WELCOME TO TANZANIA NATIONAL ASSEMBLY OFFICIAL BLOG: CONTACT US: P.O.BOX 941 DODOMA, TANZANIA, WEBSITE: parliament.go.tz , FIND US ON FACEBOOK >>> www.facebook.com/bungetz1, FOLLOW US ON TWITTER >>> @bunge_tz.>>>KARIBUNI

Wednesday, July 20, 2016

RAIS ALIPOGAWA MADAWATI YALIYOTENGENEZWA BAADA YA OFISI YA BUNGE KUBANA MATUMIZI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akipokea Dawati kutoka kwa Naibu Spika wa Bunge Dkt. Tulia Ackson kwa ajili ya kuyagawa kwa Waheshimiwa Wabunge katika Viwanja vya Karimjee, Jijini Dar es Salaam.


Rais Dkt John Pombe Magufuli na Viongozi wengine wa Kiataifa wakiwa katika picha ya pamoja na Makamishina wa Tume ya Utumishi ya Bunge mara baada ya kugawa Madawati yaliyotengezwa kwa fedha zilizopatikana baada ya Ofisi ya Bunge kubana matumizi.

Wanafunzi wa shule ya Msingi Bunge wakipakia Madawati tayari kuyapeleka shuleni kwao baada ya Rais kuyagawa

Naibu Spika wa Bunge Dkt Tulia Ackson (kulia) akimuonesha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli Madawati ili aweze kuyagawa kwa Waheshimiwa Wabunge

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akikagua Madawati yaliyotengenezwa baada ya Ofisi ya Bunge kubana matumizi.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiendelea kukagua Madawati yaliyotengenezwa baada ya Ofisi ya Bunge kubana matumizi.

Rais Dkt John Pombe Magufuli akimkabidhi Mwenyekiti wa Bunge Mhe. Mussa Azzan Zungu (Mb) Madawati kwa niaba ya Wabunge wote. Madawati hayo yametengenezwa kutokana na fedha zilizopatikana baada ya Ofisi ya Bunge kubana matumizi.

Rais Dkt John Pombe Magufuli (kulia) pamoja na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa (katikati) na Naibu Spika wa Bunge Dkt Tulia Ackson katika picha ya pamoja wakiwa wamekalia Madawati kabla ya kuyagawa kwa Waheshimiwa Wabunge.

No comments:

Post a Comment