Rais wa Umoja wa
Mabunge Duniani (IPU) na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Mhe. Dkt. Tulia Ackson ameshiriki hafla ya ufunguzi wa Kongamano la 27 la
Maspika na Wenyeviti wa Mabunge ya Jumuiya ya Madola uliofanyika leo tarehe 4
Januari, 2024, Kampala nchini Uganda.
Kongamano hilo
limefunguliwa na Rais wa nchi hiyo Mhe. Jenerali Yoweri Kaguta Museveni.
Kongamano hilo
pamoja na mambo mengine linatoa fursa kwa Maspika kubadilishana uzoefu wa uendeshaji bora wa Mabunge. Katika Kongamano
hilo linaloendelea hadi tarehe 6 Januari 2024, mada mbalimbali zitawasilishwa
na kujadiliwa ikiwemo masuala ya mazingira na mabadiliko ya tabia nchi, masuala
ya jinsia na ushirikishwaji wa vijana pamoja na ujengaji wa misimamo ya pamoja
ya kibunge.
No comments:
Post a Comment