BUNGE limepitisha Bajeti Kuu ya Serikali ya shilingi trilioni 36.68 kwa mwaka wa fedha 2021/2022 ambapo Wabunge 361 sawa na asilimia 94 wamepiga kura ya ndio.
Akitangaza matokeo ya upigaji wa kura mara baada ya mjadala wa Bajeti ya Serikali uliofanyika kwa takribani wiki moja Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai amesema kuwa Wabunge waliopiga kura ni 385 ambapo waliopiga kura ya Ndio ni 361 sawa na asilimia 94, waliopiga kura isiyo ya maamuzi (hawajakataa wala kukubali) ni 23 sawa na asilimia 6 na Wabunge watano (5) hawakuwepo wakati wa zoezi hilo la upigaji kura.
Aidha, mara baada ya upigaji huo wa kura Bunge lilipitisha Muswada wa Sheria ya kuidhinisha Matumizi ya Serikali wa mwaka 2021 (The Appropriation Bill, 2021) wenye dhumuni la kuidhinisha Matumizi ya jumla ya Shilingi 36,681,897,765,000.
Mara baada ya
kupitisha Bajeti zote za Wizara pamoja na Bajeti kuu ya Serikali, Mkutano wa
Tatu wa Bunge unatarajia kuendelea na ukamilishaji wa shughuli zilizobaki za
Kiserikali na Kamati kabla ya kuahirishwa Juni 30, 2021.
No comments:
Post a Comment