WELCOME TO TANZANIA NATIONAL ASSEMBLY OFFICIAL BLOG: CONTACT US: P.O.BOX 941 DODOMA, TANZANIA, WEBSITE: parliament.go.tz , FIND US ON FACEBOOK >>> www.facebook.com/bungetz1, FOLLOW US ON TWITTER >>> @bunge_tz.>>>KARIBUNI

Monday, April 15, 2019

TAASISI MBALIMBALI ZA ELIMU ZAENDELEA KUFANYA ZIARA ZA MAFUNZO BUNGENI

Wanafunzi na Walimu wa Shule ya Msingi Feza ya Jijini Dar es Salaam wakiwa katika Jukwaa la Wageni Bungeni wakifuatilia mijadala ya Bunge hii leo Jijini Dodoma ikiwa ni sehemu ya Ziara yao ya Mafunzo Bungeni. 

Wanafunzi wa Shule ya Msingi Feza ya Jijini Dar es Salaam pamoja na Shule ya Sekondari Mtera Dam ya Dodoma wakiwa katika Ukumbi wa Msekwa wakipata Elimu kwa Umma kutoka kwa Maafisa wa Bunge ikiwa ni sehemu ya Ziara yao ya Mafunzo Bungeni. 

Wanafunzi na Walimu  wa Shule ya Msingi Feza ya Jijini Dar es Salaam pamoja na Shule ya Sekondari Mtera Dam ya Dodoma wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kukamilisha Ziara yao ya Mafunzo Bungeni Jijini Dodoma hii leo. 

Wednesday, April 10, 2019

NAIBU SPIKA AKUTANA NA WABUNGE WA UGANDA BUNGENI JIJINI DODOMA

Naibu Spika wa Bunge Mheshimiwa Dkt. Tulia Ackson akizungumza jambo na Mkuu wa Msafara wa Wabunge na Watumishi wa Bunge la Uganda na Mnadhimu Mkuu wa Upinzani wa Bunge hilo Mhe. Ssemujju Ibrahim Ofisini kwake Jijini Dodoma hii leo.

Naibu Spika wa Bunge Mheshimiwa Dkt. Tulia Ackson akizungumza jambo na Ujumbe wa Wabunge na Watumishi wa Bunge la Uganda waliopo ziarani hapa nchini Ofisini kwake Jijini Dodoma hii leo.  

Naibu Spika wa Bunge Mheshimiwa Dkt. Tulia Ackson akiwa katika picha ya pamoja na Ujumbe wa Wabunge na Watumishi wa Bunge la Uganda waliomtembelea Ofisini kwake Jijini Dodoma hii leo.

Friday, April 5, 2019

KATIBU WA BUNGE ATEMBELEWA NA NAIBU SPIKA WA BUNGE LA CAMEROON JIJINI DODOMA

Katibu wa Bunge ambaye pia ni Katibu wa Chama cha Mabunge ya Jumuiya ya Madola Kanda ya Afrika Ndg. Stephen Kagaigai akizungumza jambo na Naibu Spika wa Bunge la Cameroon na Mwenyekiti wa Kamati ya Utendaji ya Nchi za Jumuiya ya Madola Kimataifa Mhe. Emilia Monjowa Lifaka alipomtembelea Ofisini kwake Jijini Dodoma hii leo.

Katibu wa Bunge la ambaye pia ni Katibu wa Chama cha Mabunge ya Jumuiya ya Madola Kanda ya Afrika Ndg. Stephen Kagaigai akimuelezea jambo Naibu Spika wa Bunge la Cameroon na Mwenyekiti wa Kamati ya Utendaji ya Nchi za Jumuiya ya Madola Kimataifa Mhe. Emilia Monjowa Lifaka alipomtembelea Ofisini kwake Jijini Dodoma hii leo. Kushoto ni Mjumbe wa Kamati ya UtendajI ya Jumuiya hiyo Mhe. Maria Kangoye. 

Naibu Spika wa Bunge la Cameroon na Mwenyekiti wa Kamati ya Utendaji ya Nchi za Jumuiya ya Madola Kimataifa Mhe. Emilia Monjowa Lifaka akimuelezea jambo Katibu wa Bunge ambaye pia ni Katibu wa Chama cha Mabunge ya Jumuiya ya Madola Kanda ya Afrika Ndg. Stephen Kagaigai alipomtembelea Ofisini kwake Jijini Dodoma hii leo. 

Katibu wa Bunge ambaye pia ni Katibu wa Chama cha Mabunge ya Jumuiya ya Madola Kanda ya Afrika Ndg. Stephen Kagaigai pamoja na Naibu Spika wa Bunge la Cameroon na Mwenyekiti wa Kamati ya Utendaji ya Nchi za Jumuiya ya Madola Kimataifa Mhe. Emilia Monjowa Lifaka wakiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe wa Kamati ya Utendaji ya Jumuiya hiyo walipomtembelea Ofisini kwake Jijini Dodoma hii leo. Kulia ni Mhe. Jitu Soni na kushoto ni Mhe. Maria Kangoye

SPIKA WA BUNGE LA BURUNDI AKUTANA NA KAMATI YA MAMBO YA NJE, ULINZI NA USALAMA

Rais wa Seneti ya Burundi, Mhe. Reverin Ndikuriyo akizungumza na wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama wakati yeye na ujumbe wake walipotembelea Bunge la Tanzania na kukutana na kamati hiyo, pembeni yake ni Mwenyekiti wa Kamati, Mhe. Mussa Zungu.

Rais wa Seneti ya Burundi, Mhe. Reverin Ndikuriyo akizungumza na wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama wakati yeye na ujumbe wake walipotembelea Bunge la Tanzania na kukutana na kamati hiyo, pembeni yake ni Mwenyekiti wa Kamati, Mhe. Mussa Zungu.

Rais wa Seneti ya Burundi, Mhe. Reverin Ndikuriyo akiagana na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, Mhe. Mussa Zungu wakati Rais huyo pamoja na ujumbe wake walipotembelea Bunge la Tanzania na kukutana na kamati hiyo, pembeni yake ni Mwenyekiti wa Kamati, Mhe. Mussa Zungu.
 
Rais wa Seneti ya Burundi, Mhe. Reverin Ndikuriyo akiagana na Mbunge wa Bunge, Mhe. Charles Tizeba wakati Rais huyo pamoja na ujumbe wake walipotembelea Bunge la Tanzania na kukutana na kamati Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama.

Kamati ikiendelea na kikao

Wednesday, April 3, 2019

SPIKA NDUGAI AKUTANA NA VIONGOZI WA MAJUKWAA YA HABARI

Spika wa Bunge Mheshimiwa Job Ndugai akiongea jambo na Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahahriri Tanzania Ndg. Deodatus Balile alipomtembelea Ofisini kwake Jijini Dodoma hii leo. 


Spika wa Bunge Mheshimiwa Job Ndugai akiongea jambo na Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahahriri Tanzania Ndg. Deodatus Balile pamoja na Makamu Mwenyekiti wa Taasisi ya Kimataifa ya Habari (IPI) Ndg. Hadija Patel walipomtembelea Ofisini kwake Jijini Dodoma hii leo. 

Spika wa Bunge Mheshimiwa Job Ndugai akiwa katiika picha ya pamoja na ujumbe kutoka Taasisi ya Kimataifa ya Habari (IPI) na Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) Ofisini kwake Jijini Dodoma hii leo.