WELCOME TO TANZANIA NATIONAL ASSEMBLY OFFICIAL BLOG: CONTACT US: P.O.BOX 941 DODOMA, TANZANIA, WEBSITE: parliament.go.tz , FIND US ON FACEBOOK >>> www.facebook.com/bungetz1, FOLLOW US ON TWITTER >>> @bunge_tz.>>>KARIBUNI

Friday, October 8, 2021

MAAFISA WA OFISI YA BUNGE WAKITOA ELIMU KUHUSU BUNGE KATIKA SHULE ZA SEKONDARI KIGWE NA IBIHWA ZILIZOPO WILAYA YA BAHI MKOA WA DODOMA


BARAZA LA WAFANYAKAZI LA OFISI YA BUNGE LIMEFANYA KIKAO KATIKA UKUMBI WA MSEKWA BUNGENI JIJINI DODOMA

Katibu wa Bunge ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi la Ofisi ya Bunge, Bi. Nenelwa Mwihambi akiongoza kikao cha Baraza kilichofanyika katika Ukumbi wa Msekwa, Bungeni Jijini Dodoma

Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Ofisi ya Bunge wakifuatilia uwasilishwaji wa mada katika kikao cha Baraza kilichofanyika Ukumbi wa Msekwa Bungeni Jijini Dodoma.Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Ofisi ya Bunge wakifuatilia uwasilishwaji wa mada katika kikao cha Baraza kilichofanyika Ukumbi wa Msekwa Bungeni Jijini Dodoma

Tuesday, October 5, 2021

KAMATI YA BUNGE YA MASUALA YA UKIMWI YAENDELEA NA KIKAO BUNGENI DODOMA

Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Masuala ya UKIMWI wakiwa katika kikao cha Kamati Bungeni Jijini Dodoma wakijadii Taarifa ya Ofisi ya Waziri Mkuu kuhusu changamoto za ukatili wa kijinsia, usawa wa kijinsia, mila potofu na unyanyasaji wa kijinsia katika mwitikio wa mapambano ya VVU/UKIMWI Nchini Tanzania
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu), Mheshimiwa Jenista Mhagama akizungumza katika kikao cha Kamati ya Bunge ya Masuala ya UKIMWI kilichofanyika Bungeni Jijini Dodoma. Kikao hicho kilijadili uhusu changamoto za ukatili wa kijinsia, usawa wa kijinsia, mila potofu na unyanyasaji wa kijinsia katika mwitikio  wa mapambano ya VVU/UKIMWI Nchini Tanzania

Mwenyekiti wa Kamati ya Masuala ya UKIMWI, Mheshimiwa Fatma Toufiq akizungumza katika kikao cha Kamati hiyokilichofanyika Bungeni Jijini Dodoma. Kikao hicho kilijadili uhusu changamoto za ukatili wa kijinsia, usawa wa kijinsia, mila potofu na unyanyasaji wa kijinsia katika mwitikio  wa mapambano ya VVU/UKIMWI Nchini Tanzania