Wednesday, November 27, 2024
Wednesday, November 13, 2024
Spika wa Bunge na Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU), Mheshimiwa Dkt. Tulia Ackson amekabidhi nafasi ya Mwenyekiti wa Mkutano wa Maspika kwa Spika wa Kenya katika Mkutano uliofanyika Nairobi, Kenya
Spika wa Bunge na Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU), Mheshimiwa Dkt. Tulia Ackson akizungumza katika mkutano wa Maspika wa Mabunge ya Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki uliofanyika Nairobi Jijini Nairobi nchini Kenya. Katika Mkutano huo, Mheshimiwa Dkt. Tulia alikabidhi nafasi ya Mwenyekiti kwa Spika wa Bunge la Kenya Moses Wetang’ula
Spika wa Bunge na Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU), Mheshimiwa Dkt. Tulia Ackson akipeana mkono na Spika wa Bunge la Kenya Mheshimiwa Moses Wetang’ula mara baada ya kumkabidhi nafasi ya Mwenyekiti wa Mkutano wa Maspika wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki, Mheshimiwa Dkt. Tulia ameshika nafasi hiyo kwa kipindi cha mwaka mmoja.Makabidhiano hayo yamefanyika katika Mkutano wa Maspika wa EAC uliofanyika Jijini Nairobi nchini Kenya
Spika wa Bunge na Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU), Mheshimiwa Dkt. Tulia Ackson wa kwanza kushoto akiwa katika picha ya pamoja na Spika wa Bunge la Uganda Mheshimiwa Anita Among na Spika wa Bunge la Mpito la Sudan ya Kusini Mheshimiwa Jemma Kumba wakati walipohudhuria Mkutano wa Maspika wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki uliofanyika Jijini Nairobi nchini Kenya
Spika wa Bunge na Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU), Mheshimiwa Dkt. Tulia Ackson (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Maspika wa Bunge na Makatibu wa Bunge wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki wakati walipohudhuria Mkutano wa Maspika wa Nchi hizo uliofanyika Jijini Nairobi nchini Kenya
Spika wa Bunge na Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU), Mheshimiwa Dkt. Tulia Ackson (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Maspika wa Bunge wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki wakati walipohudhuria Mkutano wa Maspika wa nchi hizo uliofanyika Jijini Nairobi nchini Kenya
Monday, November 11, 2024
Katibu wa Bunge amekabidhi nafasi ya Mwenyekiti wa Mkutano wa Makatibu wa Bunge wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa Katibu wa Bunge la Kenya
Katibu wa Bunge la Tanzania, Ndugu Baraka Leonard akishikana mkono na Naibu Katibu wa Bunge la Kenya Ndugu Jeremiah Ndombi mara baada ya kukabidhi nafasi ya Mwenyekiti wa Mkutano wa Makatibu wa Mabunge ya Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa Bunge la Kenya. Makabidhiano hayo yamefanyika katika Mkutano wa Makatibu unaofanyika Nairobi Kenya.Katibu wa Bunge la Tanzania, Ndugu Baraka Leonard akiwa pamoja na Naibu Katibu wa Bunge la Kenya Ndugu Jeremiah Ndombi mara baada ya kukabidhi nafasi ya Mwenyekiti wa Mkutano wa Makatibu wa Mabunge ya Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa Bunge la Kenya. Makabidhiano hayo yamefanyika katika Mkutano wa Makatibu unaofanyika Nairobi KenyaKatibu wa Bunge la Tanzania, Ndugu Baraka Leonard akizungumza katika Mkutano wa Makatibu wa Bunge wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki kabla kukabidhi nafasi ya Mwenyekiti wa Mkutano wa Makatibu wa Mabunge ya Nchi za Jumuiya kwa Bunge la Kenya. Mkutano huo wa Makatibu unafanyika Jijini Nairobi Nchini Kenya
Katibu wa Bunge la Tanzania, Ndugu Baraka Leonard (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Makatibu wa Bunge wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki mara baada kukabidhi nafasi ya Mwenyekiti wa Mkutano wa Makatibu wa Mabunge ya Nchi za Jumuiya kwa Bunge la Kenya. Mkutano huo wa Makatibu unafanyika Jijini Nairobi Nchini Kenya.
Wednesday, November 6, 2024
NAIBU SPIKA ZUNGU AONGOZA MAZUNGUMZO KUHUSU MASUALA YA MALENGO YA MAENDELEO ENDELEVU (SDG’S)
Naibu Spika wa Bunge, Mhe. Mussa Azzan Zungu, ameongoza mazungumzo kati ya Wabunge wa Bunge la Tanzania wa Mtandao kuhusu masuala ya malengo ya Maendeleo endelevu (SDG’S) na Wabunge wa Bunge la Kidemokrasia ya Congo wa Mtandao kuhusu masuala ya SDG’S.
Mazungumzo hayo yamefanyika leo tarehe 6 Novemba, 2024 katika Ukumbi wa Spika, Bungeni Jijini Dodoma.
Dhumuni la mazungumzo hayo ni kubadilishana uzoefu kuhusu masuala ya malengo ya maendeleo endelevu ikiwemo kuondoa umaskini, kuleta usawa na kuhakikisha huduma za afya zinamfikia kila mmoja.
Akizungumza katika kikao hicho Mhe. Zungu alisisitiza, Wabunge kuendelee kuunga mkono juhudi za Rais, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kuhusu masuala ya malengo ya Maendeleo endelevu.
Mazungumzo hayo yalihudhuriwa na Balozi wa Tanzania Nchini Congo, Mhe. Said Mshana.
Tuesday, November 5, 2024
Monday, November 4, 2024
Friday, November 1, 2024
Subscribe to:
Posts (Atom)