Shughuli za Mkutano wa Nane wa Bunge pamoja na Mapendekezo ya Ratiba ya Mkutano huo leo tarehe 12 Septemba, 2022 katika Ukumbi wa Spika Bungeni Jijini Dodoma.


 

Friday, September 9, 2022

SPIKA DKT. TULIA MGENI RASMI HAFLA YA UTOAJI WA ZAWADI KWA WASHINDI WA INSHA YA KUPINGA NDOA NA MIMBA ZA UTOTONI


Spika wa Bunge, Mhe. Dkt. Tulia Ackson, akisalimiana na Naibu Waziri Ofisi ya Rais, TAMISEMI (Afya), Mhe. Dkt. Festo Dugange wakati alipowasili katika hoteli ya St. Gasper Jijini Dodoma leo tarehe 9 Septemba, 2022 katika hafla ya utoaji wa zawadi kwa washindi wa Insha ya Kupinga Ndoa na Mimba za Utotoni. Wapili kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mhe. Rosemary Senyamule, Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii, Mhe. Stanslaus Nyongo (kulia) na Mwenyekiti wa Bodi wa Shirika la World Vision Tanzania, Dkt. Diana Mndeme




Spika wa Bunge, Mhe. Dkt. Tulia Ackson akizungumza jambo wakati wa hafla ya utoaji wa zawadi kwa washindi wa Insha ya Kupinga Ndoa na Mimba za Utotoni iliyofanyika leo tarehe 9 Septemba, 2022 katika Ukumbi wa Mikutano wa St. Gasper Jijini Dodoma.



Naibu Waziri Ofisi ya Rais, TAMISEMI (Afya), Mhe. Dkt. Festo Dugange akizungumza jambo wakati wa hafla ya utoaji wa zawadi kwa washindi wa Insha ya Kupinga Ndoa na Mimba za Utotoni iliyofanyika leo tarehe 9 Septemba, 2022 katika Ukumbi wa Mikutano wa St. Gasper Jijini Dodoma.



Wanafunzi Mbalimbali walioshiriki katika zoezi la uandishi wa insha wakiwa katika hafla ya utoaji wa zawadi kwa washindi wa Insha ya Kupinga Ndoa na Mimba za Utotoni iliyofanyika leo tarehe 9 Septemba, 2022 katika Ukumbi wa Mikutano wa St. Gasper Jijini Dodoma.

 

Spika wa Bunge, Mhe. Dkt. Tulia Ackson, akimkabidhi mfano wa hundi ya Shillingi Million 1 Mwanafunzi Genoveva Mwakihwaja aliyeibuka Mshindi wa kwanza katika hafla ya utoaji wa zawadi kwa washindi wa Insha ya Kupinga Ndoa na Mimba za Utotoni iliyofanyika leo tarehe 9 Septemba, 2022 katika Ukumbi wa Mikutano wa St. Gasper Jijini Dodoma. Kulia ni Naibu Waziri Ofisi ya Rais, TAMISEMI (Afya), Mhe. Dkt. Festo Dugange 



 Spika wa Bunge, Mhe. Dkt. Tulia Ackson (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi Wakuu kutoka Shirika la World Vision Tanzania na Wadau wa Maendeleo wakati wa hafla ya utoaji wa zawadi kwa washindi wa Insha ya Kupinga Ndoa na Mimba za Utotoni iliyofanyika leo tarehe 9 Septemba, 2022 katika Ukumbi wa Mikutano wa St. Gasper Jijini Dodoma. Kulia kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mhe. Rosemary Senyamule, Naibu Waziri Ofisi ya Rais, TAMISEMI (Afya), Mhe. Dkt. Festo Dugange (kushoto kwake), Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii, Mhe. Stanslaus Nyongo (kulia) na Mwenyekiti wa Bodi wa Shirika la World Vision Tanzania, Dkt. Diana Mndeme (wapili kulia)

Thursday, September 8, 2022

WAJUMBE KAMATI YA PAC WAPOKEA MAELEZO KUHUSU MAJUKUMU YA OFISI YA MKAGUZI MKUU WA NDANI WA SERIKALI, WACHAMBUA TAARIFA YA HESABU ZILIZOKAGULIWA NA EWURA


Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), Mhe. Naghenjwa Kaboyoka akiongoza kikao cha kamati hiyo kilichokaa na Kupokea maelezo kuhusu majukumu ya ofisi ya Mkaguzi Mkuu wa Ndani wa Serikali katika udhibiti wa matumizi ya fedha za Umma, Kupitia na kuchambua Taarifa ya Hesabu zilizokaguliwa za Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji (EWURA) kilichofanyika leo tarehe 8 Septemba, 2022 katika ofisi za Bunge Jijini Dodoma. Kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa kamati hiyo, Mhe. Japhet Hasunga

Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), Mhe. Naghenjwa Kaboyoka (katikati) akiongoza kikao cha kamati hiyo kilichokaa na kupokea maelezo kuhusu majukumu ya ofisi ya Mkaguzi Mkuu wa Ndani wa Serikali katika udhibiti wa matumizi ya fedha za Umma, Kupitia na kuchambua Taarifa ya Hesabu zilizokaguliwa za Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji (EWURA) kilichofanyika leo tarehe 8 Septemba, 2022 katika ofisi za Bunge Jijini Dodoma.

Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji (EWURA), Prof. Mark Mwandosya akijitambulisha mbele ya kamati ya kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) wakati wa kikao cha kamati hiyo kilichokaa na kupokea maelezo kuhusu majukumu ya ofisi ya Mkaguzi Mkuu wa Ndani wa Serikali katika udhibiti wa matumizi ya fedha za Umma, Kupitia na kuchambua Taarifa ya Hesabu zilizokaguliwa za Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji (EWURA) leo tarehe 8 Septemba, 2022 katika ofisi za Bunge Jijini Dodoma. Kushoto ni Mkurugenzi wa Petroli EWURA, Ndg. Gerald Maganga na Mkurugenzi wa Fedha, Utawala na Rasiliamali Watu EWURA, Ndg. Stanley Mahembe.



Mjumbe wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), Mhe. Isack Kamwelwe akichangia jambo wakati wa kikao cha kamati hiyo kilichokaa na kupokea maelezo kuhusu majukumu ya ofisi ya Mkaguzi Mkuu wa Ndani wa Serikali katika udhibiti wa matumizi ya fedha za Umma, Kupitia na kuchambua Taarifa ya Hesabu zilizokaguliwa za Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji (EWURA) leo tarehe 8 Septemba, 2022 katika ofisi za Bunge Jijini Dodoma.



Wajumbe wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) wakiwa katika kikao cha kamati hiyo kilichokaa na kupokea maelezo kuhusu majukumu ya ofisi ya Mkaguzi Mkuu wa Ndani wa Serikali katika udhibiti wa matumizi ya fedha za Umma, Kupitia na kuchambua Taarifa ya Hesabu zilizokaguliwa za Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji (EWURA) leo tarehe 8 Septemba, 2022 katika ofisi za Bunge Jijini Dodoma.