WELCOME TO TANZANIA NATIONAL ASSEMBLY OFFICIAL BLOG: CONTACT US: P.O.BOX 941 DODOMA, TANZANIA, WEBSITE: parliament.go.tz , FIND US ON FACEBOOK >>> www.facebook.com/bungetz1, FOLLOW US ON TWITTER >>> @bunge_tz.>>>KARIBUNI

Tuesday, February 1, 2022

DKT TULIA ACKSON ACHAGULIWA KUWA SPIKA



Mbunge wa Mbeya Mjini, Dkt. Tulia Ackson akila kiapo cha uaminifu mbele ya Waheshimiwa Wabunge mara baada ya kuchaguliwa kwa kura zote 376 za Wabunge waliokuwa Bungeni kuwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.


Mbunge wa Mbeya Mjini, Dkt. Tulia Ackson akila kiapo cha uaminifu mbele ya Waheshimiwa Wabunge mara baada ya kuchaguliwa kwa kura zote 376 za Wabunge waliokuwa Bungeni kuwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.


 

Dkt. Tulia akijinadi Bungeni
Waheshimiwa Wabunge wakimsindikiza Mhe. Dkt Tulia kwenda kuapa
Spika wa Bunge, Mhe. Dkt Tulia akizungumza mara baada ya kula kiapo

Spika wa Bunge, Mhe. Dkt. Tulia Ackson katika picha ya pamoja na Katibu wa Bunge, Ndg. Nenelwa Mwihambi, ndc mara baada ya kuapishwa Bungeni Jijini Dodoma.
Spika wa Bunge, Mhe. Dkt. Tulia Ackson akipata nasaha kutoka kwa Spika Mstaafu, Mhe. Pius Msekwa
Spika wa Bunge, Mhe. Dkt. Tulia Ackson (katikati) katika picha na Maspika Wastaafu, Mhe. Anne Makinda na Pius Msekwa mara baada ya kuapishwa Bungeni Jijini Dodoma.
Spika wa Bunge, Mhe. Dkt. Tulia Ackson akipongezwa na Mwenyekiti wa Kikao cha Uchaguzi wa Spika, Mhe. William Lukuvi
Spika wa Bunge, Mhe. Dkt. Tulia Ackson akimuapisha Mbunge wa Ngorongoro, Mhe. Emmanuel Lekishon Shangai Bungeni Jijini Dodoma.
Spika wa Bunge, Mhe. Dkt. Tulia Ackson akiongoza Kikao cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya  Uongozi Jijini Dodoma


DKT TULIA ACKSON ACHAGULIWA KUWA SPIKA

Mheshimiwa Dkt. Tulia Ackson (Mb) ameshinda nafasi ya Spika wa Bunge kwa kupata kura zote 376 za wabunge waliohudhuria katika uchaguzi uliofanyika leo Bungeni Jijini Dodoma.

Mheshimiwa Dkt. Tulia amewashinda wagombea wenzake wanane ambao wote waliambulia kura sifuri.

Akitoa salamu za shukrani baada ya kuapishwa katika nafasi hiyo, mbali na wengi aliowashukuru Mheshimiwa Spika alikishukuru Chama chake cha Mapinduzi kikiongozwa na Mwenyekiti, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kwa kuteua jina lake kugombea nafasi hiyo.

Aliwashukuru pia wabunge kwa kuonyesha imani kwake kwa kumpa kura za kishindo zilizomwezesha kupata heshima ya kuwa Spika na kwamba imani hiyo waliyomuonyesha itakuwa chachu ya utendaji katika kuliongoza Bunge.

“Ninawaomba tuendelee kushikamana katika kuwatumikia wananchi wenzetu na kusimamia maslahi ya Taifa letu,” alisema.

“Ninamshukuru sana Spika mstaafu Mheshimiwa Job Yustino Ndugai, alinifunza mengi, alinielekeza, alinishauri aliniongoza vizuri kama Mbunge na kama msaidizi wake katika uendeshaji wa Bunge letu, alinipa fursa mbalimbali ambazo zililenga kuboresha utendaji kazi wangu katika kipindi chote cha miaka sita nilichohudumu nafasi ya Naibu Spika” alisema

Aidha, akielezea safari yake katika siasa, alimshukuru Hayati, Rais Dkt. John Magufuli kwa kumteua kuwa Mbunge mwaka 2015 na wananchi wa Mbeya Mjini kwa kumchagua kuwa Mbunge katika Uchaguzi wa mwaka 2020.

Aliwashukuru pia wagombea wenzake na kuwataka kuungana wote kwa pamoja kuwatumika wananchi na kuijenga Tanzania imara kisiasa, kiuchumi na kijamii ili kwa pamoja waijenge Tanzania yenye mshikamano.

Aliwakumbusha Waheshimiwa Wubunge Dira Kuu inayowaongoza kufanya kazi ambayo ilitolewa na Mheshimiwa Rais Samia Suhulu Hassan katika Hotuba yake aliyoitoa Bungeni tarehe 22 Aprili, 2021 ambapo alianisha vipaumbele vya Serikali ya Awamu ya Sita.

“Kwa Hotuba ile,  matumaini ya Mheshimiwa Rais kwa  mawaziri, manaibu mawaziri  chini ya uongozi madhubuti wa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Kassim Majaliwa watavisimamia vipaumbe hivyo na kuvitekeleza kwa umahiri mkubwa.

“Kwa upande wetu sisi Wabunge kazi yetu imeainishwa vizuri ndani ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ibara ya 63, kwa mujibu Ibara hii Bunge ndicho chombo kikuu chenye madaraka na wajibu kwa niaba ya wananchi wa kuisimamia na kuishauri Serikali, Taasisi na vyombo vyake vyote katika kutekeleza majukumu yake.

“Katika muktadha wa vipaumbele vya Serikali ya Awamu ya Sita vilivyoainishwa na Mheshimiwa Rais, Bunge hili tukufu ni mfano wa daraja.

“Kwa dhamana hii mliyonipa nitatumia nguvu zangu zote kadri nitakavyojaliwa na Mwenyezi Mungu kuliongoza Bunge hili tukufu kwa makini ili liwe daraja madhubuti kati ya  wananchi na Serikali yao.

“Tutaliongoza Bunge hili kuisimmia na kuishauri Serikali ili liweze kutekeleza wajibu wake ipasavyo, tutauliza maswali, tutaihoji Serikali kwa hekima na busara na kwa kuzingatia kipao chetu kama Wabunge.

“Tutafanya hivyo kwa nia thabiti ya kuhakikisha kwamba wananchi wanapata maendeleo wanayoyatamani na nchi yetu inapiga hatua zaidi katika nyanja zote,” alisema

Wagombea waliochuana na Mheshimiwa Dkt. Tulia Aackson ni Abdullah Mohammed Said (NRA), Mhandisi Aivan Jackson Maganza (TLP), David Daud Mwaijojele (CCK), Georges Gabriel Bussungu (ADA -TEA), Kunje Ngombale Mwiru (SAU), Maimuna Said Kassim (ADC), Ndonge Said Ndonge (AAFP) na Saadoun Abrahamani Khatib (DP)



 

No comments:

Post a Comment