WELCOME TO TANZANIA NATIONAL ASSEMBLY OFFICIAL BLOG: CONTACT US: P.O.BOX 941 DODOMA, TANZANIA, WEBSITE: parliament.go.tz , FIND US ON FACEBOOK >>> www.facebook.com/bungetz1, FOLLOW US ON TWITTER >>> @bunge_tz.>>>KARIBUNI

Wednesday, November 6, 2024

NAIBU SPIKA ZUNGU AONGOZA MAZUNGUMZO KUHUSU MASUALA YA MALENGO YA MAENDELEO ENDELEVU (SDG’S)
















Naibu Spika wa Bunge, Mhe. Mussa Azzan Zungu, ameongoza mazungumzo kati ya Wabunge wa Bunge la Tanzania wa Mtandao kuhusu masuala ya malengo ya Maendeleo endelevu (SDG’S) na Wabunge wa Bunge la Kidemokrasia ya Congo wa Mtandao kuhusu masuala ya SDG’S.

Mazungumzo hayo yamefanyika leo tarehe 6 Novemba, 2024 katika Ukumbi wa Spika, Bungeni Jijini Dodoma.

Dhumuni la mazungumzo hayo ni kubadilishana uzoefu kuhusu masuala ya malengo ya maendeleo endelevu ikiwemo kuondoa umaskini, kuleta usawa na kuhakikisha huduma za afya zinamfikia kila mmoja.

Akizungumza katika kikao hicho Mhe. Zungu alisisitiza,  Wabunge kuendelee kuunga mkono juhudi za Rais, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kuhusu masuala ya malengo ya Maendeleo endelevu. 

Mazungumzo hayo yalihudhuriwa na Balozi wa Tanzania Nchini Congo, Mhe. Said Mshana.

No comments:

Post a Comment