BUNGE LA EALA NA BUNGE LA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WATOA RAMBIRAMBI KUFUATIA AJALI YA MV NYERERE
Spika wa Bunge Mheshimiwa Job Y. Ndugai (Mb), (kushoto) akimsilikiliza Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki Mheshimiwa Alhaji Adam Kimbisa. Mheshimiwa Kimbisa amkabidhi Mhe. Spika kiasi cha Shillingi Milioni Nane Laki tano na elfu Hamsini kwa niaba ya Wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki ikiwa ni rambirambi kufuatia ajali ya kivuko cha Mv Nyerere. Kulia ni Katibu wa Bunge Ndg. Stephen Kagaigai.
Spika wa Bunge akisisitiza jambo mbele ya wanahabari baada ya kupokea rambirambi kutoka kwa Wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki (EALA) Shilling i Milioni Nane Laki Tano na Hamsini elfuikiwa ni rambirambi kufuatia ajali ya kivuko cha Mv Nyerere zilizowasilishwa na Mheshimiwa Alhaji Adam Kimbisa (kushoto) .Bunge la Jamahuri ya Muungano pia limetoa rambirambi yake kiasi cha Sh. milioni 86
Spika wa Bunge Mheshimiwa Job Y. Ndugai (Mb), akipokea shilingi Milioni Nane Laki tano na Elfu Hamsini kutoka kwa Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki Mheshimiwa Alhaji Adam Kimbisa kwa niaba ya Wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki ikiwa ni rambirambi kufuatia ajali ya kivuko cha Mv Nyerere. Bunge la Jamahuri ya Muungano pia limetoa rambirambi yake kiasi cha Sh. milioni 86
No comments:
Post a Comment