WELCOME TO TANZANIA NATIONAL ASSEMBLY OFFICIAL BLOG: CONTACT US: P.O.BOX 941 DODOMA, TANZANIA, WEBSITE: parliament.go.tz , FIND US ON FACEBOOK >>> www.facebook.com/bungetz1, FOLLOW US ON TWITTER >>> @bunge_tz.>>>KARIBUNI

Friday, September 2, 2022

WAJUMBE WA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA SHERIA NDOGO WAKABIDHI HOJA ZA MAPENDEKEZO YA KAMATI KWA SERIKALI (OFISI YA WAZIRI MKUU; SERA, BUNGE NA URATIBU)


Kaimu Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Sheria Ndogo, Mhe. Ramadhan Suleiman Ramadhan akiongoza kikao cha kamati hiyo kilichokabidhi hoja za Mapendekezo ya kamati kwa Serikali (Ofisi ya Waziri Mkuu; Sera, Bunge na Uratibu) zilizowasilishwa katika Mkutano wa Saba wa Bunge ili ziweze kupatiwa majibu tukio lililofanyika katika ofisi za Bunge Jijini Dodoma leo tarehe 2 Septemba, 2022

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu; Sera, Bunge na Uratibu, Mhe. George Simbachawene (katikati) akizungumza mbele ya Wajumbe wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Sheria Ndogo wakati wa kupokea hoja za kamati hiyo zilizowasilishwa katika Mkutano wa Saba wa Bunge ili ziweze kupatiwa majibu tukio lililofanyika katika ofisi za Bunge Jijini Dodoma leo tarehe 2 Septemba, 2022, kushoto kwake ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu; Sera, Bunge na Uratibu, Mhe. Ummy Nderiananga



Mjumbe wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Sheria Ndogo, Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile akichangia jambo wakati kamati hiyo ilipokabidhi hoja za Mapendekezo ya kamati kwa Serikali (Ofisi ya Waziri Mkuu; Sera, Bunge na Uratibu) zilizowasilishwa katika Mkutano wa Saba wa Bunge ili ziweze kupatiwa majibu tukio lililofanyika katika ofisi za Bunge Jijini Dodoma leo tarehe 2 Septemba, 2022, Kushoto ni Mjumbe wa kamati hiyo, Mhe. Medard Kalemani


Wajumbe wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Sheria Ndogo wakiwa katika kikao cha kukabidhi hoja za Mapendekezo ya kamati kwa Serikali (Ofisi ya Waziri Mkuu; Sera, Bunge na Uratibu) zilizowasilishwa katika Mkutano wa Saba wa Bunge ili ziweze kupatiwa majibu tukio lililofanyika katika ofisi za Bunge Jijini Dodoma leo tarehe 2 Septemba, 2022


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu; Sera, Bunge na Uratibu, Mhe. George Simbachawene akipokea taarifa ya Mapendekezo ya kamati zilizowasilishwa katika Mkutano wa Saba wa Bunge ili ziweze kupatiwa majibu kutoka kwa Kaimu Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Sheria Ndogo, Mhe. Ramadhan Suleiman Ramadhan tukio lililofanyika katika ofisi za Bunge Jijini Dodoma leo tarehe 2 Septemba, 2022, Kulia ni katibu wa kamati hiyo, Ndg. Mkuta Masoli 

No comments:

Post a Comment