WELCOME TO TANZANIA NATIONAL ASSEMBLY OFFICIAL BLOG: CONTACT US: P.O.BOX 941 DODOMA, TANZANIA, WEBSITE: parliament.go.tz , FIND US ON FACEBOOK >>> www.facebook.com/bungetz1, FOLLOW US ON TWITTER >>> @bunge_tz.>>>KARIBUNI

Thursday, September 21, 2017


Mbunge wa Kigoma Mjini Mheshimiwa Zitto Kabwe akiingia  kuhojiwa na Kamati ya Bunge ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge leo Mjini Dodoma. Kamati hiyo chini ya Mwenyekiti wake Kapteni Mstaafu Mheshimiwa George Mkuchika imemuhoji mbunge huyo kufuatia kutoa matamshi yanayolidharirisha Bunge kwenye mitandao ya kijamii.
   
Mweyekiti wa Kamati ya Bunge ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge Mheshimiwa Kapteni Mstaafu George Mkuchika akiongoza Mahojiano ya Kamati hiyo leo Bungeni Mjini Dodoma ambapo Mheshimiwa Zitto Kabwe aliitwa kuhojiwa kufuatia kutoa matamshi ya kudharirisha Mamlaka ya Bunge kupitia kwenye mitandao ya kijamii. 

  
Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge wakiwa katika kikao cha Kamati hiyo kilichokaa kumhoji Mbunge wa Kigoma Mjini Mheshimiwa Zitto Kabwe kufuatia kutoa matamshi yanayolidharirisha Bunge kupitia mitandao ya Kijamii.

Thursday, September 14, 2017

UFAFANUZI KUHUSU SAFARI YA MHESHIMIWA LISSU KWENDA MJINI NAIROBI NCHINI KENYA ANAKOPATIWA MATIBABU

Spika wa Bunge Mheshimiwa Job Ndugai ambaye pia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Mradi wa Kulijengea uwezo Bunge LSP akitoa neno la Shukran kwa Wafadhili wa Mradi wa Awamu ya Pili wa Kulijengea uwezo Bunge LSP II unaofadhiliwa na Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa UNDP katika hafla ya uzinduzi iliyofanyika leo Bungeni Mjini Dodoma.
Mgeni rasmi katika Hafla ya uzinduzi wa Mradi wa Awamu ya Pili wa Kulijengea uwezo Bunge LSP II Waziri Mkuu Mheshimiwa Majaliwa Kassim Majaliwa akitoa neno la Shukran kwa Wafadhili unaofadhiliwa na Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa UNDP katika hafla ya uzinduzi iliyofanyika leo Bungeni Mjini Dodoma. 


Katibu wa Bunge Dkt. Thomas Kashililah akitoa tathmini ya Utekelezaji wa Mradi wa  Kulijengea uwezo Bunge LSP I  katika hafla ya uzinduzi wa Mradi huo kwa Awamu ya Pili LPS II 2017-2021 iliyofanyika leo Bungeni Mjini Dodoma.

Tuesday, September 12, 2017

SPIKA WA BUNGE AHUDHURIA HAFLA YA UZINDUZI WA MPANGO WA WIZARA YA FEDHASpika wa Bunge Mheshimiwa Job Yustino Ndugai akitoa salamu kwa wajumbe waalikwa katika hafla ya ufunguzi  wa  maboresho wa sekta ya fedha kwa taasisi za umma (PFMRP) awamu ya tano 2017/18 mpaka 2021/22 katika hafla iliyofanyika leo mjini Dodoma

Spika wa Bunge Mheshimiwa Job Yustino Ndugai akipokea kitabu cha mpango mkakati wa Wizara ya Fedha na Mipango wa miaka mitano wa maboresho ya  sekta ya fedha kwa taasisi za umma (PFMRP) awamu ya tano 2017/18 mpaka 2021/22 katika hafla iliyofanyika leo mjini Dodoma.

.

Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar amtembelea Spika wa Bunge Mjini Dodoma

Spika wa Bunge Mheshimiwa Job Ndugai akifurahi jambo wakati akimsikiliza Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mheshimiwa Zuberi Ali Maulid alipomtembelea ofisini kwake, Bungeni  Mjini Dodoma.

