Baadhi ya mabalozi
wanaoziwakilisha nchi zao nchini Tanzania wakielekea ndani ya Ukumbi wa Bunge
leo kusikiliza Hotuba ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Mambo ya
Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.
Waziri wa Elimu,
Sayansi na Mafunzo ya Ufundi Prof. Joyce Ndalichako akisalimiana na Mbunge wa
Afrika Mashariki Mhe. Shy-Rose Bhanji nje ya Ukumbi wa Bunge leo mjini Dodoma.
Mbunge wa Mafinga
Mjini Mhe. Cosato Chumi akichangia kuhusu Hotuba ya Makadirio ya Mapato na
Matumizi ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki
iliyowasilishwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki
Mhe.Augustine Mahiga leo mjini Dodoma.
Baadhi ya Mawaziri
wakifuatilia michango mbalimbali ya wabunge wakati wa mjadala wa Makadirio ya
Mapato na Matumizi ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki iliyowasilishwa leo mjini Dodoma.
Waziri wa Ardhi,
Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi akizungumza jambo na Mbunge
wa Iringa Mjini Mhe. Peter Msigwa nje ya Ukumbi wa Bunge leo mjini Dodoma.Wengine ni Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe.Augustine Mahiga(kushoto)
na Madiwani wa jimbo la Iringa Mjini waliolitembelea Bunge.
Waziri wa Ardhi,
Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi akimweleza jambo Waziri wa
Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira na Muungano Mhe. Januari Makamba nje ya
Ukumbi wa Bunge leo mjini Dodoma.
Wabunge kutoka mkoa
wa Iringa Mhe. Augustine Mahiga, Mhe. William Lukuvi na Mhe. Peter Msigwa
wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya madiwani wa Iringa mjini waliolitembelea
Bunge leo mjini Dodoma.
Naibu Spika wa Bunge
la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Tulia Ackson akiwasikiliza waangalizi
wa Uchaguzi Mkuu kutoka Umoja wa Nchi za Ulaya (EU) waliofika Ofisini kwake kuwasilisha
Taarifa ya Umoja huo kuhusu Uchaguzi Mkuu uliofanyika nchini Oktoba 25, 2015.
Waangalizi wa Uchaguzi Mkuu kutoka Umoja wa Nchi
za Ulaya (EU) wakizungumza na Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe. Tulia Ackson (hayupo pichani) ofisini kwake Dodoma.
Balozi wa Umoja wa Ulaya
Mhe. Roeland Van De Geer (kulia) akimkabidhi Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Tulia Ackson Taarifa ya kuhusu Uchaguzi Mkuu mjini Dodoma uliofanyika
nchini Tanzania Oktoba 25, 2015.
Naibu Spika wa Bunge
la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Tulia Ackson (kulia) akizungumza jambo na Waangalizi
wa Uchaguzi kutoka Umoja wa Ulaya Mhe. Judith Sargentini (kushoto) na Balozi wa Umoja huo Mhe. Roeland Van De Geer (katikati) waliofika
Ofisini kwake Dodoma leo.
Mwangalizi Mkuu wa Uchaguzi kutoka Umoja wa Ulaya Mhe. Judith Sargentini akimkabidhi Naibu Spika wa Bunge
la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Tulia Ackson Taarifa ya Uchaguzi ya Waangalizi
wa Umoja wa Ulaya (EU) kuhusu Uchaguzi Mkuu wa Tanzania uliofanyika Oktoba 25, 2015. Hafla hiyo imefanyika leo mjini Dodoma.
Naibu Spika wa Bunge
la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Tulia Ackson (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Waangalizi
wa Uchaguzi kutoka Umoja wa Nchi za Ulaya (EU) waliomtembelea Ofisini kwake leo mjini Dodoma.
PICHA/Aron Msigwa na Fatma Salum.
PICHA/Aron Msigwa na Fatma Salum.