WELCOME TO TANZANIA NATIONAL ASSEMBLY OFFICIAL BLOG: CONTACT US: P.O.BOX 941 DODOMA, TANZANIA, WEBSITE: parliament.go.tz , FIND US ON FACEBOOK >>> www.facebook.com/bungetz1, FOLLOW US ON TWITTER >>> @bunge_tz.>>>KARIBUNI

Friday, November 16, 2018

MAKAMU WA RAIS WA BUNGE LA CHINA ATEMBELEA BUNGE LA TANZANIA JIJINI DODOMA




Makamu wa Rais wa Bunge la Jamhuri ya Watu wa China Mhe. CAI Dafenga akipunga mkono wakati alipotambulishwa  Bungeni mapema leo Jijini Dodoma. Wa pili toka kulia ni Naibu Spika wa Bunge Mhe. Dkt. Tulia Ackson, Balozi wa China nchini Bi. WANG wa kwanza kulia. Makamu huyo wa Rais ametembelea Bunge la Tanzania akiambatana na Wabunge kumi na tano kwa lengo la kudumisha ushirikiano baina ya pande zote mbili.



Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai (kulia) akizungumza na Makamu wa Rais wa Bunge la Jamhuri ya watu wa China Mhe. CAI Dafeng (kushoto). Makamu huyo wa Rais akiambatana na Wabunge kumi na tano wametembelea Bunge la Tanzania kwa lengo la kudumisha ushirikiano baina ya pande zote mbili.



Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai akizungumza na Makamu wa Rais wa Bunge la Jamhuri ya watu wa China Mhe. CAI Dafeng pamoja na Ujumbe wake walipotembelea Bunge mapema leo. Mazungumzo hayo yalihudhuriwa pia na Naibu Spika wa Bunge Dkt. Tulia Ackson (wa kwanza kulia) Mwenyekiti wa Bunge Mhe. Mussa Azzan Zungu, Katibu wa Bunge Ndg. Stephen Kagaigai, Balozi China nchini Bi. WANG Ke na baadhi ya Wabunge kutoka Bunge la Tanzania na Wabunge kumi na tano kutoka Bunge la China.



Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai (kulia) akimkabidhi zawadi ya picha ya Jengo la Bunge Makamu wa Rais wa Bunge la Jamhuri ya watu wa China Mhe. CAI Dafeng (kushoto) mara baada ya kuzungumza naye Ofisini kwake Jijini Dodoma.




Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai (kulia) katika picha ya pamoja na Makamu wa Rais wa Bunge la Jamhuri ya watu wa China Mhe. CAI Dafeng (kushoto) mara baada ya kuzungumza naye Ofisini kwake Jijini Dodoma.



Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai (katikati) katika picha ya pamoja na Makamu wa Rais wa Bunge la Jamhuri ya watu wa China Mhe. CAI Dafeng, (wa pili kutoka kushoto) Naibu Spika wa Bunge Dkt. Tulia Ackson (wa pili kutoka kulia) Mwenyekiti wa Bunge Mhe. Mussa Azzan Zungu (wa kwanza kulia) na Balozi China nchini Bi. WANG Ke (wa kwanza kushoto) mara baada ya mazungumzo Ofisini kwake Jijini Dodoma

Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai (kulia) akiagana na Makamu wa Rais wa Bunge la Jamhuri ya watu wa China Mhe. CAI Dafeng mara baada ya kuzungumza naye Ofisini kwake Jijini Dodoma. Kushoto ni Balozi China nchini Bi. WANG Ke.

Tuesday, November 13, 2018

WIZARA YA FEDHA YATOA SEMINA KWA WAJUMBE WA KAMATI YA BAJETI

Spika wa Bunge Mheshimiwa Job Ndugai  akitoa shukrani kwa Benki ya Diamond Tust mbele ya Waandishi wa Habari mara baada ya kupokea  Mashine  maalum ya kuwasaidia watoto wanaozaliwa kabla ya kufikisha miezi tisa iliyotolewa na Benki hiyo kwa Hospitali ya Wilaya ya Kongwa hii leo.


Spika wa Bunge Mheshimiwa Job Ndugai akipokea mojawapo ya Mashine  maalum ya kuwasaidia watoto wanaozaliwa kabla ya kufikisha miezi tisa iliyotolewa na Benki ya Diamond Tust kwa Hospitali ya Wilaya ya Kongwa hii leo.

Spika wa Bunge Mheshimiwa Job Ndugai  akisikiliza maelezo kutoka kwa mwanzilishi wa Taasisi ya Doris Mollel Foundation Ndg. Doris Mollel kuhusiana na picha inayoonyesha mtoto aiyezaliwa kabla ya muda wake. Taasisi hiyo ikishirikiana na Benki ya Diamond Trust walitoa msaada wa  Mashine  maalum ya kuwasaidia watoto wanaozaliwa kabla ya kufikisha miezi tisa kwa Hospitali ya Wilaya ya Kongwa hii leo.

Saturday, November 10, 2018

WIZARA YA FEDHA WATOA SEMINA KWA WAJUMBE WA KAMATI YA BAJETI

Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti wakifuatilia jambo katika Semina iliyotolewa na Wizara ya Fedha na Mipango hii leo kwenye Ukumbi wa Msekwa Jijini Dodoma.

Ndg. Michael Nyagoya ambae ni Kaimu Kamishna Msaidizi Idara ya Sera na Utafiti Kitengo cha Maendeleo ya Sekta ya Fedha akitoa Mada wa Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti hii leo kwenye Ukumbi wa Msekwa Jijini Dodoma.

Sehemu ya watumishi kutoka Ofisi ya Bunge pamoja na Wabunge wakifuatilia jambo katika Semina iliyotolewa na Wizara ya Fedha na Mipango kwa Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti hii leo kwenye Ukumbi wa Msekwa Jijini Dodoma.