Spika wa Bunge Mheshimiwa Job Ndugai (wa kwanza kulia) akifurahi katika picha ya pamoja na Spika wa Baraza la Wawakilishi  Zanzibar Mheshimiwa Zuberi Ali Maulid alipomtembelea ofisini kwake, Bungeni  Mjini Dodoma na Mheshimiwa Jenista Mhagama Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira, na Watu wenye Ulemavu 
Spika wa Bunge Mheshimiwa Job Ndugai (wa kwanza kulia) akifurahi katika picha ya pamoja na Spika wa Baraza la Wawakilishi  Zanzibar Mheshimiwa Zuberi Ali Maulid alipomtembelea ofisini kwake, Bungeni  Mjini Dodoma na Mheshimiwa Jenista Mhagama Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira, na Watu wenye Ulemavu Saturday, September 9, 2017

PROFESA MAKAME MBARAWA AWASILISHA MAELEZO YA MUSWADA WA SHERIA YA RELI WA MWAKA 2017 KWA KAMATI YA BUNGE YA MIUNDOMBINU

Kaimu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Miundombinu, Mheshimiwa Rashid Chuachua akizungumza katika kikao cha Kamati hiyo kilichokutana kwa ajili ya kusikiliza maoni ya wadau kuhusu Muswada wa Sheria ya Reli wa mwaka 2017, Kushoto ni Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa akiwasilisha maelezo ya Muswada wa Sheria ya Reli wa mwaka 2017 kwa Kamati ya Bunge ya Miundombinu, kulia ni Kaimu Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mheshimiwa Rashid Chuachua.
Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Miundombinu wakimsikiliza Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa akiwasilisha maelezo kuhusu Muswada waSheria ya Reli wa mwaka 2017 ambao umeshasomwa Bungeni kwa mara ya kwanza.

Thursday, September 7, 2017

RAIS DKT MAGUFULI APOKEA TAARIFA MBILI ZA KAMATI ZA BUNGE ZA KIUCHUNGUZI WA BIASHARA YA MADINI YA TANZANITE NA ALMASI, IKULU JIJINI DAR ES SALAAM

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt John Pombe Magufuli akipokea  toka kwa Waziri Mkuu Mheshimiwa Kassim Majaliwa  ripoti  mbili za Kamati Maalum  za Bunge zilizofanya uchunguzi wa Biashara ya Madini ya Almasi na Tanzanite hapa nchini, Ikulu Jijini Dar es Salaam.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa  Dkt John Pombe Magufuli akizungumza mara baada ya kupokea ripoti  mbili za Kamati Maalum  za Bunge zilizofanya uchunguzi wa Biashara ya Madini ya Almasi na Tanzanite Ikulu Jijini Dar es Salaam.
  Waziri Mkuu Mheshimiwa Kassim Majaliwa  akizungumza wakati wa kukabidhi ripoti za  kiuchunguzi  za Biashara ya Madini ya Tanzanite na Almasi kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli Ikulu Jijini Dar es Salaam.
  Spika wa Bunge Mheshimiwa Job Ndugai akizungumza wakati wa kukabidhi ripoti za  kiuchunguzi  za Biashara ya Madini ya Tanzanite na Almasi kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli Ikulu Jijini Dar es Salaam
       Mwenyekiti wa Kamati  Maalum ya Bunge iliyofanya uchunguzi wa Biashara ya Madini ya Tanzanite hapa nchini Mheshimiwa  Dotto Biteko akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi ripoti hiyo kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli Ikulu Jijini Dar es Salaam.
      Mwenyekiti wa Kamati  Maalum ya Bunge iliyofanya uchunguzi wa Biashara ya Madini ya Almasi hapa nchini Mheshimiwa Mussa Azzan Zungu akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi ripoti hiyo kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli Ikulu Jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Mheshimiwa John Pombe Magufuli (katikati), katika picha ya pamoja na  Waziri Mkuu Mheshimiwa  Kassim Majaliwa (wa pili waliokaa kushoto) na Spika wa Bunge Job Ndugai (wa pili waliokaa kulia),  Mweyekiti wa Kamati  Maalum ya Bunge iliyofanya uchunguzi wa Biashara ya Madini ya Almasi hapa nchini Mhe Mussa Azzan Zungu  (wa kwanza kulia waliokaa) na Mweyekiti wa Kamati  Maalum ya Bunge iliyofanya uchunguzi wa Biashara ya Madini ya Tanzanite hapa nchini Mhe Dotto Biteko (wa kwanza kushoto waliokaa) na Wajumbe wa Kamati zote mbili (waliosimama) mara baada ya kuzipokea ripoti hizo Ikulu Jijini Dar es Salaam.