SPIKA WA BUNGE AKIONGOZA KIKAO CHA MASHAURIANO BAINA YA SERIKALI NA KAMATI YA BAJETI SIKU MOJA KABLA YA KUSOMWA KWA BAJETI KUU YA SERIKALI.
Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (katikati) akiongoza kikao cha
mashauriano baina ya Serikali na Kamati ya Bajeti. Kikao hicho ambacho
kimefanyika siku moja kabla ya kusomwa kwa Bajeti kuu ya Serikali ni
kwa ajili Kufanya Majumuisho Kwa kuzingatia Hoja zenye Maslahi kwa Taifa
zilizojitokeza wakati wa kujadili Bajeti za Wizara. Kulia kwa Mhe Spika
ni Waziri Mkuu, Mheshimiwa Kassim Majaliwa na Kushoto kwake ni Katibu
wa Bunge, Dkt. Thomas Kashililah na anaefuata ni Naibu Spika wa Bunge,
Mheshimiwa Dkt. Tulia Ackson.
No comments:
Post a Comment