WELCOME TO TANZANIA NATIONAL ASSEMBLY OFFICIAL BLOG: CONTACT US: P.O.BOX 941 DODOMA, TANZANIA, WEBSITE: parliament.go.tz , FIND US ON FACEBOOK >>> www.facebook.com/bungetz1, FOLLOW US ON TWITTER >>> @bunge_tz.>>>KARIBUNI

Monday, January 31, 2022

TISA KUGOMBEA USPIKA

Katibu wa Bunge, Ndg. Nenelwa Mwihambi, ndc amesema hadi kufikia leo saa Kumi Jioni Majina ya jumla ya Wagombea Tisa (9) yalikuwa yamewasilishwa na kukidhi matakwa ya kisheria kwa ajili ya uchaguzi wa Spika unaotarajiwa kufanyika kesho tarehe 1 Februari, 2022.

Akizungumza na Waandishi wa Habari Jijini Dodoma, Katibu wa Bunge amesema kuwa miongoni mwa Wagombea hao nane sio Wabunge na mmoja ni Mbunge.

Aliwataja magombea hao kuwa ni Abdullah Mohammed Said (NRA), Mhandisi Aivan Jackson Maganza (TLP), David Daud Mwaijojele (CCK), Georges Gabriel Bussungu (ADA -TEA), Kunje Ngombale Mwiru (SAU), Maimuna Said Kassim (ADC), Ndonge Said Ndonge (AAFP), Saidoun Abrahamani Khatib (DP) na Mheshimiwa Dkt. Tulia Ackson (Mb).