Kamati ya Kudumu ya
Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imefanya ziara katika katika Pori Tengefu la Loliondo ili
kujionea hali hailisi ya mgogogro wa muda mrefu katika pori hilo kwa kutembelea
baadhi ya maeneo muhimu ambayo ndio hutajwa kama kiini cha mgogoro huo.
Mwenyekiti wa
kamati hiyo Mheshimiwa Muhandisi Atashasta
Nditiye anasema wamejionea walicho kiona na wataishauri serikali
ipasavyo ili iweze kutoa maamuzi sahihi ili kumaliza mvutano wa muda mrefu
katika eneo hilo
Mheshimiwa
Mhandisi Nditiye amesema wajumbe wa kamati hiyo, wamefanikiwa kupita sehemu
kubwa ya eneo hilo, ambalo linapendekezwa kugawanywa ili kutengwa eneo la
kilomita 1500 kwa ajili ya uhifadhi wa ikolojia ya Serengeti.
Akitoa maelezo kwa
wajumbe wa kamati hiyo, Mhifadhi mkuu wa hifadhi ya Serengeti, William
Mwakilema alisema kwa manufaa yaTaifa na dunia ni muhimu kutengwa eneo la
kilomita 1500 ili lihifadhiwe.
Alisema eneo hilo
ambalo ni mapito ya nyumbu kutoka hifadhi ya Masai Mara nchini Kenya, hadi
Serengeti na baadaye hifadhi ya Ngorongoro pia ndio eneo la mazalia ya nyumbu na
vyanzo vya maji, limeharibiwa sana na mifugo na shughuli za kibinaadamu na lisipo
hifadhiwa uhai wa Serengeti upo mashakani.
Hata hivyo,
Mwenyekiti wa halmashauri ya Loliondo, Methew Siloma alisema msimamo wao bado wanapinga
kutengwa eneo hilo kwa kuwa ni la vijiji na wanataka kutafutwa suluhu.
Mbunge Geita, Joseph
Kasheku (Msukuma) ambaye ni mjumbe wa kamati hiyo alieleza kuwa ameona udhaifu uliopo
katika utunzwaji wa eneo hilo na kutaka jamii inayozunguka eneo hili
ishirikishe ili kutambua umuhimu wa eneo hilo.
Wabunge wengine Mheshimiwa
Grace Kiwelu na mheshimiwa Lucy Owenya wa viti maalum mkoa Kilimanjaro
wameshauri kutazamwa maslahi mapana ya taifa katika kulinda ikolojia ya
Serengeti.
Kwaupande wake
Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe, alisema dhamira ya serikali
ni kuhakikisha ikolojia ya Serengeti inalindwa kwa manufaa ya sasa na vizazi vijavyo.
Eneo hilo la pori
Tengefu la Loliondo lenye kilomita za mraba 4000, limeingia katika mgogoro
baada ya wizara ya Maliasilina Utalii, kutangaza uamuzi ya kutaka kulitenga
eneo la kilomita 1500 kwa ajili ya uhifadhi na eneo lililobaki kurejeshwa kwa
halmashauri ya Ngorongoro.
Waziri wa Maliasili na utalii Mhe. Prof Jumanne Maghembe akifafanua jambo kwa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii wakati walipotembelea Pori Tengefu la Loliondo |
No comments:
Post a Comment