Katibu wa Bunge, Ndg. Nenelwa
Mwihambi, ndc amesema hadi kufikia leo saa Kumi Jioni Majina
ya jumla ya Wagombea Tisa (9) yalikuwa yamewasilishwa na kukidhi matakwa ya
kisheria kwa ajili ya uchaguzi wa Spika unaotarajiwa kufanyika kesho tarehe 1
Februari, 2022.
Akizungumza na Waandishi wa Habari
Jijini Dodoma, Katibu wa Bunge amesema kuwa miongoni mwa Wagombea hao nane sio
Wabunge na mmoja ni Mbunge.
Aliwataja magombea hao kuwa ni Abdullah
Mohammed Said (NRA), Mhandisi Aivan Jackson Maganza (TLP), David Daud
Mwaijojele (CCK), Georges Gabriel Bussungu (ADA -TEA), Kunje Ngombale Mwiru
(SAU), Maimuna Said Kassim (ADC), Ndonge Said Ndonge (AAFP), Saidoun Abrahamani
Khatib (DP) na Mheshimiwa Dkt. Tulia Ackson (Mb).