WELCOME TO TANZANIA NATIONAL ASSEMBLY OFFICIAL BLOG: CONTACT US: P.O.BOX 941 DODOMA, TANZANIA, WEBSITE: parliament.go.tz , FIND US ON FACEBOOK >>> www.facebook.com/bungetz1, FOLLOW US ON TWITTER >>> @bunge_tz.>>>KARIBUNI

Tuesday, March 5, 2019

KAMATI YA BAJETI YATEMBELEA KIWANDA CHA KUTENGENEZA TRANSFOMA

Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Bajeti, Mhe. George Simbachawene akiwa  na Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda cha kutengeneza Transfoma (TANELEC) , Ndugu Zahir Salim wakati Kamati ilipotembelea Kiwanda hicho kilichopo Jijini Arusha.

Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Bajeti, Mhe. George Simbachawene akisalimiana na Waziri wa Nishati, Mhe. Medard Kalemani wakati Kamati hiyo ilipotembelea Kiwanda cha kutengeneza Transfoma (TANELEC) kilichopo Arusha , pembeni ya Waziri ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda hicho, Ndugu Zahir Salim.

Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda cha kutengeneza Transfoma (TANELEC) , Ndugu Zahir Salim akiwaelezea wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Bajeti jinsi mitambo mbalimbali ya kuzalisha transfoma inavyofanya kazi, pembeni yake ni Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhe. George Simbachawene na Waziri wa Nishati, Mhe. Medard Kalemani. Kamati ilitembelea Kiwanda hicho kilichopo Jijini Arusha

Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda cha kutengeneza Transfoma (TANELEC) , Ndugu Zahir Salim akiwaelezea wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Bajeti jinsi mitambo mbalimbali ya kuzalisha transfoma inavyofanya kazi, pembeni yake ni Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhe. George Simbachawene na Waziri wa Nishati, Mhe. Medard Kalemani. Kamati ilitembelea Kiwanda hicho kilichopo Jijini Arusha

Mfanyakazi wa Kiwanda cha kutengeneza Transfoma (TANALEC), Sara Laizer akielezea majukumu yake kwa wajumbe kwa Kamati ya Bunge ya Bajeti, Kamati hiyo ilitembelea kiwanda hicho kilichopo Arusha. Nyuma yake ni Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhe. George Simbachawene na Waziri wa Nishati, Mhe. Medard Kalemani

Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Bajeti wakitembelea Kiwanda cha kutengeneza Transfoma (TANELEC kuona jinsi kiwanda hicho kinavyofanya kazi, wa kwanza mbele ni Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhe. George Simbachawene, Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda hicho, Ndugu Zahir Salim na Waziri wa Nishati, Mhe. Medard Kalemani. Kamati ilitembelea Kiwanda hicho kilichopo Jijini Arusha

Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Bajeti, Mhe. George Simbachawene akipanda mti wa kumbukumbu wakati Kamati hiyo ilipotembelea Kiwanda cha Kutengeneza Tansfoma TANALEC kilichopo Arusha. Nyuma ni Waziri wa Nishati, Mhe. Medard Kalemani, Mkuu wa Wilaya ya Arusha, Mhe. Gabriel Daqarro na Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda hicho, Ndugu Zahir Salim

Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Bajeti wakiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Nishati Mhe. Medard Kalemani na uongozi wa Kiwanda cha kutengeneza Transfoma  cha TANELEC, wajumbe hao walitembelea Kamati hiy kuona jinsi kiwanda hicho kinavyofanya kazi.

No comments:

Post a Comment