WELCOME TO TANZANIA NATIONAL ASSEMBLY OFFICIAL BLOG: CONTACT US: P.O.BOX 941 DODOMA, TANZANIA, WEBSITE: parliament.go.tz , FIND US ON FACEBOOK >>> www.facebook.com/bungetz1, FOLLOW US ON TWITTER >>> @bunge_tz.>>>KARIBUNI

Saturday, December 18, 2021

TIMU ZA BUNGE LA TANZANIA ZANGARA MASHINDANO YA MABUNGE YA AFRIKA MASHARIKI, ZAONDOKA NA VIKOMBE NANE

 

Wachezaji wakishangilia baada ya kubeba vikombe
Naibu Spika na Timu ya Netibali wakichukua kombe lao 
Wachezaji wa Mpira wa Kikapu wakibeba Kombe lao
Wachezaji wa Mpira wa Wavu wakibeba Kombe lao
Mhe. Simai akivishwa medali baada ya kuibuka mshindi wa pili mchezo wa kutembea kwa kasi
Naibu Spika akifurahia medali yake baada ya kuibuka mshindi wa pili mchezo wa kutembea kwa kasi kwa upande wa Wanawake
Mkata upepo namba moja, Mhe. Anatropia Theonest akichukua medali kama zote 
                                           
                                                ------------

Mashindano ya 11 ya Mabunge Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki yaliyokuwa yakifanyika Jijini Arusha  yamemalizika huku Timu za Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania zikishinda vikombe nane.Timu zilizoibuka washindi wa jumla na kuwa Mabigwa ni pamoja na;

·       Timu ya Mpira wa Miguu

·       Timu ya Mpira wa Pete (Netball)

·       Timu ya Mpira wa Wavu (Volleyball) Wanaume

·       Timu ya Mpira wa Wavu (Volleyball) Wanawake

·       Timu ya Mpira wa Kikapu ( Basketball) Wanaume

·       Timu ya Mpira wa Kikapu ( Basketball) Wawake

·       Timu ya Kuvuta Kamba Wanaume

·       Timu ya Riadha Wanawake

Aidha katika mashindano mingine Timu za Bunge la Tanzania zimeibuka Washindi wa Pili katika michezo ifuatayo;

·       Mchezo wa Kutembea kwa kasi Wanawake-Naibu Spika, Dkt. Tulia Ackson aliibuka Mshindi wa Pili.

·       Mchezo wa Kutembea kwa kasi Wanaume-Mbunge wa Nungwi, Mhe. Simai Hassan Sadik aliibuka Mshindi wa Pili

·       Timu ya Kuvuta Kamba Wanawake waliibuka Washindi wa Pili

·       Mchezo wa Darts Timu ya Wanaume wallibuka Washindi wa Pili.

Michezo ya Mabunge Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki ilihusisha Timu kutoka Mabunge 6 ya Tanzania, Kenya, Burundi, Zanzibar, Sudan Kusini, Uganda na Bunge la Afrika Mashariki ambao walikuwa wenyeji. 

Thursday, December 16, 2021

TIMU YA MPIRA WA KIKAPU (KE) TANZANIA YAPIGA MAGOLI 52:30 TIMU YA BARAZA LA WAKILISHI


 

TIMU YA MPIRA WA MIGUU YA BUNGE LA TANZANIA YAENDELEA KUTOA DOZI MICHEZO AFRIKA MASHARIKI, YAICHAKAZA BURUNDI GOLI 5-1

Mshambuliaji wa Timu ya Mpira wa Miguu ya Bunge la Tanzania, Simai Hassan Sadiki (kulia) akimtoka Beki wa Timu ya Burundi wakati wa mechi ya Mashidano ya Michezo ya Mabunge ya Jumuiya ya Afrika Mshariki inayoendelea Jijini Arusha. Timu ya Tanzania ilishinda kwa goli 5-1.

 Nahodha  wa Timu ya Mpira wa Miguu ya Bunge la Tanzania, Cosato Chumi  (kushoto) akidhibiti mpira mbele ya  Mabeki wa Timu ya Burundi wakati wa mechi ya Mashidano ya Michezo ya Mabunge ya Jumuiya ya Afrika Mshariki inayoendelea Jijini Arusha. Timu ya Tanzania ilishinda kwa goli 5-1.

Kiungo  wa Timu ya Mpira wa Miguu ya Bunge la Tanzania, Ramadhan Suleiman  Ramadhan  (kulia) apiga pasi mbele ya Kiungo wa wa Timu ya Burundi wakati wa mechi ya Mashidano ya Michezo ya Mabunge ya Jumuiya ya Afrika Mshariki inayoendelea Jijini Arusha. Timu ya Tanzania ilishinda kwa goli 5-1.

Mshambuliaji wa Timu ya Mpira wa Miguu ya Bunge la Tanzania, Ridhiwan Kikwete (katikati) akiwatoka Mabeki wa Timu ya Burundi wakati wa mechi ya Mashidano ya Michezo ya Mabunge ya Jumuiya ya Afrika Mshariki inayoendelea Jijini Arusha. Timu ya Tanzania ilishinda kwa goli 5-1.

