WELCOME TO TANZANIA NATIONAL ASSEMBLY OFFICIAL BLOG: CONTACT US: P.O.BOX 941 DODOMA, TANZANIA, WEBSITE: parliament.go.tz , FIND US ON FACEBOOK >>> www.facebook.com/bungetz1, FOLLOW US ON TWITTER >>> @bunge_tz.>>>KARIBUNI

Tuesday, April 12, 2016

OFISI YA BUNGE ALIPOWASILISHA HUNDI YA BILIONI SITA KWA MHE. RAIS BAADA YA KUBANA MATUMIZI


Rais Dkt. John Pombe Magufuli akitazama Hundi Kifani yenye thamani ya Shilingi Bilioni Sita mara baada ya kukabidhiwa na Naibu Spika Dkt. Tulia Ackson mara baada ya Ofisi ya Bunge kutekeleza kwa vitendo kauli ya kubana matumizi ili fedha hizo zikatumike kwa ajili ya ununuzi wa madawati kwa ajili ya wanafunzi.


Naibu Spika Dkt. Tulia Ackson  akimkabidhi Rais Dkt. John Pombe Magufuli Hundi Kifani yenye thamani ya Shilingi Bilioni Sita mara baada ya Ofisi ya Bunge kutekeleza kwa vitendo kauli ya kubana matumizi yasio na Tija ili fedha hizo zikanunulie madawati kwa ajili ya wanafunzi.


Rais Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Naibu Spika Dkt. Tulia Ackson kulia, Katibu wa Bunge Dkt. Thomas Kashilillah pamoja na wafanyakazi wengine wa Bunge wakiwa wameishika hundi Kifani hiyo yenye thamani ya Shilingi Bilioni Sita. Rais Dkt. Magufuli ameipongeza Taasisi ya Bunge kutokana na hatua hiyo ya kubana matumizi na kuamua fedha zao zitumike katika kununulia madawati kwa ajili ya wanafunzi.

Naibu Spika Dkt. Tulia Ackson akiongea Ikulu kabla kumkabidhi Rais Dkt. John Pombe Magufuli hundi kifani yenye thamani ya Shilingi Bilioni Sita.


Rais Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Katibu Mkuu Kiongozi Mhandisi John Kijazi wapili kulia, Dkt. Tulia Ackson wakwaza kulia, Katibu wa Bunge Dkt. Thomas Kashilillah wakwanza kushoto, Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, Kamishna Valentino Mlowola Ikulu Jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment