WELCOME TO TANZANIA NATIONAL ASSEMBLY OFFICIAL BLOG: CONTACT US: P.O.BOX 941 DODOMA, TANZANIA, WEBSITE: parliament.go.tz , FIND US ON FACEBOOK >>> www.facebook.com/bungetz1, FOLLOW US ON TWITTER >>> @bunge_tz.>>>KARIBUNI

Tuesday, December 11, 2018

SPIKA WA BUNGE AKUTANA NA JAJI MKUU WILAYANI KONGWA

Spika wa Bunge Mheshimiwa Job Ndugai ambae pia ni mbunge wa Jimbo la Kongwa akizungumza jambo katika Kikao kilichoendeshwa na Jaji Mkuu wa Tanzania Mheshimiwa Prof. Ibrahim Hamis Juma kwa Watendaji wa Mahakama ya Wilaya ya Kongwa.

Spika wa Bunge Mheshimiwa Job Ndugai pamoja na Jaji Mkuu wa Tanzania Mheshimiwa Prof. Ibrahim Hamis Juma wakiwa katika picha ya pamoja na Watendaji mbalimbali wa Wilaya ya Kongwa.

Spika wa Bunge Mheshimiwa Job Ndugai (kulia) akijadiliana jambo na Jaji Mkuu wa Tanzania Mheshimiwa Prof. Ibrahim Hamis Juma mara baada ya Ziara ya Jaji Mkuu katika Mahakama ya Wilaya ya Kongwa.

SPIKA WA BUNGE ATEMBELEWA NA WAGENI KUTOKA NAMIBIA

Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai akipokea zawadi kutoka kwa mgeni wake kutoka Nchini Namibia Ndugu Desmond Amunyela aliyemtembelea Ofisini kwake Jijini Dodoma.mgeni huyo alieleza kusudio la Namibia la kujenga Kituo cha Kimataifa Wilayani Kongwa  cha Kumbukumbu ya Kupigania uhuru wa Nchi za Kusini mwa Afrika.

Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai akizungumza na mgeni wake kutoka Nchini Namibia Ndugu Desmond Amunyela aliyemtembelea Ofisini kwake Jijini Dodoma.Mgeni huyo alieleza kusudio la Namibia la kujenga Kituo cha Kimataifa Wilayani Kongwa  cha Kumbukumbu ya Kupigania uhuru wa Nchi za Kusini mwa Afrika.

Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai akionyeshwa mchoro wa Kituo cha Kimataifa kitakachojengwa Wilayani Kongwa  cha Kumbukumbu ya Kupigania uhuru wa Nchi za Kusini mwa Afrika kutoka kwa Ndugu Desmond Amunyela aliyemtembelea Ofisini kwake Jijini Dodoma aliyembatana na Ndugu Iyaloo ya Nangolo wote wakitokea Nchini Namibia.

Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai akiwaonyesha Ukumbi wa Bunge la Tanzania wakeni wake kutoka Nchini Namibia Ndugu Desmond Amunyela na Ndugu  Iyaloo ya Nangolo  mara baada ya kumtembelea Ofisini kwake Jijini Dodoma.wageni hao walieleza kusudio la Namibia la kujenga Kituo cha Kimataifa Wilayani Kongwa  cha Kumbukumbu ya Kupigania uhuru wa Nchi za Kusini mwa Afrika.