Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania Mhe. Dkt. Tulia Ackson akiongoza kikao cha 34 cha Bunge la Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania leo mjini Dodoma.
Waziri Mkuu wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa akifurahia jambo na Waziri
wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye ndani ya Ukumbi wa
Bunge kabla ya kuanza kwa kikao cha 34 cha Mkutano wa 3 wa Bunge mjini Dodoma.
Wanafunzi
wa Shule ya Msingi na Sekondari Moga iliyoko jijini Dar es salaam wakifuatilia
shughuli za kikao cha 34 cha Bunge mjini Dodoma. Wanafunzi 90 wa shule hiyo
wamelitembelea Bunge hilo kujifunza namna linavyoendeshwa.
Baadhi ya
Mawaziri na Wabunge wakiwa ndani ya Ukumbi wa Bunge wakati wa kikao cha 34
mjini Dodoma.
Naibu Waziri
wa Malisili na Utalii Mhe.Mhandisi Ramo Makani akijibu maswali ya Wabunge
yaliyoelekezwa kwenye wizara hiyo wakati wa kipindi cha Maswali na majibu leo,
Dodoma.
Waziri wa
Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu Wenye
Ulemavu Mhe. Jenista Muhagama akitoa ufafanuzi kuhusu masuala mbalimbali ya
utendaji wa Serikali ndani ya ukumbi wa Bunge leo mjini Dodoma.
Waziri wa
Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango akiwasilisha Bungeni Makadirio ya Mapato na
Matumizi ya Wizara ya Fedha na Mipango kwa mwaka wa Fedha 2016/2017 leo mjini Dodoma. Wizara
hiyo inaliomba Bunge lipitishe kiasi cha shilingi Trilioni 8.7 kwa ajiri ya
matumizi ya kawaida na matumizi mengine.
Waziri wa
Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango (kushoto) na Naibu wake Dkt. Ashatu Kijaji
wakiandika maoni ya Wabunge waliokuwa wakichangia Makadirio ya Mapato na
Matumizi ya Wizara Fedha na Mipango kwa mwaka wa Fedha 2016/2017 leo mjini
Dodoma.
Waziri
Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa(kulia)
akimsikiliza Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe.
Luhaga Mpina nje ya Ukumbi wa Bunge leo.
Waziri
Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa(kushoto)
akisalimiana na Mbunge wa Kilolo Mhe. Venance Mwamoto nje ya Ukumbi wa Bunge,
Dodoma.
Baadhi
ya Walimu na Wanafunzi wa Shule ya Msingi na Sekondari Moga iliyoko jijini Dar
es salaam wakiwa katika picha ya pamoja nje ya Ukumbi wa Bunge mara baada ya
kutoka ndani ya ukumbi wa Bunge kufuatilia shughuli za kikao cha 34.
Waziri wa
Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango (kushoto) akizungumza jambo na Naibu Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Suzan Kolimba (kulia)
kwenye viwanja vya Bunge, Dodoma.
No comments:
Post a Comment