Nahodha Msaidizi Timu ya Mpira wa Miguu ya Bunge la Tanzania, Athony Mavunde  akiwatoka viungo wa wa Timu ya Burundi wakati wa mechi ya Mashidano ya Michezo ya Mabunge ya Jumuiya ya Afrika Mshariki inayoendelea Jijini Arusha. Timu ya Tanzania ilishinda kwa goli 5-1.

 

Monday, December 13, 2021

TIMU YA KUVUTA KAMBA WANAUME BUNGE LA TANZANIA YAONGOZA

 


Timu ya Bunge la Tanzania Wanaume ya kuvuta Kamba ikishangilia baada ya kutangazwa kuwa Mabingwa katika Michezo ya Mabunge ya Jumuiya ya Afrika Mashariki inayoendelea Jijini Arusha.


Timu ya Bunge la Tanzania Wanaume ya kuvuta Kamba ikishangilia baada ya kutangazwa kuwa Mabingwa katika Michezo ya Mabunge ya Jumuiya ya Afrika Mashariki inayoendelea Jijini Arusha.

Timu ya Bunge la Tanzania Wanaume ya kuvuta Kamba ikishangilia baada ya kutangazwa kuwa Mabingwa katika Michezo ya Mabunge ya Jumuiya ya Afrika Mashariki inayoendelea Jijini Arusha.Timu ya Bunge la Tanzania Wanaume ya kuvuta Kamba ikishangilia baada ya kutangazwa kuwa Mabingwa katika Michezo ya Mabunge ya Jumuiya ya Afrika Mashariki inayoendelea Jijini Arusha.

Thursday, December 9, 2021

PICHA:TIMU YA BUNGE LA TANZANIA YA WANAWAKE YA MPIRA WA WAVU YAITANDIKA TIMU YA BUNGE LA KENYA SETI 3-0

Timu ya Bunge la Tanzania ya Wanawake ya Mpira wa Wavu (yenye jezi ya bluu) imeitandika Timu ya Bunge la Kenya kwa Seti 3-0 katika mechi ya mashindano ya Michezo ya Mabunge ya Jumuiya ya Afrika Mashariki inayoendelea Jijini Arusha.
Timu ya Bunge la Tanzania ya Wanawake ya Mpira wa Wavu (yenye jezi ya bluu) imeitandika Timu ya Bunge la Kenya kwa Seti 3-0 katika mechi ya mashindano ya Michezo ya Mabunge ya Jumuiya ya Afrika Mashariki inayoendelea Jijini Arusha.
Timu ya Bunge la Tanzania ya Wanawake ya Mpira wa Wavu (yenye jezi ya bluu) imeitandika Timu ya Bunge la Kenya kwa Seti 3-0 katika mechi ya mashindano ya Michezo ya Mabunge ya Jumuiya ya Afrika Mashariki inayoendelea Jijini Arusha.


 Timu ya Bunge la Tanzania ya Wanawake ya Mpira wa Wavu (yenye jezi ya bluu) imeitandika Timu ya Bunge la Kenya kwa Seti 3-0 katika mechi ya mashindano ya Michezo ya Mabunge ya Jumuiya ya Afrika Mashariki inayoendelea Jijini Arusha.

Tuesday, December 7, 2021

TIMU YA BUNGE LA TANZANIA YAIBUKA KIDEDEA MCHEZO WA MPIRA WA PETE DHIDI YA TIMU YA BARAZA LA WAWAKILISHI ZANZIBAR

 

Mchezaji wa Timu ya Bunge ya Mpira wa Pete, Mheshimiwa Esther Matiko akidaka mpira wakati Timu ya Bunge ilipocheza na Timu ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar katika Uwanja wa Kumbukumbu ya Shekhe Amri Abeid kwenye michuano ya michezo ya Mabunge ya Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki inayoendelea Jijini Arusha.Timu ya Bunge iliibuka kidedea kwa Magoli 44-32
Mchezaji wa Timu ya Bunge ya Mpira wa Pete, Mheshimiwa Amina Mabrouk akidaka mpira wakati Timu ya Bunge ilipocheza na Timu ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar katika Uwanja wa Kumbukumbu ya Shekhe Amri Abeid kwenye michuano ya michezo ya Mabunge ya Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki inayoendelea Jijini Arusha.Timu ya Bunge iliibuka kidedea kwa Magoli 44-32
Wachezaji wa Timu ya Bunge ya Mpira wa Pete (wenye nyeupe) wakichuana vikali na Timu ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar katika Uwanja wa Kumbukumbu ya Shekhe Amri Abeid kwenye michuano ya michezo ya Mabunge ya Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki inayoendelea Jijini Arusha.Timu ya Bunge iliibuka kidedea kwa Magoli 44-32
Wachezaji wa Timu ya Bunge ya Mpira wa Pete (wenye nyeupe) wakiwa katika picha ya pamoja na Timu ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar  baada ya kumaliza kucheza katika Uwanja wa Kumbukumbu ya Shekhe Amri Abeid kwenye michuano ya michezo ya Mabunge ya Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki inayoendelea Jijini Arusha.Timu ya Bunge iliibuka kidedea kwa Magoli 44-32