Mhariri Mtendaji wa Gazeti la Mtanzania Bw. Denis
Msacky akijieleza mbele ya Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge Nipashe
kwa kosa la kutoa taarifa zinazohusu
ushahidi na mwenendo wa kikao cha Kamati
hiyo bila kupata idhini ya Bunge kitendo ambacho ni kinyume na kifungu cha 34
(1) (f) na (g) ya Sheria ya Kinga,
Madaraka na Haki za Bunge, Sura ya 296.
Mhariri/Mwandishi wa Habari Gazeti la
Mtanzania Bw. Bakari Kimwaga akiapaa kabla ya kuanza akijieleza mbele ya Kamati ya Haki, Maadili na
Madaraka ya Bunge Nipashe kwa kosa la kutoa
taarifa zinazohusu ushahidi na mwenendo wa kikao cha Kamati hiyo bila kupata idhini ya
Bunge kitendo ambacho ni kinyume na kifungu cha 34 (1) (f) na (g) ya Sheria ya Kinga, Madaraka na Haki
za Bunge, Sura ya 296.
Mhariri Mtendaji wa Gazeti la Mwananchi Bw. Angetile Osiah na Mwanasheria wake mbele ya Kamati
ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge Nipashe kwa kosa la kutoa taarifa zinazohusu ushahidi na
mwenendo wa kikao cha Kamati hiyo bila
kupata idhini ya Bunge kitendo ambacho ni kinyume na kifungu cha 34 (1)
(f) na (g) ya Sheria ya Kinga, Madaraka
na Haki za Bunge, Sura ya 296.
Mhariri wa Gazeti la Nipashe Bw. Edmond
Msangi akijieleza mbele ya Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge Nipashe
kwa kosa la kutoa taarifa zinazohusu
ushahidi na mwenendo wa kikao cha Kamati
hiyo bila kupata idhini ya Bunge kitendo ambacho ni kinyume na kifungu cha 34
(1) (f) na (g) ya Sheria ya Kinga,
Madaraka na Haki za Bunge, Sura ya 296.
Na Debora Sanja
Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge, imewahoji wahariri
pamoja Waandishi wa Habari wa Magazeti ya Mtanzania, Mwananchi na Nipashe kwa kosa
la kutoa taarifa zinazohusu ushahidi na
mwenendo wa kikao cha Kamati hiyo bila
kupata idhini ya Bunge.
Akizungumza mara baada ya kuwahoji mashahidi hao, Mwenyekiti
wa Kamati hiyo, Mhe. Almasi Athuman
Maige (Mb) alisema wahusika wote walifika mbele ya Kamati na kujibu
tuhuma hizo ambazo ni kinyume na kifungu cha 34 (1) (f) na (g) ya Sheria ya Kinga, Madaraka na Haki
za Bunge, Sura ya 296.
Mheshimiwa Maige alisema Kamati baada ya kuwasikiliza mashahidi
wote waliofika itaandaa Taarifa yake na kuiwasilisha kwa Spika wa Bunge,
Mheshimiwa Job Ndugai.
“Kanuni zimeweka masharti kuwa shughuli za Kamati hii
zinazofanywa zitabakia kuwa ni siri hadi hapo itakapomaliza kazi yake na
kuwasilisha taarifa Bungeni,” alisema.
Aliwataja waliofika katika Kamati hiyo kuwa ni Ndugu Denis
Msaki ambaye ni Mhariri Mtendaji wa gazeti la Mtanzania na mwandishi wake Ndugu
Bakari Kimwanga, Ndugu Edmond Msangi Mhariri Mtendaji wa Gazeti la Nipashe na
mwandishi wake Ndugu Gwamaka Alipipi na Ndugu Angetile Osiah Mhariri Mtendaji
wa gazeti la Mwananchi na Mwandishi wake
Ndugu Elias Msuya.
No comments:
Post a Comment