Timu
za Klabu ya michezo za Bunge zimeendelea kufanya vizuri katika michezo ya
Shirikisho la Michezo ya Wizara na Idara za Serikali (SHIMIWI) inayoendelea leo
tarehe 3 Oktoba Mkoani Iringa.
Timu
ya kamba wanawake imeigaragaza timu ya Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo
kwa pointi 2-0 huku timu ya kamba wanaume ikiiburuza timu ya Ujenzi kwa pointi
1-0 wakati wa mchezo uliofanyika katika viwanja vya Chuo Kikuu Kishiriki cha
Elimu Mkwawa.
Nayo
timu ya netiboli imeibuka kidedea baada ya kuibugiza magoli 31 - 16 timu ya
Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum wakati wa
mchezo uliofanyika katika viwanja vya Chuo Kikuu cha Ruaha (RUCU).
Kwa
upande wa timu ya soka ya Bunge imeicharaza goli 2 -1 timu ya soka ya Wizara ya
Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa wakati wa mchezo uliofanyika katika uwanja wa CCM
Samora Mkoani hapa.
Michezo
SHIMIWI inaendelea kutimua vumbi Katika viwanja mbalimbali na inategemewa
kuhitimishwa tarehe 14 Oktoba, 2023, Mkoani Iringa.
No comments:
Post a Comment