Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Mhe. Mussa Azzan Zungu (Mb), amengoza kikao cha Kamati ya Uongozi
kilichofanyika leo tarehe 8 Aprili, 2025 katika Ukumbi wa Spika, Bungeni Jijini
Dodoma.
Pamoja na mambo mengi kikao hicho kilipokea na kujadili
Mapendekezo ya Ratiba ya Mkutano wa Kumi na Tisa wa Bunge.
Mkutano wa Kumi na Tisa wa Bunge umeanza leo tarehe 8 Aprili, 2025, Bungeni Jijini Dodoma.
Vile vile, Kikao hicho kilihudhuriwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu; Sera, Bunge na Uratibu, Mhe. William Lukuvi (Mb) na Katibu wa Bunge, Ndg. Baraka Leonard.