SPIKA DKT. TULIA MGENI RASMI BUNGE MARATHON
·
Ashiriki katika mbio za km 5
Spika wa Bunge, Mhe. Dkt. Tulia Ackson (Mb), mgeni rasmi katika
mbio za Bunge Marathon zilizofanyika tarehe 13 Aprili, 2024 katika Uwanja wa
Jamhuri Jijini Dodoma.
Mbio hizo za Bunge marathon zimehudhuriwa na viongozi mbalimbali
akiwemo Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mhe. Rosemary Senyamule, Katibu Tawala Mkoa wa
Dodoma, Ndg. Kaspar Mmuya, Waheshimiwa Wabunge na Katibu wa Bunge, Ndg. Nenelwa
Mwihambi, ndc.
Lengo likiwa ni kuchangisha kiasi cha Shilingi Bilioni 3 kwa ajili
ya ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Wavulana Bunge.
Huku kauli mbiu ikiwa ni “Shiriki Michezo kwa Maendeleo ya Taifa
Letu”.
No comments:
Post a Comment