Wajumbe wa kamati
ya kudumu ya Bunge ya Miundombinu wakiongozwa na Mwenyekiti wa kamati hiyo,
Mhe. Selemani Kakoso wamepokea na kujadili taarifa ya Wizara ya Ujenzi kuhusu
utendaji wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) kwa kipindi cha Julai - Oktoba,
2023; Mafanikio na Changamoto katika kikao kilichofanyika leo tarehe 19 Oktoba,
2023 katika ofisi za Bunge Jijini Dodoma.
Aidha, kikao hicho
kimehudhuriwa na Naibu Waziri wa Ujenzi, Mhe. Godfrey Kasekenya, Katibu Mkuu wa
Wizara ya Ujenzi, Mhe. Balozi Aisha Amour na Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Majengo
Tanzania (TBA), Arch. Daud Kondoro.
No comments:
Post a Comment